Nemesis
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 5,462
- 4,364
Hivi Sheria na taratibu za Uchaguzi wa viongozi ndani chama Chadema, haziruhusu mtu kuchukua form mbili au tatu kugombea nafasi tofauti tofauti?..
Je, ina maana mtu anayegombea Uenyekiti haruhusiwi kugombea Ukatibu au nafasi nyingine yaani akishindwa nafasi moja ndio basi imetoka hiyo..
Naomba kuelemishwa kwani yaonyesha wazi kuwa uchaguzi huu ndani ya Chadema umechukuliwa kama ndio kielelezo cha Uchaguzi mkuu wa 2010..
Kwa mujibu wa orodha waliyoitoa hakuna nafasi ya Katibu Mkuu wala Naibu Katibu Mkuu. Nadhani hizo ni nafasi za uteuzi.