Kesi za talaka zizingatie muda kwenye kutoa hukumu kuepusha ukatili dhiki ya mwanamke

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Wasimamizi wa sheria za ndoa wanachangia sana ongezeko la uharifu dhidi ya binadam!

Kesi nyingi za talaka zikifika mahakaman zinapigwa danadana sana kiasi cha kuchukua muda mrefu huko mahakaman jambo linalochangia madhara kwa wanandoa wenyewe!

Athari kubwa inamkumba sana mwanamke ambaye yupo limited na muda wa menopause ili kuendeleza kuzaa na kuanzisha familia nyingine!

Mwanaume anaweza endelea kupigisha danadana huku akiwa anazalisha wanawake wengine huko, lakini mhanga katika kesi ni mwanamke ambaye hawezi na hatakiwi kubeba mimba inje ya ndoa!

Kuna haja gani kesi za talaka kuchukua muda mrefu wakati mashahidi wakuu ni wanandoa wenyewe?

Serikali kwanini inafumbia macho unyama huo wa makusudi dhidi ya wanawake?

Kuna haja gani kesi ya talaka kuchukua muda mwingi zaidi ya mwaka?
 
Wanasema Eti wanawapa muda wa kutafakali maana huenda ni hasira tu lakini muda ukipita huenda wakagairi kuachana.

Sasa muda usiwe mrefu , iwe walau miezi 2-3 tu basi, badala ya miaka .
 
NINA UZOEFU NA MAHAKAMA, HASA HIZI KESI ZA TALAKA.
MAHAKAMANI KUNA KESI ZA TAKALAKA ZINACHUKUA MIEZI MIWILI AU MITATU KUISHA! NA ZINGINE ZAIDI YA MIAKA 10!
MAHAKAMANI NI USHAHIDI, TENA USIO NA MASHAKA!
SIO SEHEMU YA KWENDA NA KUANZA SIMULIZI ZA MATESO YA KWENYE NDOA.
KWAMBA UMESIKIA VISA VYA KWENYE NDOA ZA ZA WENGINE HUKO MTANDAONI NA MITAANI ZA UONGO NA KWELI KISHA UKIJIVISHA, UKAONEKANA WEWE NDIO UMETENDEWA.!
WALE WANAO KWENDA HUKO KWA USHAWISHI WA NDUGU NA MARAFIKI, NA MICHEPUKO WANAISHIA KWENDA RUDI KWENDA RUDI KWENDA RUDI.KWA KUKOSA SABABU YA MSINGI.

MFANO:

MWANAMKE UNAKWENDA KUOMBA TALAKA KWA SBB YA VIPIGO VYA MARA KWA MARA TOKA KWA MUME:
1.JE UMEWAHI PELEKA MALALAMIKO KWA WAZAZI? USTAWI? DAWATI LA JINSIA? POLISI? KANISANI?BAKWATA?WASIMAMIZI WA NDOA? WASHENGA?
2.JE UMEWAHI TIBIWA HOSPITALI AU KULAZWA KWA SBB YA KIPIGO? JE UNA ALAMA/MAKOVU YA KUPIGWA?
3.JE KUNA WATU WALIOTAYARI KUTHIBITISHA VIPIGO JUU YAKO? JE NI WATOTO? WASAIDIZI WA KAZI ? WANAFAMILIA WENGINE?
4.JE SABABU YA VIPIGO NI NINI? UWE TAYARI KUSEMA.

SASA WEWE BEBA MIZIGO YAKO, ONDOKA NDANI YA NDOA NENDA KAPANGISHE CHUMBA.
KISHA NENDA KADAI TALAKA MAHAKAMANI HUKU UKIWA HUNA MAJIBU KAMILI YA MASWALI HAYA MANNE.
HUO UTAKUA MWANZO WA SAFARI ISIYO NA MATUMAINI.

KABLA YA KUDAI NA KWENDA MAHAKAMANI, ANZA KUTENGENEZA USHAHIDI.
MESEJI, AUDIO, VIDEO, PICHA, VIKAO VYA USURUHISHI, NK NK.
ULIZA ULIZA KWA WANASHERIA JUU YA SHAURI/MADAI YAKO(KUNA JUKWAA LA SHERIA HAPA), UPATE KUJUA ZAIDI.
USIEGEMEE ZAIDI KWA TAFSIRI ZA SHERIA ZA MITAANI. UTAUMIA
 
Kuna wengine wanadai talaka baada ya muda unakuta anaujauzito WA huyo bwana!! Na wakati mwingine inaweza kuwa biashara kama ikiwezeshwa Kwa haraka Bora isiwe kama kuchuma mtaji WA dhuluma
 
Wasimamizi wa sheria za ndoa wanachangia sana ongezeko la uharifu dhidi ya binadam!

Kesi nyingi za talaka zikifika mahakaman zinapigwa danadana sana kiasi cha kuchukua muda mrefu huko mahakaman jambo linalochangia madhara kwa wanandoa wenyewe!

Athali kubwa inamkumba sana mwanamke ambaye yupo limited na muda wa menopause ili kuendeleza kuzaa na kuanzisha familia nyingine!

Mwanaume anaweza endelea kupigisha danadana huku akiwa anazalisha wanawake wengine huko, lakini mhanga katika kesi ni mwanamke ambaye hawezi na hatakiwi kubeba mimba inje ya ndoa!

Kuna haja gani kesi za talaka kuchukua muda mrefu wakati mashahidi wakuu ni wanandoa wenyewe?
Serikali kwanini inafumbia macho unyama huo wa makusudi dhidi ya wanawake?
Kuna haja gani kesi ya talaka kuchukua muda mwingi zaidi ya mwaka?
Kama mwanaume anapigisha danadana, kitu gani kinamzuia mwanamke kufanya hivyo hivyo? Kwa nini unafikiria ni unyama dhidi ya wanawake tu? Kuna kesi za talaka ambazo unyama ni dhidi ya mwanaume.
 
Wanasema Eti wanawapa muda wa kutafakali maana huenda ni hasira tu lakini muda ukipita huenda wakagairi kuachana.

Sasa muda usiwe mrefu , iwe walau miezi 2-3 tu basi, badala ya miaka .
Ni ajabu sana!
 
Kama mwanaume anapigisha danadana, kitu gani kinamzuia mwanamke kufanya hivyo hivyo? Kwa nini unafikiria ni unyama dhidi ya wanawake tu? Kuna kesi za talaka ambazo unyama ni dhidi ya mwanaume.
Umeelewa hoja lakini?
 
Tume ya haki za binadam iaangalie jambo hili wahanga wakubwa ni wanawake na watoto!
Kesi za talaka ziamuliwe mapema ili kuondoa attention ya migogoro inayowapotezea muda mwingi hata kuzorotesha uchumi wao na pia wanakuwa hatarini kuumizwa!

Pamoja na yote mwanamke kwa sababu ya kidhitisho cha tumbo ...hawezi kubeba mimba hadi pale kesi yake ya talaka ikikamilika!
 
KUMBUKA:Kuna wanawake matapeli.Anaolewa ili apate uhalali wa kudhulumu mali za mwanaume.Ana buy-buy time tu ili ahalalishe kugawana mali.Shtuka.Wezi ni wengi mjini na vijijini.
Tume ya haki za binadam iaangalie jambo hili wahanga wakubwa ni wanawake na watoto!
Kesi za talaka ziamuliwe mapema ili kuondoa attention ya migogoro inayowapotezea muda mwingi hata kuzorotesha uchumi wao na pia wanakuwa hatarini kuumizwa!

Pamoja na yote mwanamke kwa sababu ya kidhitisho cha tumbo ...hawezi kubeba mimba hadi pale kesi yake ya talaka ikikamilika!
 
Wasimamizi wa sheria za ndoa wanachangia sana ongezeko la uharifu dhidi ya binadam!

Kesi nyingi za talaka zikifika mahakaman zinapigwa danadana sana kiasi cha kuchukua muda mrefu huko mahakaman jambo linalochangia madhara kwa wanandoa wenyewe!

Athali kubwa inamkumba sana mwanamke ambaye yupo limited na muda wa menopause ili kuendeleza kuzaa na kuanzisha familia nyingine!

Mwanaume anaweza endelea kupigisha danadana huku akiwa anazalisha wanawake wengine huko, lakini mhanga katika kesi ni mwanamke ambaye hawezi na hatakiwi kubeba mimba inje ya ndoa!

Kuna haja gani kesi za talaka kuchukua muda mrefu wakati mashahidi wakuu ni wanandoa wenyewe?

Serikali kwanini inafumbia macho unyama huo wa makusudi dhidi ya wanawake?

Kuna haja gani kesi ya talaka kuchukua muda mwingi zaidi ya mwaka?
Nani alikuambia hautakiwi kubeba nje ya ndoa?Yeye anazaa nje,kwa nini wewe usizae?Au unaogopa ile"watanionaje".Talaka ni peace of paper tu.
 
Back
Top Bottom