Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
Kaka unazidi kulikoroga. Sasa haya ya kukubali dhana ya uwajibikaji wa pamoja ndani ya chama hata kama yeye anaona ni makosa si ndio yaleyale ya wiki iliyopita ya sakata la NEC-CCM Vs Sitta na wenziwe?
mzee hii dhana unaielewa lakini??
 
Ukiamua kuwa mwanachama wa chama cha siasa basi unapaswa kupita katika misingi inayokiongoza chama husika. Pengine ndugu yangu Omarlyas anataka Zitto awe Mwenyekiti wa chama cha wagombea binafsi ambao hawana itikadi, sera wala mwelekeo mmoja.

Ndiyo maana jana wakati akihojiwa na DW Zitto huyo huyo alifikia hatua ya kusema kwamba yeye anaamini katika ujamaa wakati Mbowe anaamini katika ubepari. Je haoni kwamba chama ambacho kingemfaa ni CCM ambacho hadi leo katika maandishi kinadai ni cha kijamaa japo hakiufuati? Hiki ni kichekesho.

Acha niendelee kulikoroga ilimradi tu nausema ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu kiasi gani. Zitto ni rafiki yetu, sawa, ni ndugu yetu, sawa, ni kijana shupavu, sawa, lakini katika hili la uenyekiti wa Chadema, hajapevuka, si kwa sababu ya umri wake kama ilivyopotoshwa na baadhi ya wana JF, bali uchanga wake katika kuzingatia, kuheshimu na kuitekeleza kwa vitendo misingi ya uongozi bora ya ufanyaji kazi wa pamoja, kwa nia moja hata kama ni kwa njia tofauti.
 
Ni jambo la kusikitisha sana kwamba, hivi sasa mtu anapotoa maoni yake ambayo huonekana kuwa tofauti na mawazo ya wengi basi mtu huyo hupewa majina mengi machafu; ametumwa, amehongwa au anajipendekeza

Pole sana kaka. Nadhani umeweka mambo sawa na nimependa sana sehemu nilizoweka alama nyekundu. Watu wamekuwa wakiishi kwa kuzua na kusingiziana na kibaya zaidi baadhi ya watu hufanya hivyo wakijua wanachosema si cha kweli ila hufanya hivyo kujijengea ngome ya KIFISADI.

Umefanya vizuri sana kutoa ufafanuzi kuhusu mahusiano yako na Muhingo. Kuwa na mahusiano na mtu yeyote si uhaini. Kuna watu wana mahusiano na watu ambao hadharani wanarushiana maneno makali makali, kuna watu wana uhusiano wa kusaidiana/kusaidiwa na watu wanaowakashifu, na kadhalika lakini hiyo haina maana kwamba mmoja amebadili msimamo wake ama hata dini kwa upande mwingine. Mimi nina mahusiano na watu ambao hakika hawapendi hata kuona nafanya ninachokifanya sasa na wengine wanatamani hata nisiwepo duniani, lakini sijawahi kuwakwepa nikiamini Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa yote.

Kibanda, umekuwa mwalimu na mwanafunzi wakati wote, HONGERA SANA.
 
Ni wangapi humu ndani wamewahi kuiona Katiba ya CHADEMA?

Katiba hiyo ilivurugwa na Vijana waliojazana Mkao Makuu CHADEMA kwa kuchagizwa na kupigiwa upatu na Kina Zitto. Katiba hiyo isiyoeleweka ndiyo inayoivuruga CHADEMA hivi sasa na kuviza juhudi zote za kukijenga chama mikoani.
 
Kaka unazidi kulikoroga. Sasa haya ya kukubali dhana ya uwajibikaji wa pamoja ndani ya chama hata kama yeye anaona ni makosa si ndio yaleyale ya wiki iliyopita ya sakata la NEC-CCM Vs Sitta na wenziwe?

