Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
Halisi

Nakubaliana na mtazamo wako. Uandishi wa Kibanda umekuwa kama mtu anayetoa hukumu. Yale sio maoni, kwani yangekuja kwa mtindo wa swali.

Suala kubwa hapa sio umri, bali uhusiano wa Zitto na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA. Inaonekana yapo mambo mengine makubwa zaidi ya haya tunayoyasikia. Kwa bahati mbaya, hali hiyo inapojitokeza uwezekano wa kuvuka salama ni mdogo sana. Kidudu mtu huweza kujipenyeza kwa urahisi sana.
 
kwa maoni yangu hii hatua ilibidi Zitto ajadili kichama na wakuu wao waangaie umuhimu wa yeye kusimama kama con ya chama,lakini kama amekurupuka u,basi zitto atakuwa na agenda ya siri ya kukidhofisha chama kuelekea 2010,na hii sum itakuwa imemwagwa from ccm,wakielewa wazi kuwa Zitto akikoroga tu na wanachama kibao wanajikoroga na kuondoa imani kwa wananchi,wat wa type hii wapo jamni.ameshindwa nini kukubaliana na wenzake?labda wamemtuma siamini anawza kujiharibia namna ii.kama ndivyo hafai na ana uchu wa madaraka pia.
 
Kibanda ni kituko! Zitto katangaza nia ya kugombea tu na haina maana ndio kishakuwa Mwenyekiti.

Umefika wakati tuache busara za wajumbe waamue nani awe Mwenyekiti wao kutokana na uwezo na historia zao. Haya mambo ya kutishana na kukatishana tamaa yanatokea wapi?

Umri? my foot! mbona amekuwa mbunge kijana na kaonyesha uwezo mkubwa ndani ya Bunge kuliko kina Kingunge wenye umri 3 times umri wa Zitto.

Hakuna alie zaliwa Mwenyekiti, kama uwezo anao na wajumbe wakaona hivyo apewe. Nyerere alipokuwa waziri mkuu wa kwanza baada ya Uhuru alikuwa kijana zaidi kuliko Zitto.

Kibanda aseme kweli yake badala ya kuzunguka mbuyu kuwa katumwa na bosi wake kumkatisha tamaa Zitto hakuna zaidi.

Ushindwe Kibanda!
 
Hamna lolote mnasurport CHADEMA Kwa sababu ya UDINI uliowajaa. Na KINA KIBANDA na wenzake wanao surport CHADEMA wanampinga ZITTO kwa sababu ni MUISLAM Tena Muislam mzuri kwa imani yake. Kwa iyo kanisa na baadhi yao akina kibanda wanmuona kama KIRUSI.

nani hajui kama CHadema CHAMA KATOLIKI NA KINAUNGWA MKONO NA KMAKANISA 100 percent.
WAISLAAM AMKENI MSIKUBALI KUWA NGAZI SEKTA ZOTE WANATAKA WAWE WAO(WAKRISTO) AKIWEPO MUISLAAM HAFAI.

BADILIKENI NCHI YETU SOTE TUIFANYE TANZANIA LAND OF OPPORTUNITY KILA MWENYE UWEZO APEWE NAFASI KUTOA MCHANGO WAKE KUENDELEZA NCHI

KWAO WAO WAISLAM HAWAJASOMA TUUUUUUUU!


Kweli huyu ni great thinker??? I doubt!!!
 
Wakati atakapokuwa akiyatafakari hayo, Zitto anapaswa kuyarejea maneno aliyoyatoa Rais Jakaya Kikwete siku alipoteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM pale Dodoma, Mei mwaka 2005, alipokiri yeye mwenyewe kwamba lilikuwa jambo jema kwake kuukosa urais mwaka 1995.

Naliona anguko la kihistoria la Zitto.

Hata Kikwete alipokosa uraisi mwaka 1995 alichukua form akagombea na kukosa na ndipo aliporudi tena. Kwa hiyo anachofanya Zito sio cha ajabu
 
Zitto: Nina sababu za kutaka kumng'oa Mbowe


*MWENYEWE AMKARIBISHA ULINGONI WAPAMBANE


Na Boniface Meena

NAIBU katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema ana sababu za msingi za kuamua kuuwania uenyekiti wa chama hicho, huku mwenyekiti wake Freeman Mbowe akimkaribisha katika kinyang'anyiro hicho.

Zitto, ambaye yuko nchini Ujerumani kikazi, aliiambia Mwananchi jana kwamba, ameamua kuingia katika kinyang'anyiro cha uenyekiti kupambana na Mbowe kwa lengo la kuandaa chama kuchukua dola.

Lakini Mbowe, ambaye uongozi wake umeifanya Chadema kuwa tishio kwa chama tawala na upinzani, alisema anamkaribisha mwanasiasa huyo kijana katika kuwania nafasi hiyo, akisema uamuzi huo ni haki ya kila mwanachama wa chama hicho kugombea nafasi yoyote kama ana sifa.

"Sina mengi ya kusema; kama alivyosema Dk Slaa (Willibrod) kila mwanachama anaruhusiwa kugombea nafasi yoyote, hivyo sina tatizo na Zitto kuwania nafasi hiyo," alisema Mbowe.

Zitto, ambaye ameibukia kuwa mwanasiasa maarufu mwenye uwezo wa kujenga hoja, alisema anatambua kazi nzuri ambayo Mbowe ameifanya katika chama, lakini akaongeza kuwa, uamuzi wa kupambana naye unalenga kukiandaa chama kuchukua dola katika chaguzi zijazo.

"Ninajua kazi ambayo Mwenyekiti Mbowe kaifanya kwenye chama. Ni kazi kubwa sana na hata mimi kuwepo kwangu katika siasa, Mbowe amechangia sana, alisema Zitto ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32.

"(Mbowe) Ni kiongozi ninayemheshimu na kwa kweli anakipenda sana chama na amejitolea sana kwa ajili ya chama."

Hata hivyo, Zitto, ambaye aliwahi kukaririwa akisema nia yake siku moja ni kushika nafasi ya juu ya uongozi katika nchi akimaanisha urais, alisema ni lazima chama kionekane sasa kipo tayari kuchukua dola.

"Mbowe ni kiongozi mzuri sana wa chama ambacho kipo katika siasa za upinzani. Watanzania sasa ni lazima wapewe sera mbadala za kuonyesha kuwa tunaweza kutawala. Jambo la msingi kuliko vyote ni kuona chama kinabaki kimoja na imara. Hili ndilo lengo langu," alisema.

Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini ambaye alijiunga na Chadema akiwa na umri wa miaka 16, alisema ingawa katika uongozi wa Mbowe amekuwa na mafanikio, chama hicho kimekuwa katika hali ya kufukuza wanachama.

"Tumefukuza sana wanachama. Haiwezekani tukajenga chama cha kufukuzana tu. Ni lazima tukubali kutokubaliana," alisema.

"Kugombea kwangu ni wito wa kurejesha umoja katika chama wakati tunajiandaa kuchukua dola. Uchaguzi Mkuu wa 2010 utakuwa wa kihistoria kwa kuwa kwa uzoefu wangu unaweza kulazimisha serikali kuundwa na waziri mkuu ambaye hatoki CCM. Hatuwezi kwenda huko tukiwa divided (tumegawanyika)."

Akielezea mafanikio ya Mbowe, Zitto alisema mwenyekiti huyo ameiwezesha Chadema kutoka kupata asilimia tatu ya kura katika uchaguzi wa mwaka 2000 mpaka asilimia 8 mwaka 2005.

"Tunamshukuru kwa kukiimarisha chama chetu. Sasa ni wakati wa chama kuelekea kushika dola. Lazima kukiandaa chama kushika dola," alisema Zitto.

"Hiyo ndio kazi ambayo nimeombwa kuifanya na wana-Chadema mikoani na wilayani. Hii ndio kazi ambayo kwa moyo mzito nimekubali kuifanya."

Mbowe, 48, hakutaka kuzungumzia kwa jina uamuzi wa naibu katibu wake kugombea nafasi ya uenyekiti ambayo imekuwa ikipata mbadala bila ya upinzani mkali.

Mbowe ni mwenyekiti wa tatu wa chama hicho akifuwafuatia waziri wa zamani wa fedha, gavana na muasisi wa Chadema, Edwin Mtei; na baadaye naibu gavana wa zamani, Bob Makani. Wenyeviti hao waliachia madaraka kwa hiari yao.

Wakati uamuzi huo ukiashiria mpambano mkali baina ya wawili hao, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu amechukua fomu kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti.

Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, katika nafasi hiyo, Profesa Baregu anachuana na Maulida Anna Komu na Mbunge wa Mpanda Kati, Said Amour Arfi.

Alisema hadi jana, ambayo ilikuwa siku ya mwisho ya kurudisha fomu hizo, watu 33 walikuwa wamejitokeza kuwania uongozi katika Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bawacha), 33 Baraza la Vijana (Bavicha) na 13 Baraza la Wazee.

"Kikao cha wazee wa chama kitakaa Agosti 29 mwaka huu kupitia fomu za wagombea," alisema Dk Slaa.

Kwa mujibu wa Dk Slaa ili kutaka haki itendeke chama kimeamua kusimamisha uchaguzi wa ngazi ya mkoa katika Mikoa ya Mara na Mbeya kutokana na harufu ya rushwa, huku ikisimamisha chaguzi za Arusha na Manyara kwa sababu mikoa hiyo inaendelea kujikongoja.

Katika tukio jingine, Dk Slaa jana alimkabidhi kadi ya uanachama wa Chadema aliyekuwa katibu wa itikadi na uenezi wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hiyo, Selasini alisema, ameamua kufanya hivyo ili kuendeleza mapambano ya kisiasa kupitia chama hicho ambacho alisema kimeonekana kuwa na nia ya dhati kuwafikia wananchi.

Alisema kuhamia kwake Chadema kutampa fursa ya kuwania ubunge wa jimbo la Rombo kama chama kitampitisha ili aweze kupambana na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Basil Mramba.
 
Jamani kwani kuna kitu gani cha kushangaza?

Zitto alishatueleza huko nyuma (hapa jamvini JF) nia yake ya kutaka kuwa Rais wa nchi hii, i believe uamuzi wake wa sasa ni katika kuanza na kukamilisha nia yake hiyo (hata kama itachukua miaka 15 ijayo).......keep it up Zitto, no one should stop you from working to achieve your goals......all the best
 
Jambo la kwanza kama nilivyosisitiza, Kwa Zitto kugombea ni kitu kizuri kwa sababu anazo sifa zote na hata kumshinda aliyepo kama alivyo Dr. Slaa.

Ila kugombea ni jambo moja na kushinda ni jingine.Kwa maoni yangu, Zitto lazima ashinde ili jahazi livuke salama.Kama Mbowe analiona hili, akiamua kuwa mstaarabu, ni vema akamfagilia njia Zitto apite jahazi lisonge mbele.

Ila pia lazima tukubali, Zitto ana guts za ajabu sana. Haya sio maconfo ya kawaida, lazima Zitto nae anayo ajenda yake na uamuzi wake kugombea ndio maana amegombea kwa stail aliyotumia.Ameamua akatafuta ushauri angeshauriwa asigombee, ili kuepuka kushauriwa kinyume cha dhamira yako, ni vizuri kutimiza matakwa ya dhamira yako na kusubiri matokeo.Hiki ndicho kipimo kizuri sana cha demokrasia ndani ya chama.

Kama Zitto kaamua kugombea ili kutest zali, huku akijua Chadema kina wenyewe na wenyewe ndio wale wale, basi atatupwa nje na baada ya uchaguzi, bunge likishavunjwa, huyoo, atajitimkia zake kama Prof. Safari na CUF.

Kama hana ajenda yoyote, akishindwa anakubali hiyo ndio demokrasia, atabaki kuwa mwana chama safi na mtiifu wa Chadema na kusubiri kurejea Bungeni Dodoma.

Demokrasia Idumu.
 
Pasco

The Following User Says Thank You to Pasco For This Useful Post: Zitto (Today)

Kumbe Mheshimiwa Zitto yupo na anachungulia mabandiko na hoja zetu ni hivi punde katoa shukrani kwa Pasco kwa bandiko lake.

Mhe. tunaomba utoe majibu ya baadhi ya mabandiko watu wana kiu ya kujua mengi kutoka kwako
 
Last edited by a moderator:
The Following User Says Thank You to Pasco For This Useful Post: Zitto (Today)


Kumbe Mheshimiwa Zitto yupo na anachungulia mabandiko na hoja zetu ni hivi punde katoa shukrani kwa Pasco kwa bandiko lake.

Mhe. tunaomba utoe majibu ya baadhi ya mabandiko watu wana kiu ya kujua mengi kutoka kwako

:


Alishajibu toka jana usiku kwa bahati mbaya wengine tulikua hatujasoma na hapo juu nimeweka. Amejibu kifupi sana lakini ni maneno mazito mno tumpe nafasi.

alisema



Quote:


Democracy at work in CHADEMA............. chama hakitavunjika, kitamaliza uchaguzi kikiwa imara kabisa. tukumbatie demokrasia na tusiihofu.
 
Last edited:
Zitto
Muachie uenyekiti Slaa.Wewe subiri upitishwe kuwa katibu.Msianze fujo halafu mkaiparaganyisha chadema

Dr. Slaa hagombei uenyekiti, kwahiyo wanaochuana ni Zitto na Mbowe, pia ni haki yake kikatiba.
 
Chadema this your golden chance to become born again party.

Ni fursa kujikwamua kwenye kashfa inayowanyemelea

1. Christian party
2. Chama cha northern ( especially- kilimanjaro , arusha & manyara)
3. Chama chenye kuheshimu sana influence ya kichaga

i call upon you chadema members, kipeni sura ya kizalendo halisi chama chenu, utaifa na kuwa chama mbadala ambacho kiko tayari kuiongoza nchi yetu pindi sisi watz tutakapojiridhisha kuwa ccm yetu inapaswa kupumzishwa.

Hilo litawezekana tu kama mtajiweka wazi na safi juu ya hayo matatu niliyoyasema.

"viva tanzania"
 
na ninyi bana!hivi huwa hamsomi thread za watu?mbona mnarudia rudia mambo?
 
jamani kugombea uongozi ni njia rahisi kabisa ya kueleza umma msimamo wako au kuweza kuleta mabadiliko ambayo unayaona ni muhimu kwa chama chako. Ukufwatilia kwa mfano Nadar aligombea na alijua kabisa kuwa kuwa htaweza kushinda bali aligombea ili mawazo yake yaweza kusikika. Wote tunajua alichofanya Nadar kwa Al (thanks God! we couldn't afford 12 years of liberals in WH) lakini ameweza kuzishape agenda zake za kilibelari.

Zitto anagombea Chadema ili kuweza kutoa mawazo mbadala na kukuza demokrasia. Huu uchaguzi wa chadema ulikuwa unapita tu before zitto kujitokeza kugombea lakini sasa ni mijadala kila sehemu na hii ni nzuri kwa chadema kwani kinahitaji watu wafuatilie huu uchaguzi kwa karibu.

Analyst wengi walidai kuwa ule mchuano wa Hillary na barack ungekimaliza chama lakini haikuwa hivyo bali ulizidi kukiimalisha chama hasa upnde wa media ambako wakati mgombea wa Republican alikuwa ameshaanza kulipia coverage zake hawa wakawa wanaenjoy free coverage. Zitto kugombea ni kitukizuri sana na tunamwomba afanye kampeni nzuri ili nae mbowe aweze kufanya hivyona kufanya wangombea kuwa serious.

nani anasahau kuwa uchaguzi wa mwaka 2005 hata debate ya maraisi haikuweko? si kwa sababu ya huu ujinga wa kupitisha mtu bila ya challengies zozote na unaona sasa matunda yake? kumbe debate ingesaidia sis kujua nani yeye kazi yake ni kucheka au kusikiliza issue na kuzifanyia kazi.

Mimi naamini kabisa kuwa zitto hana nia mbaya kwa kuamua kuchukua hii hatua ukiwa na IQ normal unaweza tu ukamtizama mtu na kuweza kumjua nini anawaza na msimamo wake . kuna tofauti kubwa kati ya zitto na tambwe hiza au guninita na ziko wazi kwa yale wanayoyaongeao, kumbuka kuwa kile kimtokacho mtu ndicho kimjaacho.

Zitto siyo mdogo Clinto alipokuwa na umri kama wa zitto alishakuwa na majukumu mazitto kuliko haya anayotaka kuyafanya zitto. ndiyo maana alipofika umri wa miaka 42 alikuwa rais mzuri ( oooh yes centrist na siyo leftist kama BO).

Zitto kwa kugombea umefanya jambo zuri sana kwanza kukitangaza chama ( free coverage guaranteed mpaka uchaguzi upite) na pili utafanya uchaguzi uwe wa ushindani na siyo wa anayemtaka mwenyekiti aseme ndiyoooooooooooooooooooo na siye mtaka aseme hapana!
 
Sajo,

Tanzania Daima ni mali binafsi ya Freeman Mbowe!

Bantu,

Mimi na wewe tunafahamu kwamba Tanzania Daima ni mali binafsi ya Mtuhuru lakini jopo la Watanzania wanachofahamu ni kwamba hilo ni gazeti la Chadema na si mali binafsi ya Mwenyekiti wa Chadema. Ni gazeti la Upinzani. Utata unaanzia hapo.
 
Hamna lolote mnasurport CHADEMA Kwa sababu ya UDINI uliowajaa. Na KINA KIBANDA na wenzake wanao surport CHADEMA wanampinga ZITTO kwa sababu ni MUISLAM Tena Muislam mzuri kwa imani yake. Kwa iyo kanisa na baadhi yao akina kibanda wanmuona kama KIRUSI.

nani hajui kama CHadema CHAMA KATOLIKI NA KINAUNGWA MKONO NA KMAKANISA 100 percent.
WAISLAAM AMKENI MSIKUBALI KUWA NGAZI SEKTA ZOTE WANATAKA WAWE WAO(WAKRISTO) AKIWEPO MUISLAAM HAFAI.

BADILIKENI NCHI YETU SOTE TUIFANYE TANZANIA LAND OF OPPORTUNITY KILA MWENYE UWEZO APEWE NAFASI KUTOA MCHANGO WAKE KUENDELEZA NCHI

KWAO WAO WAISLAM HAWAJASOMA TUUUUUUUU!
Naona unakusudia kuvuruga mada. Watu wanajadili mustakabali wa nchi hapa siyo misikiti na makanisa. We ndo unajithibitisha kuwa umejaa udini, ndg yangu ukiendelea hivyo utatuchelewesha safari yetu. Naamini unaweza kubadilika hata kama umeshakuwa.
 
Jamani hebu mbona tuna hofu kiasi hiki kumbe huyu Zitto ni tishio kiasi hiki? Maskini zile ndoto za CHACHA Wange zimeanza kumuandama Zitto, ninajua Zito utaweza na Pia utakuwa M/Kiti wa CHADEMA.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu kinusuru Chama cha Chadema na hawa Mafisadi.
 
Huyu kibanda katumwa na Mbowe,Zitto angalia usijepata ajali bure

FL,

Sidhani kama ni sahihi kusema Kibanda katumwa na Mbowe kutoa makala hii, kujaribu kuhamishia mjadala kwa Mh.Mbowe. Tungejaribu kuangalia historia ya huyu jamaa (Kibanda)tujue amekuwa na mtazamo gani juu ya ushiriki wa Mh.Zitto kny siasa za Tanzania. Pia tumsikilize Mh.Mbowe tuone anatoa comments gani juu ya hili, ndipo tunaweza kucomment vizuri on this!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom