Naomba 'conclusions' ziwe kwenye ukweli. Kwamba miezi mitatu sijawa makao´makuu ni uwongo. Viongozi wote wa chama tulikuwa Biharamulo kwenye kampeni mwezi uliopita tu na baada ya hapo kuwa na vikao kadha wa kadha nje na ndani ya makao makuu.
Nadhani sio uungwana kutoa maoni katika masual ambayo huna uhakika na ukweli wake. Tusiwe emotional.
Hakuna kambi ya Zitto wala ya Mbowe katika CHADEMA. Kwa hakika uchaguzi utakwisha na chama kitakuwa imara zaidi. Mimi binafsi sigombei kwa sababu nina chuki na Mbowe au mtu yeyote wa karibu yake. Nagombea kwa sababu ni lazima chama kibadilike na kisonge mbele. Kwanini uchaguzi uonekane ni chanzo cha kuvunja chama? Mazingira ya NCCR ndio mazingira ya CHADEMA? Huu ni upotoshaji tu.
CHADEMA ina historia ya uchaguzi na chama kubaki kimoja. Mwaka 1998 Bob Makani aligombea na Ndesamburo uenyekiti wa Taifa na chama hakikupasuka. Kumekuwa na Matatizo kwamba Mbowe alipoteza makamu wake wawili kwa tofauti za mtazamo ie Dkt. Kabourou na Chacha Wangwe ambae hivi sasa ni marehemu. Hii ni sehemu ya historia ya chama, kwamba katika kipindi cha miaka 5 ya uongozi wa awamu ya tatu ya CHADEMA Makamu 2 wawili wa wenyeviti waligombana na Mwenyekiti na mmoja kuondka na mwingine kusimamishwa na kisha kufariki dunia. Kipindi hicho hicho pia Naibu katibu Mkuu Bara Akwilombe akaondoka.
Vinginevyo kuna maisha baada ya uchaguzi. Sote Mbowe na Mimi tutakiwa kuendelea kujenga chama baada ya uchaguzi. Sasa woga wote huu unatoka wapi na kuanza kuweka mahitimisho hasi? Baada ya uchaguzi kama nikishindwa nitaendelea kuwa Mbunge wa chama, Katibu wa Wabunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama. Baada ya uchaguzi Mbowe akishindwa ataendelea kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kama ilivyo Mtei na Makani. Sote hatuna ujanja zaidi ya kujenga chama na kukiimarisha.
Baadhi ya Watanzania tuna tabia ya mawazo mgando kwamba uchaguzi ni chuki, kutukanana nk. Sasa mkishatukanana, mtajenga tena chama baada ya uchaguzi? Cheo ni dhamana inasema moja ya ahadi ya mwana TANU...............