Ujana ni uthubutu, isingekuwa uthubutu wa Mwalimu hata Tanzania tusingepata uhuru kwa style na wakati ule kwani wapo waliokuwa wakiamini kuwa muda bado, yeye ni mchanga, mvaa makaputura hawezi kuongoza n.k..

omarilyas
Kweli hata mimi naona Kibanda anazidi kulikoroga ile mbaya! Jamaa naona anatuletea mambo ya CCM hapa kwamba haupaswi kuwa na mtizamo tofauti na chama, ni yaleyale ya zidumu fikra za mwenyekiti. Hii inathibitishwa pia na kauli yake kwenye makala kwamba Zitto alitakiwa kwanza aombe ruksa kwa mwenyekiti anayemaliza muda (Mbowe) kabla hajachukua fomu za kugombea. Huu ni mfumo wa CCM kwani rais anakuwa mwenyeketi automatically na hapaswi kupingwa mpaka anapomailza mihula yote miwili ya uongozi....damn! I'm sick!
 
lakini pia tujadili mambo kwa kina,Zitto achaguliwe kuiongoza CHADEMA kwa umadhubuti wake au ni kwa ushabiki tu wa tunaompenda kwa kusema maneno mazito bungeni dhidi ya viongozi wa serikali?

Tujifunze kwa CCM na Makamba wao. Alipokuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, watu walidhani anafaa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, lakini kila mmoja wetu anajua cheo alichopewa ndiyo limekuwa Anguko lake,hapo nadhani ndipo hoja ya Kibanda ilipo.
 
Ni wangapi humu ndani wamewahi kuiona Katiba ya CHADEMA?

Katiba hiyo ilivurugwa na Vijana waliojazana Mkao Makuu CHADEMA kwa kuchagizwa na kupigiwa upatu na Kina Zitto. Katiba hiyo isiyoeleweka ndiyo inayoivuruga CHADEMA hivi sasa na kuviza juhudi zote za kukijenga chama mikoani.
Saidia kuleta Katiba ya Chadema hapa wewe mwenyewe na do high light yale maeneo unayosema hayana maana ama yana utata tuanzie hapo
 
Kweli hata mimi naona Kibanda anazidi kulikoroga ile mbaya! Jamaa naona anatuletea mambo ya CCM hapa kwamba haupaswi kuwa na mtizamo tofauti na chama, ni yaleyale ya zidumu fikra za mwenyekiti. Hii inathibitishwa pia na kauli yake kwenye makala kwamba Zitto alitakiwa kwanza aombe ruksa kwa mwenyekiti anayemaliza muda (Mbowe) kabla hajachukua fomu za kugombea. Huu ni mfumo wa CCM kwani rais anakuwa mwenyeketi automatically na hapaswi kupingwa mpaka anapomailza mihula yote miwili ya uongozi....damn! I'm si

Jamani uthubutu wa kweli siyo uthubutu usiojali majaaliwa wa Thabiti (anayethubutu) bali ni baada ya tafakari ya Kina. Ni ujinga kufikiri hoja ya Kibanda imejaa u-CCM. kusubiri iko kwenye vyama vyote vya siasa duniani. hata Obama mwaka 2004 alikuwa ni maarufu ndani ya Democrat lakini hakugombea.
 
Kweli hata mimi naona Kibanda anazidi kulikoroga ile mbaya! Jamaa naona anatuletea mambo ya CCM hapa kwamba haupaswi kuwa na mtizamo tofauti na chama, ni yaleyale ya zidumu fikra za mwenyekiti. Hii inathibitishwa pia na kauli yake kwenye makala kwamba Zitto alitakiwa kwanza aombe ruksa kwa mwenyekiti anayemaliza muda (Mbowe) kabla hajachukua fomu za kugombea. Huu ni mfumo wa CCM kwani rais anakuwa mwenyeketi automatically na hapaswi kupingwa mpaka anapomailza mihula yote miwili ya uongozi....damn! I'm sick!

Kama mwenyekiti wa chama atakuwa na msimamo tofauti na chama chake basi hatakuwa anakiwakilisha chama bali anajiwakilisha mwenyewe,kwenye chama kuwa na msimamo wa pamoja kwenye mambo ya msingi ni jambo la lazima hasa kwa viongozi wakuu.
 
Nimeisoma makala yangu yote mara mbili mbili na kuihakiki akili yangu na kubaini kwamba pengine kuna aya moja tu ambayo pengine imepotosha dhana nzima iliyokusudiwa.

Hata hivyo ni jambo la kusikitisha kwamba 'The Home of Great Thinkers' inataka kuchafuliwa na Watanzania ambao ni wavivu wa kufikiri na ambao kwao wao furaha ni kuona kukithiri kwa mitikisiko isiyo ya lazima ndani ya vyama vya siasa hususan hivi vichanga vya upinzani.

Ninayo imani kubwa kwa Zitto na pengine ninaujali sana mustakabali wake kuliko ilivyo kwa wengi ambao leo hii wanajifanya wakimtetea na kumpigania kinafiki ili mbele ya safari wapate maneno ya kuinyoshea kidole Chadema, au Mbowe au Zitto.

Sijakatishwa tamaa.

KIBANDA makala yako imesimamia kwa Mbowe hata kama mimi ni mvivu wa kufikiri. umekuwa ukirudia rudia KIJANA HUYU au KIJANA HUYO hii kuonesha kuwa Zitto ni mtoto MDOGO hawezi kitu uenyekiti.

umeenda mbele zaidi kwa kusema kuwa Zitto mentor wake ni Mbowe.hiyo umemvunja kabisa kwani wanachadema wakisoma kama MENTOR anagombea kwanini tusimpe mentor tumpe mtoto AU kijana mchanga?

Umesema kuwa Chadema chini ya DR.Slaa na Mbowe wameipaisha juu hukusema kuwa Zitto akishirikiana na hao wawili wamekipaisha chama.
Zitto amejiunga Chadema wakati Mbowe akiwa hana madaraka. mara nyingi Zitto katoa kauli humu humu JF kuwa wako watu wengi wamemsaidia kufika hapo alipo fika, amemtaja DR.Salim Ahmed Salim lakini hakuwahi kusema kuwa MBOWE ni mentor wake.

Gazeti hili unaloliongoza watu wengi wanadhani ni la Chadema wakati ni la Mbowe. hivyo basi naamini kwa vile gazeti hili linatumiwa sana na wanachadema kama John Mnyika alikuwa akiandikia sana, Kitila MKUMBO,Mwanakijiji na wengi wanaodhaniwa ni wapenzi au makada wa Chadema.

kitendo hicho kimepelekea gazeti lako naamini litakuwa likisomwa kwa umakini na matawi Ya Chadema nchi nzima.makala yako akisoma mtu wa Mtwara mwanachadema ambaye ni mjumbe wa Mkutano mkuu wa Chadema tayari umempa jibu kuwa kura yake aipeleke wapi?

umsema kuwa CCM au Usalama wamekuwa na utaratibu wa kuvuruga vyama ukatoa mifano na kuhitimisha kuwa Zitto kaingia kwenye mtego huo.
Kibanda kama ni kampeni basi tayari umemmaliza Zitto.umeshindwa kutaja mapungufu hata kidogo ya Mbowe kama kukataa kulipa madeni ya Nssf ambapo ni doa kwa kiongozi makini, kuendesha zoezi la kuteua wabunge wa viti maluum kupitia Chadema kwa misingi ya ukabila chini yake Mbowe KAMA mwenyekiti.

Mbowe alishindwa kuweka chombo au baraza la wanawake Chadema wafanye kazi hiyo ya kuchaguana.wakajazwa watu wa familia na wenye mahusiano na mkoa wa Kilimanjaro. ulikuwa na nafasi ya kubalance Story yako.

gazeti hilo hilo ukaweka READ STORY kuwa Zitto azua mjadala na ukaeleza kuwa wazee wa Chadema wamemuomba Mbowe achukue Fomu ya uenyekiti ili akivushe chama, maneno hayo yanatafsiri nzito sana kwa mwanachama wa kawaida wa Chadema kuwa kama wazee wenye chama wamepima na kuona Mbowe anafaa kwanini kura yangu nimpe KIJANA HUYU au Mwanasiasa Mchanga KWA mujibu wa maneno yako.

pia kama Zitto ni mtu wako wa karibu kwanini usimwite au kumtumia email ukamsikia kabla ya kumchafua kwenye gazeti la Mbowe? ok Mbowe umempigia kampeni kupitia gazeti alilokuajiri jee Zitto akasemee wapi?

Kibanda HUKUMTENDEA HAKI ZITTO.

Andika makala nyingine kusahihisha habari hii kwani ukija kujibu hapa huwezi kupata audence kama uliyonayo kwenye gazeti La Tanzania Daima ambalo kama sikosei ni la pili kwa circulation nyuma ya Mwananchi.Kwenye online lina watu wengi sana hilo unalijua. umemchafua Zitto bwana Kibanda.
 
Hapa ndipo tulipofikishwa na waandishi wa aina ya huyu Kibanda. Tatizo waafrika hatupendi challenge tunataka kutukuzwa na kuwa mabwana kila siku. Hii ni mpaka lini jamani. Hebu tubadilike jamani. Zitto ana nafasi na haki ya kugombea uenyekiti kama mtu mwengine. Anguko la kufanya nini????

Unaweza kupata picha watu wa aina ya kabanda ndo wengi hapa nchini ambao upeo wao umeishia kwenye maslahi na ushabiki bila kupima ukweli. Aibu jamani ndugu zangu....
 
Kama mwenyekiti wa chama atakuwa na msimamo tofauti na chama chake basi hatakuwa anakiwakilisha chama bali anajiwakilisha mwenyewe,kwenye chama kuwa na msimamo wa pamoja kwenye mambo ya msingi ni jambo la lazima hasa kwa viongozi wakuu.

Hapa mnaleta maboa ya mtu mmoja kuchagukuwa bila kupingwa kwa kuwa wengine namejitoa. Mwacheni Zitto ajaribu akishidwa next time hata kikwete hakugombea mara moja uraisi
 
Mbowe ana udhaifu wake tena wa hali ya juu sana, lakini siyo kwenye kila kitu. lakini dhamira yake ya kuijenga CHADEMA ni kubwa zaidi kuliko ya Zitto.

Zitto anajifikiria yeye na "akili" zake nyingi na umaarufu alionao kwa sasa. yeye ni Naibu Katibu mkuu wa Chama inakuwaje kwa miezi mitatu mfululizo ashindwe kufika makao Makuu ya chama chake tena kikiwa kwenye mchakato wa kuelekea kwenye uchaguzi wake wa ndani ya Chama?

Kama Katibu, mikakati yake ya kuhakikisha Chama kinaongeza idadi ya viongozi wa ngazi ya serikali za mitaa ikoje?
 
Jamani uthubutu wa kweli siyo uthubutu usiojali majaaliwa wa Thabiti (anayethubutu) bali ni baada ya tafakari ya Kina. Ni ujinga kufikiri hoja ya Kibanda imejaa u-CCM. kusubiri iko kwenye vyama vyote vya siasa duniani. hata Obama mwaka 2004 alikuwa ni maarufu ndani ya Democrat lakini hakugombea.

Obama hakuwa na umaarufu huo unaouzungumzia kuweza kushinda uraisi mwaka 2004,alipata national recognition baada ya speech yake kwenye Democratic National Convention wakati wakimpitisha John Kerry kuwa mgombea uraisi,it was too late.....
 
Mbowe ana udhaifu wake tena wa hali ya juu sana, lakini siyo kwenye kila kitu. lakini dhamira yake ya kuijenga CHADEMA ni kubwa zaidi kuliko ya Zitto.

Zitto anajifikiria yeye na "akili" zake nyingi na umaarufu alionao kwa sasa. yeye ni Naibu Katibu mkuu wa Chama inakuwaje kwa miezi mitatu mfululizo ashindwe kufika makao Makuu ya chama chake tena kikiwa kwenye mchakato wa kuelekea kwenye uchaguzi wake wa ndani ya Chama?

Kama Katibu, mikakati yake ya kuhakikisha Chama kinaongeza idadi ya viongozi wa ngazi ya serikali za mitaa ikoje?

Madai haya nadhani Zitto atakuja kuyajibu maana najua anasoma hizi habari anavuta pumzi.
 
Ukiamua kuwa mwanachama wa chama cha siasa basi unapaswa kupita katika misingi inayokiongoza chama husika. Pengine ndugu yangu Omarlyas anataka Zitto awe Mwenyekiti wa chama cha wagombea binafsi ambao hawana itikadi, sera wala mwelekeo mmoja.

Ndiyo maana jana wakati akihojiwa na DW Zitto huyo huyo alifikia hatua ya kusema kwamba yeye anaamini katika ujamaa wakati Mbowe anaamini katika ubepari. Je haoni kwamba chama ambacho kingemfaa ni CCM ambacho hadi leo katika maandishi kinadai ni cha kijamaa japo hakiufuati? Hiki ni kichekesho.

Acha niendelee kulikoroga ilimradi tu nausema ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu kiasi gani. Zitto ni rafiki yetu, sawa, ni ndugu yetu, sawa, ni kijana shupavu, sawa, lakini katika hili la uenyekiti wa Chadema, hajapevuka, si kwa sababu ya umri wake kama ilivyopotoshwa na baadhi ya wana JF, bali uchanga wake katika kuzingatia, kuheshimu na kuitekeleza kwa vitendo misingi ya uongozi bora ya ufanyaji kazi wa pamoja, kwa nia moja hata kama ni kwa njia tofauti.

Du jamani PRESHA inapandaaa!!!
 
kazi kweli kweli, lakini kibanda ungeweza kuuchambua upungufu wa zitto kwa kubase kwenye fact zaidi (kama unazo) kuliko hisia zako tu, tungekuelewa, lakini si kutoa tu mashambulizi sababu Mbowe kapata mpinzani kwenye uenyekiti. kwa nini wasipewe chance na democrasia ichukue mkondo wake?
 
...ni vema nafasi ya uenyekiti CHADEMA inagombewa na wagombea wawili tena wote wazuri...nadhani hii itabadili fikra za watu kudhani chama ni mwenyekiti kushika hatamu na ikiwezekana atawale hadi akatae au muda wake uishe....

...tutegemee hii itakuwa fundisho kwa ccm mwakani wakubali kupeleka majina mawili yenye ushindani mkutano mkuu kugombea kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama......sio kuleta ujanja ujanja mara kura tatu......ambao ulitumika kupunguza ushindani kati ya salim na kikwete mwaka 2005.....nadhani kura 560 alizopata salim ukijumlisha na kura za mwandosya...ni dhahiri mshindi kama angekuwa kikwete au salim angepita kwa margin ndogo sana na hiii ingeonesha ukomavu wa demokrasia....

GO CHADEMA GO!!!...... Waacheni wagombee ..you will come out strong...nadhani watu hawajamuelewa zito kabwe ..kwa umri mdogo alionao ..anatuma signal ..kuwa yupo tayari kuwa national leader .....mara umri utakapofikia kikatiba...na hii ni moja ya maandalizi.....CHADEMA wana demokrasia ...kama au kuliko CCM ndio maana wanaachiana oungozi kwa amani bila mizengwe...
 
Kwanza napenda kuwafahamisha wachangiaji wa JF kwamba niliandika makala ya uchambuzi (analysis) iliyochapishwa katika ukurasa wa 11 wa maoni na mawazo ya watu binafsi. Baadhi ya watu wamenihukumu kwa kuwa bias wakati yale ni maoni na si habari kama inavyodaiwa na kuelezwa na wachangiaji mbalimbali.

Pili haikuwa lengo langu kuanika udhaifu wa mtu yeyote katika ile makala bali lengo langu lilikuwa ni kumuonyesha Zitto athari za kuitumia ndivyo sivyo haki yake ya kikatiba ya kugombea uenyekiti. Mimi binafsi naamini katika demokrasia lakini pia natambua kwamba demokrasia ikitumika vibaya inaweza kutumika vibaya.

Pengine nilichokisahau ni kuandika pia kwamba, Zitto, Mbowe na wana Chadema walipaswa kutambua kuwa wanakwenda katika uchaguzi wa ndani katika chama chao wakati wakiwa tishio kubwa kwa CCM na katika kipindi kifupi sana kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.

Kwa sababu hiyo basi, wote wanapaswa kuwa makini kuepuka kuzalisha vidonda ambavyo vinaweza kusababisha chama hicho kikawa dhaifu sana badala ya kuwa imara wakati huu. Ni kwa mantiki hiyo nilitumia neno 'anguko' nikionyesha hofu ya kupwaya kwa chama hicho.

Hata hivyo nikiwa mwanahabari, natambua baadhi ya maoni ya wachangiaji wanaojifanya wakimtetea Zitto ni vijana wa CCM ambao tumewasikia mitaani wakisema 'acha Zitto apewe tuwaonyesha jeuri ya CCM'.

Niseme wazi nimekuwa nikiamini siku zote kwamba Zitto ni 'visionary leader' na ambaye kwake yeye hutanguliza maslahi ya chama chake kabla ya yake binafsi. Naamini anaweza akatimiza malengo yake yote mengine ya kisiasa pasipo kuwa mwenyekiti.

Tunaweza kusema lolote tunalolipenda lakini wako watu ambao wanao uwezo wa kujisifu kwamba wameifikisha Chadema na Zitto hapo walipo leo, miongoni mwa watu hao ni sisi 'Wahariri wa Tanzania Daima' ambao siku zote tume-shape ajenda za huyu kijana shupavu.

Nautambua ujasiri wake, nauenzi uwezo wake lakini pia nautambua udhaifu wake kama kiongozi. Anao uhuru wa kukataa au kuukubali ushauri. Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, ndani ya Chadema anaungwa mkono na vijana wajinga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom