Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
FL,

Sidhani kama ni sahihi kusema Kibanda katumwa na Mbowe kutoa makala hii, kujaribu kuhamishia mjadala kwa Mh.Mbowe. Tungejaribu kuangalia historia ya huyu jamaa (Kibanda)tujue amekuwa na mtazamo gani juu ya ushiriki wa Mh.Zitto kny siasa za Tanzania. Pia tumsikilize Mh.Mbowe tuone anatoa comments gani juu ya hili, ndipo tunaweza kucomment vizuri on this!
Mkuu Subiri mbowe asema ndo useme jamani kwani mbowe anahatimiliki ya uenyekiti chadema?yeye nani asipingwe?yaani nimesoma hii nakala inasema eti mwanasiasa mchanga sijui nini,mara kachukua fomu bila kumuuliza mbowe kama anangombea au la,MAKUBWA HAYA
 
Kibanda kwenye makala hii umekuwa upande mmoja wa Mbowe,unasema kuwa Zitto ni kijana na unakubali amesimamia mambo makubwa ya kisiasa nchini, pia amekuwa naibu Katibu mkuu kwanini ashindwe kusimamia kazi ya uenyekiti wakati Mtendaji mkuu wa chama ni katibu mkuu? Zitto awe na subira kwani hujui kuwa muda uliopo ndio wako na muda ujao si wako? una maana vijana ni taifa la Kesho? JK amekuwa naibu Katibu mkuu wa CCM akiwa na miaka 25.

amekuwa naibu waziri kwenye wizara nzito ya nishati akiwa na miaka 33.kama ZITTO ana SHINE bungeni kwanini ashindwe uenyekiti wa Chadema?
Just to put the record straight, Jk aliukwaa unaibu Waziri mwishoni mwa awamu ya kwanza ya Mzee Mwinyi ie 1989,na JK hajawahi asilani kuwa naibu Katibu Mkuu si wa TANU wala CCM, isipokuwa amewahi kuwa Katibu wa CCM wa wilaya mbali mbali ikiwemo Nachingwea na Masasi ambacho kilikuwa kituo chake cha mwisho kabla ya kuwa Naibu Waziri wa Nishati chini ya Mzee Maokola Majogo.Tupige hesabu hapo maana maana JK amezaliwa mwaka 1950.
 
hamjauelewa mchezo ulioko hapa. Kibanda anatumiwa na wala si mbowe bali na kundi la mafisadi ili kuvuruga uchaguzi wa chadema na kuisambaratisha. Na anatumiwa na walewale!

kuthibitisha maneno yangu kanunuliwa gari la kufanana yeye na Muhingo, Mhariri Mtendaji wa New Habari na yote yametoka kwa mfadhili mmoja na yanafuatana namba. Kibanda ni fisadi kama wengine
Astaghafirulah,kama ni ya kweli haya basi sekta ya habari kwisha kazi maana nani sasa amfunge mwenzie kengele!
 
Mkuu Subiri mbowe asema ndo useme jamani kwani mbowe anahatimiliki ya uenyekiti chadema?
Sipingi Zitto kugombea uenyekiti, nachopinga mimi ni sentensi yako kwamba Kibanda katumwa na Mbowe.......hii inawezekana si kweli!
yeye nani asipingwe?
Hujanielewa ni demokrasia ya kweli tu kumpinga Mh. Mbowe lakini tusimzushie......i.e kamtuma Kibanda!
yaani nimesoma hii nakala inasema eti mwanasiasa mchanga sijui nini,mara kachukua fomu bila kumuuliza mbowe kama anangombea au la,MAKUBWA HAYA
To me huu ni mtazamo finyu na wa kizamani sana wa Bwana Kibanda. Kama walivyosema wengi, hakuna hoja yamsingi aliyoleta Kibanda zaidi ya kuonyesha haelewi demokrasia ni nini!
 
Zitto azua mjadala

• Wazee CHADEMA walinda mchakato usiingiliwe

na Waandishi Wetu

HATUA ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, kuchukua fomu ya kugombea wadhifa wa uenyekiti, inaonekana kuibua mjadala katika anga la siasa hapa nchini.

Kuibuka kwa mjadala huo kwa kiwango kikubwa kumetokana na hatua ya mwanasiasa huyo kijana kuamua kukabiliana na Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika ndani ya CHADEMA, zinaeleza kwamba uamuzi huo wa Zitto unaonekana kuwashtua viongozi mbalimbali wa juu wa chama hicho.

Mbali ya hao, uamuzi huo wa Zitto kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa chama hicho, unaonekana kugusa mijadala ndani ya vyama vingine vya siasa, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Makada kadhaa wa CCM waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti juzi na jana walisema, mabadiliko ya uongozi ndani ya CHADEMA ni jambo linalofuatiliwa kwa karibu.

Kama ilivyokuwa kwa CCM, mchakato huo unaonekana kukigusa pia Chama cha Wananchi (CUF) ambacho ndani ya Bunge kimeunda serikali kivuli kwa ushirikiano na CHADEMA.

Hata hivyo, kikubwa kinachozusha mijadala na maswali, ni hatua hiyo ya Zitto kuamua kugombea akichukua fomu Kigoma na kutuma watu wa kumrejeshea pasipo yeye mwenyewe kukutana na viongozi wenzake wa juu.

"Uamuzi wa Zitto kuchukua fomu ya uenyekiti si jambo la ajabu hata kidogo. Kinachotatanisha ni kwamba, huyu jamaa ameamua kugombea kwa staili ya kakakuona.

"Ametoweka katika Ofisi za Makao Makuu kwa zaidi ya miezi mitatu, akasikika akiwa Kigoma na aliporejea Dar hakukutana na kiongozi mwingine yeyote hadi alipotuma watu kumrejeshea fomu juzi," alisema kiongozi mmoja wa juu wa CHADEMA aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.

Jitihada za Tanzania Daima Jumatano kuwasiliana na Zitto kwa njia ya simu jana, hazikufanikiwa na taarifa zinasema alikuwa nchini Ujerumani kwa shughuli binafsi.

Hata hivyo, alipozungumza na Tanzania Daima Jumatano mwishoni mwa wiki kuhusu kuwapo kwa taarifa zilizokuwa zikimhusisha na kugombea wadhifa huo, Zitto alikiri kuwapo kwa shinikizo kutoka miongoni mwa viongozi wenzake ndani ya chama hicho.

"Nimekuwa nikipata shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya watu ndani ya chama wanaonitaka nigombee uenyekiti. Nimekuwa nikitafakari sana na hadi sasa bado sijaamua kugombea au la," alisema Zitto siku ya Jumapili.

Alipoulizwa iwapo alikuwa amefanya mawasiliano yoyote na viongozi wenzake wa CHADEMA kuhusu yeye kuwa na mpango wa kugombea, Zitto alisema asingeweza kufanya uamuzi wowote kabla ya kumtaarifu Mbowe na Katibu Mkuu wake, Dk. Wilbrod Slaa.

Gazeti hili lilipowasiliana na Mbowe siku ya Jumapili na jana kuhusu uamuzi huo wa Zitto kugombea, mara zote mwanasiasa huyo aliwaelekeza waandishi wetu kuwasiliana na Ofisi ya Katibu Mkuu ambayo alisema ndiyo inayoratibu shughuli zote za uchaguzi wao.

Hata hivyo, pamoja na kutokuwa tayari kuingia kwa undani, jana Mbowe alilihakikishia gazeti hili kwamba tayari alikuwa amejaza na kurejesha fomu za kugombea uenyekiti katika Ofisi ya Katibu Mkuu.

Wakati Mbowe akikataa kutoa ufafanuzi mwingine wowote wa ziada, ofisa mmoja wa juu wa CHADEMA alilieleza Tanzania Daima Jumatano kuwa, uamuzi wa mwenyekiti huyo kuchukua fomu za kugombea, ulichagizwa na shinikizo au ushauri wa wazee wa chama hicho.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, Mbowe alijaza fomu hizo baada ujumbe wa wazee hao wa chama uliowajumuisha, Profesa Mwesiga Baregu, Victor Kimesera na Bob Makani kukutana naye na kumshauri kugombea tena nafasi hiyo.

"Ninachoweza kukuthibitishia ni kwamba, Mbowe alikuwa amefikia uamuzi wa kutogombea uenyekiti hadi baada ya kushawishiwa na wazee ambao walimuomba kukivusha kwanza chama katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani," alisema mtoa habari wetu.

Baadhi ya wanasiasa waliozungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa nyakati tofauti tangu tetesi za Zitto kuwa na nia ya kugombea nafasi hiyo akichuana na mwenyekiti wa sasa, walieleza kuwa ingawa hatua hiyo inaonyesha jinsi demokrasia ilivyokaa ndani ya CHADEMA, kwa upande mwingine inaweza kukipeleka pabaya chama hicho.

Mmoja wa wanasiasa hao aliyezungumza na gazeti hila jana kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini, alieleza kuwa hatua ya Zitto kuwania nafasi ya uenyekiti, ina lengo la kukidhoofisha chama hicho kwa sababu inaweza kuleta mgawanyiko miongoni mwa wanachama.

Alisema uwezekano wa kutokea kwa mgawanyiko ndani ya chama ni mkubwa, kwa sababu CHADEMA sasa imekuwa ikiangaliwa kwa jicho baya na vyama vingine vya siasa kutokana na mafanikio ambayo kimeyapata kwa muda mfupi.

"Zitto, kama mwanachama wa CHADEMA anayo haki ya kuwania nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama ilimradi ametimiza masharti, lakini uamuzi wake wa sasa ameuchukua wakati mbaya kwa sababu anaweza kutumiwa na maadui wa chama kukidhoofisha," alisema mwanasiasa huyo.

Mwanasiasa mwingine aliyetoa maoni yake kuhusu uchaguzi huo, ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed, ambaye alieleza kuwa kujitokeza kwa Zitto kuchuana na Mbowe kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, ni dalili za kukomaa kwa demokrasia ndani ya chama hicho.

Hamad, ambaye pia ni Mbunge wa Wawi (CUF), alisema kujitokeza kwa wanasiasa wenye majina makubwa kuchuana kuwania nafasi ya kuiongoza CHADEMA, kunaonyesha jinsi demokrasia ilivyopea ndani ya chama hicho ingawa pia ni dalili za wazi za wanachama kutokubaliana na uongozi uliopo.

"CHADEMA wanaonyesha jinsi demokrasia ilivyopea ndani ya chama chao, lakini pia, unapoona mtendaji wa ngazi ya juu ndani ya chama anajitokeza kugombea nafasi inayoshikiliwa na kiongozi mwenzake, hiyo ni dalili ya wazi ya kutoridhishwa na uongozi uliopo.

"Hivyo, ingawa Zitto yupo sahihi, lakini hatua yake hiyo inaonyesha wazi kuwa anataka mabadiliko katika uongozi wa juu kwa kuwa haridhiki na jambo fulani," alisema Hamad.

Aidha, aliufananisha uchaguzi huo wa CHADEMA na ule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo wanachama wake hujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, zikiwemo zile za ngazi za juu, lakini anapopatikana mshindi hurejea kuwa kitu kimoja.

Alisisitiza kuwa, chama chake na kambi nzima ya upinzani, vitakuwa tayari kushirikiana na kiongozi yeyote atakayechaguliwa kukiongoza chama hicho, kwa sababu ndiye atakuwa chaguo la wana CHADEMA.

Kwa upande wake, wakili wa kujitegemea na mmoja wa waanzilishi wa mageuzi hapa nchini, Mabere Marando, alieleza kuwa haoni tatizo kwa Zitto kujitokeza kuchuana na Mbowe kuwania nafasi ya juu ya uongozi ndani ya chama, kwa sababu demokrasia ndani ya vyama vya siasa inaelekeza hivyo.

"CHADEMA wanaonyesha jinsi demokrasia ilivyokomaa ndani ya chama chao, anapojitokeza mwanachama kumpinga kiongozi aliyepo, ndiyo kukomaa kwa demokrasia. Hapo atakayeshinda inajulikana ndiye anayependwa na wanachama, hivyo anakuwa na uhalali usio na shaka wa kuongoza," alisema Marando.

Kwa upande wake, Ndimara Tegambwage, mmoja wa wanasiasa wa mwanzo kujiunga na vyama vya siasa vya upinzani, alisema kujitokeza kwa Zitto kuchuana na Mbowe, kunaonyesha kuwepo kwa fursa ya kila mwanachama kugombea nafasi ya uongozi.

"CHADEMA wameonyesha kuwa wana uhuru, sioni kama hilo litaleta mgogoro, ilimradi mipango na taratibu zao za uchaguzi ndani ya chama zinafuatwa," alisema Ndimara.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa, amesema licha ya baadhi ya wanachama wa chama chao waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kupokea vitisho kutoka kwa baadhi ya wanasiasa walio nje ya chama hicho, ya kuwataka kuondoa majina yao, hakuna mwanachama aliyetishika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana makao makuu ya chama hicho, Dk. Slaa alisema uchaguzi huo unaangaliwa kwa namna tofauti tofauti na watu wa aina mbalimbali wakiwemo wanaoitakia mabaya CHADEMA.

Hata hivyo, hakuweka wazi vitisho vinavyotolewa kwa baadhi ya wagombea.
Alisema mchakato wa uchaguzi unaendelea vizuri ambapo watu wenye nafasi tofauti katika jamii wamejitokeza kugombea ngazi mbalimbali.

Aliyataja matabaka ya watu hao kuwa ni pamoja na wasomi na wafanyabiashara.
"Watu wanaogombea wamekuwa wengi sana, na hii ni faraja kwetu kwani inakuza demokrasia na inaonyesha kuwa Watanzania sasa wanazijua haki zao za kikatiba za kuchagua na kuchaguliwa," alisema Dk. Slaa.

Akizungumzia mchuano wa nafasi ya uenyekiti, alisema hadi jana wanachama waliochukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi hiyo ni wawili aliowataja kuwa ni Mbowe na Zitto.

Hata hivyo, alieleza kuwa huenda idadi ya wagombea wa nafasi hiyo ikaongezeka baada ya kupokea fomu za wanachama wa mikoani walioomba kuwania nafasi za uongozi.
Kuhusu wagombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti kwa upande wa Bara, Dk. Slaa alisema inawaniwa na wanachama watatu aliowataja kuwa ni Profesa Mwesiga Baregu, Anna Maulida Komu na Said Arfi.
Alisema CHADEMA kimeongeza vyombo vitatu ndani ya chama hicho ambavyo viongozi wake watapigiwa kura, na alivitaja kuwa ni Baraza la Wanawake (Bawacha) ambapo wamejitokeza wagombea 33, Baraza la Vijana (Bavicha) ambalo nafasi zake zinawania na vijana 33 na baraza la wazee lenye wagombea 13.

Dk. Slaa alizungumzia pia mikoa ambayo imezuiliwa kufanya uchaguzi ngazi ya mkoa kutokana na dosari mbalimbali ikiwemo mikoa ya Mbeya, Mara na Arusha ambayo imebainika rushwa kutumika na kutotimiza vigezo vya kufanya uchaguzi.
Katika hatua nyingine, aliyekuwa Katibu Mwenezi Taifa wa chama cha NCCR- Mageuzi, Joseph Selasini, jana alijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama na Dk. Slaa. Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi, Selasini alisema ameamua kujiunga CHADEMA baada ya kuona kuwa kinajali demokrasia na uhuru wa kweli.
 
Last edited:
sioni tatizo hapo kwa zitto kugombea..umri sio issue..sema wkt wa campaign zao ndo tutajua ka zitto kafikishwa bei yake na ccm au namna gani..itajulikana tu..kama ipo ipo tu..hii ndo bongo...watabana wataachia..tutajua ukweli..na tukijua kwakweli zitto ka umekula mlungula kwa ccm tutakutazama kwa jicho baya sana...ole wako!!!!
 
jamani eeeh wao CHADEMA wanasema ndiyo demokrasia sasa mnataka nini, tunataka viongozo wa vyama kama akina Mrema eti mtu mwingine akigombea anafukuzwa uanachama!!! angalieni yaliyofanyika CUF, muulizeni Prof Safari!! waacheni CHADEMA wakomaze demokrasia
 
Nina uhakika Mbowe hakufurahia hata kidogo makala ya Kibanda, Ninajaribu kumfikiria kibanda alitaka kusema nini katika makala yake nikagundua tu kuwa aliadika kujipendekeza kwa mwajiri wake ili aonekane kuwa anasapiti kwa nguvu zake zote kumbe ni kumharibia Freeman.

Mwenyekiti wa chadema, Freeman Mbowe anajua siasa za ushindani na ndiyo maana wakati wa kutangaza matokeo ya urais mwaka 2005, alikwenda Diamond jubilee na kumkumbatia kikwete kwa ushindi alioupata ingawa alijua kuwa ni ushindi uliotokana na fedha za wizi kutoka EPA, alijua kuwa CCM walicheza faulu nyingi mpaka kupata ushindi, lakini Freeman alijua kuwa CCM walishinda akakubali. Lipi la ajabu kwa Zitto kuchukua fomu???

Kibanda acha kujipendekeza hivyo!!! sasa unazidi ndugu yangu! Gazeti lako litakosa umaarufu wake ukiendelea kufanya hivyo. Acha Mbowe ashindane na Zitto kisiasa wala si kwenye magazeti na usimharibie Mbowe katika hili. Wana chadema wanawaheshimu sana Zitto na Mwenyekiti wake. Acha waamue ni nani ataendeleza libeneke hili la demokrasia na maendeleo!

Mbowe ataibuka mshindi na kabwe atakubali kushindwa na kuendelea kuwa katibu msaidizi.
 
Just to put the record straight, Jk aliukwaa unaibu Waziri mwishoni mwa awamu ya kwanza ya Mzee Mwinyi ie 1989,na JK hajawahi asilani kuwa naibu Katibu Mkuu si wa TANU wala CCM, isipokuwa amewahi kuwa Katibu wa CCM wa wilaya mbali mbali ikiwemo Nachingwea na Masasi ambacho kilikuwa kituo chake cha mwisho kabla ya kuwa Naibu Waziri wa Nishati chini ya Mzee Maokola Majogo.Tupige hesabu hapo maana maana JK amezaliwa mwaka 1950.

Jk kazaliwa oktoba 1955.kapata unaibu waziri wa madini mwaka 1988,kamaliza chuo kikuu 1975 akiwa na miaka 20 akapangiwa kazi za chama Singida ndio kituo chake cha kwanza kama katibu wa chama. akaenda Tabora na mwaka 1977 akapelekwa makao makuu ya chama Zanzibar ofisi ya Kisiwandui kama Naibu Katibu mkuu wa CCM ofisi ya Zanzibar.mara tu baada ya kuzaliwa CCM.
 
The question here is what will happen after the election if he loose,.....
 
“Ninachoweza kukuthibitishia ni kwamba, Mbowe alikuwa amefikia uamuzi wa kutogombea uenyekiti hadi baada ya kushawishiwa na wazee ambao walimuomba kukivusha kwanza chama katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani,” alisema mtoa habari wetu.

Yale yale! typical CCM style, we still have a long way to go
 
Pasco,

Unafikiri kwa nini Zitto, of all the wadau wa jf wanaofuatilia hii thread,kakushukuru kwa post yako hii?
 
Last edited by a moderator:
Msiogope wana Chadema na wapenda demokrasia nchini. Hii ndiyo Demokrasia sahihi. CHadema wanataka kuionyesha CCM kuwa mambo ya kumzuia mtu asigombee wakati katiba haisemi hivyo, ni kudumaza demokrasia.Zitto anaposema anataka kukijenga chama kuelekea kushika dola hana maana kuwa MBowe hawezi ila ana maanisha kuwa dola haiwezi kushikwa sawasawa kama chama hakina demokrasia ya kweli - yaani CCM haifai kushika dola kwani haina demokrasia ya kweli. Pia anapozungumzia kuwa na sera mbadala haina maana kuwa yeye binafsi ndiye mwenye sera mbadala bali Chama kwa ujumla.

Juu ya suala la kufukuzana, hapa anawasema waziwazi CCM ambao mwenye mawazo mbadala anatishiwa kufukuzwa - Angalia walivyomtishia Sitta

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%
 
Hivi Sheria na taratibu za Uchaguzi wa viongozi ndani chama Chadema, haziruhusu mtu kuchukua form mbili au tatu kugombea nafasi tofauti tofauti?..
Je, ina maana mtu anayegombea Uenyekiti haruhusiwi kugombea Ukatibu au nafasi nyingine yaani akishindwa nafasi moja ndio basi imetoka hiyo..
Naomba kuelemishwa kwani yaonyesha wazi kuwa uchaguzi huu ndani ya Chadema umechukuliwa kama ndio kielelezo cha Uchaguzi mkuu wa 2010..
 
1. Mbowe is a failure who is out of the country -more than half the time- presumably finishing his degree.

2. Ninapoanza kusoma reports za sababu za Zitto kuingia kwenye kinyang'anyiro hiki- midn you reports- just reports, sababu zake, regardless of whether he will be successfull of fail, sababu zake ziko impressive.

3. Hii inaonyesha ukomavu wa siasa na demokrasia ya hali ya juu, vitu ambavyo CCM hata baada ya miaka 32 -discounting the TANU years- katika power hawajaweza kufanya
 
Kura za Wazee na Wanawake - Mbowe

Kura za Vijana na watu Makini - Zitto
 
Kibada anaona mbali, anahisia za chama kuanguka kutokana na uimara wa mbowe kukifadhili na kujitolea kwa chama.

Mbowe akitoka Chadema itaanguka kwa kishindo kikubwa kama hawatapata wabunge wengi mwaka ujao wa uchaguzi. Wote ni Vijana nina imani walikuwa na fursa ya kukaa pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kisiasa. Vinginevyo ukiona dalili kama hizo ujue kuna jambo aidha mamluki wameanza kuingia Chadema. Tusubiri na tuone matokeo yake.

Watu wengi sana na wenye busara wanashauri sana CHADEMA watafute kwanza wabunge wakutosha watakaoweza kuwajengea imani wananchi then dhana nzima ya kugombea urais ndipo ianze. Zitto akigombea urais kwa mwaka ujao akishindwa na CCM ataanguko sana kisiasa.

Ni kweli Zitto ana haki zote kama mwanachama kugombea nafasi yoyote ndani ya chama chake. Lakini kwa mtu mchunguzi atagundua jinsi Zitto amekuwa akihusika ktk matukio ya ajabu ajabu kwa siku za hivi karibuni kama vile kushabikia kununuliwa kwa mitambo ya Dowans na pia kuhusishwa kwake na Kikwete kiasi imani ya wanachama wengi ikaanza kupungua. Nasema ni ngumu kwa wengi kuzingatia hilo lakini Zitto kama mgombea uraisi mtarajiwa anapaswa kuwa makini sana na hatua zake za sasa ajijenge zaidi na kuzidisha imani kwa watu badala ya kuvimbishwa na umaarufu ambao ndio mtego kwa wanasiasa wengi ambao hufuatiwa na anguko.

Kuhusu uzoefu, nadhani anao wa kumtosha lakini anayo nafasi ya kujifunza zaidi na kwa kweli umri SOMETIMES ni determinant ya cheo ndio maana katiba imemtaka mgombea uraisi wa nchi awe na umri wa kuamzia miaka 40. nadhani kuna some sense of connection between umri wa mtu, uzoefu na uongozi wa umma.

Binafsi naamini anao uwezo lakini anahitajika pia kujenga uvumilivu wa kisiasa kama anavyosahuriwa na Kibanda. Hata hivyo ni ushauri tu uamuzi ni wake mwenyewe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom