Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
Hivi Sheria na taratibu za Uchaguzi wa viongozi ndani chama Chadema, haziruhusu mtu kuchukua form mbili au tatu kugombea nafasi tofauti tofauti?..
Je, ina maana mtu anayegombea Uenyekiti haruhusiwi kugombea Ukatibu au nafasi nyingine yaani akishindwa nafasi moja ndio basi imetoka hiyo..
Naomba kuelemishwa kwani yaonyesha wazi kuwa uchaguzi huu ndani ya Chadema umechukuliwa kama ndio kielelezo cha Uchaguzi mkuu wa 2010..

Kwa mujibu wa orodha waliyoitoa hakuna nafasi ya Katibu Mkuu wala Naibu Katibu Mkuu. Nadhani hizo ni nafasi za uteuzi.
 
Kibanda ametoa maoni yake binafsi, ni mbaya kwa mwandishi wa habari kuwa biased kiasi hiki. Tueche demokrasia ichukue mkondo wake.

Kabisaaaaa, na nasema KIBANDA NI MPUUUZI SANA ndio nimesema MPUUZI na wala sikutegemea mtu mwenye ujuzi na uzoefu wa kazi yake kuwa biased hivi.

Ila kwa kweli lazima tukubali sisi wananchi bado ni wanafki sana na tunadanganyika sana na vijisenti vidogo vidogo bila hata kuangalia atahri zake kwa taifa zima.

Mimi binafsi nasema issue ya umri sio tatizo kabisa na katika hoja zangu zilizopita nilisisitiza sana vijana kujipanga na kuwa na fikra endelevu kuanzia hali ya binafsi mpk kitaifa napenda sana kumpongeza Mhe Zitto Kabwe na Mungu amzidishie na ikiwezekana ashinde kwa vigezo alivyonavyo maana sasa hivi tungependa kuona mawazo mapya ndani ya siasa za wapinzani na sio dead log ambazo zinazidi kutupeleka ambako hata hatujui wapi tunakwenda
 
Nemesis,
Mkuu nimekupata, sasa inakuwaje ktk nafasi au niseme orodha zilizotolewa. Mtu anaruhusiwa kugombea nafasi zaidi ya moja au!..
 
Kibanda kwenye makala hii umekuwa upande mmoja wa Mbowe,unasema kuwa Zitto ni kijana na unakubali amesimamia mambo makubwa ya kisiasa nchini, pia amekuwa naibu Katibu mkuu kwanini ashindwe kusimamia kazi ya uenyekiti wakati Mtendaji mkuu wa chama ni katibu mkuu? Zitto awe na subira kwani hujui kuwa muda uliopo ndio wako na muda ujao si wako? una maana vijana ni taifa la Kesho? JK amekuwa naibu Katibu mkuu wa CCM akiwa na miaka 25.

amekuwa naibu waziri kwenye wizara nzito ya nishati akiwa na miaka 33.kama ZITTO ana SHINE bungeni kwanini ashindwe uenyekiti wa Chadema?
mzee hizi data umezipata wapi?profile inaonyesha amezaliwa mwaka 1950 na alikuwa naibu waziri mwaka 1988...kwenye profile inaonyesha kuwa alikuwa Executive Functionary/Officer wa TANU ndo unaibu katibu mkuu?
anyways, inawezekana source za profile ya mkulu zinatofautiana.
 
Pole sana Kibanda maana wakati mwingine the name can 100% resemble kitu hicho.Utasikia mtu anaitwa Chuki, Sikujua, Mateso , Tabu na akawa na mashida sana .Kibanda yeye kama jina lake amekuwa kweli hajataka kugeuka aone upende mwingine .

Kibanda lazima atambue kwamba kama Mbowe aliamua kukaa pembeni hadi kaombwa hivyo hana shida maana yeye ni mwanachama tu na atafurahi akishinda na akishindwa pia atafurahi .Mbowe ana vision na ni mwanachama wa Chadema siamini kwamba ana zengwe kwa jinsi nimjuavyo.

Kumwita Zitto mtoto ni upuuzi mkubwa na mawao yake Kibanda hayana tofauti na Kingunge na mafisadi wenzake juu ya waraka wa wakatoliki .Wanasema mbaya lakini hawasemi mtari upi unaufanya kuwa mbaya .

Wanaodhania kwamba Zitto anaweza kuuza Chama nao wana haki ya maoni yao lakini Zitto alisha sema hana bei .Katokea mbali na kasulubiwa sana na CCM kuanzia huko nyuma na alisha iona hakuingia hawezi kuingia akawa mpuuzi kama Kabourou ambaye ni kama Bundi sasa penye ndege .

Lazima tuwe wastaarabu hata watu hukubaliani nao wakifanya vyema lazima kuwapa haki yao .Zitto ana utamaduni huo kama wangu .Kampa Chenge asante kwa kumsaidia kumwelewa na akapata alicho kipata .JK kuwa karibu na Zitto ubaya uko wapi ? Zitto kaharibu wapi kwa ukaribu huo ?

Mimi nadhani yeyote kati ya Zitto ama Mbowe akichukua Chama tena ni sawa na wote 2 hawatakuwa nanongwa Zitto atakuwa na nafasi zaidi kama atashindwa .

Uoga mkubwa uko kwa CCM kama Zitto atachukua ataamsha ari ya Watanzania kuona CCM kuna shida na watu kubadilika kwa kasi kubwa ndiyo maana hawalali sasa CCM na kueneza fitina. Mie ningalipenda kuona changes ili Chadema izidi kuwaka na neno kuna Ukabila Chadema Chama cha wachaga hata kama si hivyo ufe tuone CCM watakuja na lipi .Zitto atakuwa ni kiongozi wa Chadema hatakuwa mwenye Chadema na kama tutaona hafai akiwa madarakani kuna Vikao anabadilishwa kuna ubaya gani .Acheni majungu Zitto ingia na Mbowe ingia ndiyo maana Chadema ni Chadema leo .

Kibanda mwacheni alale kwenye kibanda chake ataamka baadaye .
 
Nemesis,
Mkuu nimekupata, sasa inakuwaje ktk nafasi au niseme orodha zilizotolewa. Mtu anaruhusiwa kugombea nafasi zaidi ya moja au!..

Mkuu hili silijui, labda akina Mnyika au Wakuu wenyewe (Dr. Slaa au Zitto) kama wanaweza kutujibu kwa haraka.
 
Mweshimiwa aliyetoa mawazo yake kama ameona kikwazo ni Umri basi atakua amekosea Hata siku moja umri sio tatizo cha masingi ni (Vision,Policy)direction ambayo Zitto anataka chama kieleke ndio uwe mjadala na sio Umri.

Kwa mtazamwo wangu mimi naona mchango wa Zitto kitaifa hautakua mkubwa akiwa Mwenyekiti wa Chadema ama alivyo mbunge now.

Country first Party next
 
Baadhi ya watu wanafikiri Siasa ni "Chuki"...Watz hawana culture hio..Zitto kuwashukuru hao Mafisadi haimaanishi basi nae fisadi...Kutetea Ununuzi wa Mitambo ni sababu ya Msingi, kila mtu anafikra zake kupima SIASA vs Hali ya Uchumi wakati husika. Ndio maana watu hukaa vikao....ktk Vikao kuna kutafautiana na ndio Ubinaadamu...!!!..otherwise turudi ktk system za Udikteta!!!

Nafikiri Mbowe kitendo chake cha Kukimbia/Kushindwa Masomo HULL imesend a wrong signal kwa Wasomi...!!! Ieleweke kuwa Kukua kwa chadema sio kazi ya mtu mmoja, ni timu nzima..hata wapiga debe ndani ya JF....!!!Kumpata "Mkandara" kujiunga na Chadema si kazi ndogo...ni wapambe tu wa Chadema ndani ya JF wamemvuta!!!

Kitila Mkumbo alikuwa na nafasi nzuri sana, naona yeye kaogopa kuonekana Mpinzani wa Mwenyekiti wa Sasa au Tuseme ana linda Ugali wake kule UDSM...!!

Kitendo cha Zitto ni kitendo cha Kijasiri sana, kwa mtu wa kawaida asingeweza chukua maamuzi mazito kiasi hicho....!!!

Hivi akitokea Mtu CCM wa Kupambana na JK itakuwaje....? na Ndio maana wazee akina Malecela wakasema kabisa ni utamaduni wao kuachiana kipindi cha miaka 10...Labda watokee wazee wa Chadema nao waseme kuwa Zitto kaa pembeni sie tunautaratibu wetu hadi tumuulize M/Kiti wa sasa kama anakitaka cheo au Hakitaki...!!!
 
Pasco,unafikiri kwa nini Zitto,of all the wadau wa jf wanaofuatilia hii thread,kakushukuru kwa post yako hii?

kaka bishanga...ni utashi tu...may be muda wake pia mdogo haumruhusu kupitia yote...Maana hapa kuna thread kama 2-3 za Zitto pekee yake za Jana na Leo tu...sasa akianza kufuatilia zote na atoe thanks...basi itakuwa kazi sana...!!!

By the way tufanye tunayoyaweza usikae kusubiria "Ahsante-Thanks za JF" km wakaa ktk keyboard ukisubiri thanks hayo ni matatizo yako binafsi...!!!
 
- Wabongo kwa siasa bwana sijui tulilogwa na nani, I mean what is the ishu hapa? Zitto amechukua fomu kwa sababu anataka kua Mwenyekiti kisa na mkasa haridhiki na kazi ya Mwenyekiti wa sasa, that is the bottomline.

- Amevunja sheria? Hapana. Je anamchukia Mwenyekiti wa sasa wa Chadema, hapana, ni nothing but Demokrasia at work, sasa tuiache i-play itself badala ya kujaribu kupandikizia mbegu za uadui baina yake na Mwenyekiti wa sasa Chadema, taifa haliwezi kunufaika na uadui usio na masilahi yake kama huu tunao ujaribu kuupandikiza hapa.

Respect.


Field Marshall Es!
 
- Haya ni maneno ya Zitto toka blog moja huko pembeni, saafi sana hebu msome kidogo:-


Naomba 'conclusions' ziwe kwenye ukweli. Kwamba miezi mitatu sijawa makao´makuu ni uwongo. Viongozi wote wa chama tulikuwa Biharamulo kwenye kampeni mwezi uliopita tu na baada ya hapo kuwa na vikao kadha wa kadha nje na ndani ya makao makuu.

Nadhani sio uungwana kutoa maoni katika masual ambayo huna uhakika na ukweli wake. Tusiwe emotional.

Hakuna kambi ya Zitto wala ya Mbowe katika CHADEMA. Kwa hakika uchaguzi utakwisha na chama kitakuwa imara zaidi. Mimi binafsi sigombei kwa sababu nina chuki na Mbowe au mtu yeyote wa karibu yake. Nagombea kwa sababu ni lazima chama kibadilike na kisonge mbele. Kwanini uchaguzi uonekane ni chanzo cha kuvunja chama? Mazingira ya NCCR ndio mazingira ya CHADEMA? Huu ni upotoshaji tu.

CHADEMA ina historia ya uchaguzi na chama kubaki kimoja. Mwaka 1998 Bob Makani aligombea na Ndesamburo uenyekiti wa Taifa na chama hakikupasuka. Kumekuwa na Matatizo kwamba Mbowe alipoteza makamu wake wawili kwa tofauti za mtazamo ie Dkt. Kabourou na Chacha Wangwe ambae hivi sasa ni marehemu. Hii ni sehemu ya historia ya chama, kwamba katika kipindi cha miaka 5 ya uongozi wa awamu ya tatu ya CHADEMA Makamu 2 wawili wa wenyeviti waligombana na Mwenyekiti na mmoja kuondka na mwingine kusimamishwa na kisha kufariki dunia. Kipindi hicho hicho pia Naibu katibu Mkuu Bara Akwilombe akaondoka.

Vinginevyo kuna maisha baada ya uchaguzi. Sote Mbowe na Mimi tutakiwa kuendelea kujenga chama baada ya uchaguzi. Sasa woga wote huu unatoka wapi na kuanza kuweka mahitimisho hasi? Baada ya uchaguzi kama nikishindwa nitaendelea kuwa Mbunge wa chama, Katibu wa Wabunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama. Baada ya uchaguzi Mbowe akishindwa ataendelea kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kama ilivyo Mtei na Makani. Sote hatuna ujanja zaidi ya kujenga chama na kukiimarisha.

Baadhi ya Watanzania tuna tabia ya mawazo mgando kwamba uchaguzi ni chuki, kutukanana nk. Sasa mkishatukanana, mtajenga tena chama baada ya uchaguzi? Cheo ni dhamana inasema moja ya ahadi ya mwana TANU...............
 
- Haya ni maneno ya Zitto toka blog moja huko pembeni, saafi sana hebu msome kidogo:-

Baada ya uchaguzi kama nikishindwa nitaendelea kuwa Mbunge wa chama, Katibu wa Wabunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama. Baada ya uchaguzi Mbowe akishindwa ataendelea kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kama ilivyo Mtei na Makani. Sote hatuna ujanja zaidi ya kujenga chama na kukiimarisha.

Mkuu FMES nafikiri hapo kwenye red colour ndio msumari wa mwisho wa jeneza na hapa sasa ndio naanza kuamini kwamba 2010 ndio mwaka wetu wananchi wa Mapinduzi ndani ya Tanzania. Kazi imeanza sasa na alama za nyakati sasa zinasomeka vizuri.

Msemo;

"Kama huna meno kwanini ung'ang'anie fundo la Muwa................."
 
Baadhi ya watu wanafikiri Siasa ni "Chuki"...Watz hawana culture hio..Zitto kuwashukuru hao Mafisadi haimaanishi basi nae fisadi...Kutetea Ununuzi wa Mitambo ni sababu ya Msingi, kila mtu anafikra zake kupima SIASA vs Hali ya Uchumi wakati husika. Ndio maana watu hukaa vikao....ktk Vikao kuna kutafautiana na ndio Ubinaadamu...!!!..otherwise turudi ktk system za Udikteta!!!

Mr. Chuma

Tusiwe wepesi wa kusahau, Mh. Zitto kwenye Mitambo ya Dowans akubali kabisa kwamba alichemsha, mpaka Mwakyembe akasema hivi ni Zitto ninaye mfahamu au ni mwingine! Nikikumbuka ile picha ya utetezi wa Dowans vs Ngeleja na nchi kuwa gizani mpaka leo ni kitendawili.

Kuwashukuru Chenge na MAFISADI kuna nini? aishukuru Serikali kwani ndo kodi za Wananchi zimetumika vilivyo! kwanza kama siyo wizi wao huo nchi tiyari ingeshasambaza lami TZ nzima!

Huyu ni mwanasiasa inabidi awe makini, sasa ndo anaingia U/Kiti lazima watu washituke, ila ni haki yake.

NITASEMA UKWELI DAIMA
 
Mr. Chuma

Tusiwe wepesi wa kusahau, Mh. Zitto kwenye Mitambo ya Dowans akubali kabisa kwamba alichemsha, mpaka Mwakyembe akasema hivi ni Zitto ninaye mfahamu au ni mwingine!

NITASEMA UKWELI DAIMA

DU, yaani wewe kati ya Zitto na Mwakyembe unamuamini MWAKYEMBE? Ama kweli watanzania hawawajui wanasiasa wao zaidi ya wanavyoambiwa na WAHANDISI WA HABARI WETU.....

Nakushauri utafute authority zingine za kuamini lakini sio huyu POLITICAL MERCENARY...mtaishia kunyang'anya nchi MOBUTU na kumkabidhi KABILA SENIOR aliyeharibu kwa muda mfupi aliokuwa madarakani hadi baada ya Nyerere kushindwa kumuondoa mwanawe akaamua kumuondoa mwenyewe...Ama yale ya KUMUONDOA MOI kumuingiza KIBAKA (soma ITS OUR TURN TO EAT: THE STORY OF KENYAN WHISTLE BLOWER. Kama upo bongo tuwasiliane nikupatie....nakushauri kuchukua jitihada za kuwajua vizuri wanasiasa wetu kabla ya kuwapa imani zenu...

omarilyas
 
Ukisoma kwa makini makala ya Kiibanda hilo anguko ana maana kusema hivi Zitto atoke Kigoma huku aje achukue madaraka kwenye chama cha wenyewe walicho kihangaikia na kuki fadhili miaka nenda miaka rudi no way!. Hawawezi kufanya kosa la kumpa chama mark my word.

Lakini kama utaangalia kwa jicho la umakini zaidi umefika wakati Chadema ikaongozwa na wasomi wa kweli ( calibre ya Zitto ) Huyu Mbowe mtu aliefeli shule, akafeli biashara asiachwe afelishe chama pia. Tunako kwenda huko siasa zinazo takiwa ni za kujenga hoja sio kuvaa magwanda ya mgambo na vitisho kwenye majukwaa.

Zitto ana fit the bill lakini kwa ukabila ulio jaa Chadema sadly hato pata na pengine ndio ikawa the begiging of the end of Zitto kabwe
 
KIBANDA!! Huku tukiwa tunataka akina Zito waongezeke katika nchi hii, Mwenzetu unataka wapungue kama si kwisha kabisa.
Acha mawazo mgando.
Age is nothing katika hili.
 
Kaka Kibanda tafadhali washa simu tuwasiliane. Haujatenda dhambi ila strategy tu imebackfire.... Haya ni mambo ya ni kawaida tu ukingia kazini bila ya kupunguza munkari...

Nakala yako ya ITS OUR TURN TO EAT: THE STORY OF KENYAN WHISTLE BLOWER itachukuliwa na wengine soon...

omarilyas
 
ndiyo gharama za demokrasia mama mia. itakuwa kazi ikiwa atazuiwa kwa sababu zisizo za kidemokrasia maana wakati huo silabi DE katika CHADEMA itakuwa haina maana tena.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom