Uwepo wa rais Mbeya kesho kwenye 8-8 ndio kumeahirisha hukumu ya kesi ya Bandari?

kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
3,056
8,710
Salam wakuu,

Wengi wanajua kuwa leo Mahakamani hapo Mbeya kulipaswa kusomwa hukumu ya kesi inayovuta masikio na hisia za watu wengi, ambayo imetunguliwa na mawakili wa nne wakujitegemea dhidi ya Jamhuri (AG) na Bunge pia kupitia Katibu wa Bunge.

Historia ya kuibuka kwa shauri hili inajulikana,kuahirishwa kwa hukumu za kesi pia sio jambo geni Ila kwa hii inaleta hisia hasi!

Kwanini hisia hasi? Kwanza wengi tunajua kua rais Samia anatuhumiwa kuhusika na mkataba tata ulioibua kesi hii na moja kwa moja inasemwa ameuza Mali za Tanganyika kwa wajomba(waarabu wa Dubai).

Kumekuwa na jitihada kubwa sana kwa serikali ya Samia kutetea na kuhakikisha Jambo hilo linaendelea na Ni zuri (japo watu wanahoji,kama ni zuri kwa nini hakujumuisha na bandari za Zanzibar anapotokea?)

Kesho Mbeya rais arashiriki maadhimisho ya 8-8 na kwa kawaida Mbeya ni mji ambao hauna nidhamu ya kinafiki,kama mtakumbuka hapo Mbeya rais Kikwete aliwahi kupopolewa Mawe kwenye msafara wake, Magufuli aliwahi kuzomewa pia huko awali.

Kuahirishwa kwa hukumu ya kesi husika siku moja kabla ya raisi kuwa Mbeya kwenye maadhimisho ni kuepusha aibu na fedheha ya kuzomea?

Kuahirishwa kwa hukumu,ni kua hukumu imeshapangwa na watawala wanahofia itapokewa kwa hasira na kuzua heka heka?

Hukumu itasomwa siku moja ama 2 baada ya Rais kuwa ameshaondoka Mbeya,je ujio wake hapo kesho ndio sababu?

Kwenye japo la mahakimu wanne,mmoja kukosekana hakuzuii watatu waliobaki kutokusema hukumu,kwa nini ihairishwe?!! Ujio wa raisi?

Binafsi inatoa taswira tayari kua hukumu hiyo ni ya kubumba,kama ni ya haki basi ingeendelea tu.

Kwenye familia ama maisha yetu,ukiwa unatenda ama unataka kutenda jambo la fedheha,husubiri kwanza umma utulie usikutane na heka heka, naona ndio haya!
 
Aibu ni aibu tu, iwe umezomewa laivu ai umezomewa miyoni mwa watu, hata akiondoka watu watazomea picha zake, cha msingi kama kweli wana nia njema na Nchi hii basi wauweke ukweli hadharani, kwa faida ya kizazi kijacho.
 
Kwaiyo tusadiki maneno ya Ristam Azizi kuwa Majaji huwa wanapigiwa simu!!

Unafikiri kwa bahati mbaya alitamka hayo?!! Wizi wa Kagoda unaukumbuka?!! Mmiliki wa Kagoda si alikua Rostam,kesi ilienda mahakamani?! Wizi wa dowans unaukumbuka?!! Mmiliki wa Dowans si alikua Rostam,ulisikia kesi?!!

Kwa nini makampuni ya kimataifahayataki migogoro yao kuamriwa mahakama za Tanzania?!?
 
Duh!ila huyu jamaa katupiga sana nchi hii!
 
Duh!ila huyu jamaa katupiga sana nchi hii!
Ndio maana billionea mkubwa.

Ile tenda tu ya ujenzi wa barabara kutoka Ubungo hadi Kibaha kwa kutumia kampuni yake tayari ni mabilion yahela

Bado mgodi wa Almasi kule Shinyanga kauchukua kupitia kampuni yake ya Caspian construction.

Bado kqnunuq Tigo,Zantel,Auric Air etc.
 
Itakuwa Jaji kapigiwa simu asionekane leo ili wahairishe

Atafutwe RC Juma Homera atuambie
 
Yani nchi ya ajabu sana hii

Jana ndio maana events ya Mpira ikatekwa kisiasa.

Kikwete alikua akienda uwanjani,hajawahi kuteka tukio.

Magufuli alienda uwanjani,hakuwahi kuteka tukio.

Wa sasa hata mechi zakawaida za ligi,vijana wanaebeshwa picha na mabango ya Mama.

Jana kuna tukio la hovyo likafanyikwa la maigizo ya albino,huku wahusika kwenye stage wakiwa wamevaa fulana za Mama,sijui wahusika wanaona ufahari!!
 
Salam wakuu,

Wengi wanajua kuwa leo Mahakamani hapo Mbeya kulipaswa kusomwa hukumu ya kesi inayovuta masikio na hisia za watu wengi, ambayo imetunguliwa na mawakili wa nne wakujitegemea dhidi ya Jamhuri (AG) na Bunge pia kupitia Katibu wa Bunge.
Umeona wapi jamii ikakaa kimya kupopolewa MAWE kwa kiongozi yeyote yule ?!!!!

Mh.Rais yuko Mbeya na haya mambo ya hukumu huvuta watu wengi maeneo ya mahakamani na mjini unataka watu wa PROTOKALI ya safari za Rais waridhie tu mchanganyiko wa majambo hayo mawili?!!!

Hivi shule tunakwenda kusomea "LGBT"?!!!
 
Ndio maana billionea mkubwa.

Ile tenda tu ya ujenzi wa barabara kutoka Ubungo hadi Kibaha kwa kutumia kampuni yake tayari ni mabilion yahela

Bado mgodi wa Almasi kule Shinyanga kauchukua kupitia kampuni yake ya Caspian construction.

Bado kqnunuq Tigo,Zantel,Auric Air etc.
Yaani mtu mmoja afanye hayo yote peke yake ?!!!

Haiwezekani.....
 
Salam wakuu,

Wengi wanajua kuwa leo Mahakamani hapo Mbeya kulipaswa kusomwa hukumu ya kesi inayovuta masikio na hisia za watu wengi, ambayo imetunguliwa na mawakili wa nne wakujitegemea dhidi ya Jamhuri (AG) na Bunge pia kupitia Katibu wa Bunge.

Historia ya kuibuka kwa shauri hili inajulikana,kuahirishwa kwa hukumu za kesi pia sio jambo geni Ila kwa hii inaleta hisia hasi!!

Kwanini hisia hasi?! Kwanza wengi tunajua kua rais Samia anatuhumiwa kuhusika na mkataba tata ulioibua kesi hii na moja kwa moja inasemwa ameuza Mali za Tanganyika kwa wajomba(waarabu wa Dubai).

Kumekuwa na jitihada kubwa sana kwa serikali ya Samia kutetea na kuhakikisha Jambo hilo linaendelea na Ni zuri (japo watu wanahoji,kama ni zuri kwa nini hakujumuisha na bandari za Zanzibar anapotokea?!).

Kesho Mbeya rais arashiriki maadhimisho ya 8-8 na kwa kawaida Mbeya ni mji ambao hauna nidhamu ya kinafiki,kama mtakumbuka hapo Mbeya rais Kikwete aliwahi kupopolewa Mawe kwenye msafara wake, Magufuli aliwahi kuzomewa pia huko awali.

Kuahirishwa kwa hukumu ya kesi husika siku moja kabla ya raisi kuwa Mbeya kwenye maadhimisho ni kuepusha aibu na fedheha ya kuzomea?!!

Kuahirishwa kwa hukumu,ni kua hukumu imeshapangwa na watawala wanahofia itapokewa kwa hasira na kuzua heka heka?!!

Hukumu itasomwa siku moja ama 2 baada ya Rais kuwa ameshaondoka Mbeya,je ujio wake hapo kesho ndio sababu?!!

Kwenye japo la mahakimu wanne,mmoja kukosekana hakuzuii watatu waliobaki kutokusema hukumu,kwa nini ihairishwe?!! Ujio wa raisi?!!

Binafsi inatoa taswira tayari kua hukumu hiyo ni ya kubumba,kama ni ya haki basi ingeendelea tu.

Kwenye familia ama maisha yetu,ukiwa unatenda ama unataka kutenda jambo la fedheha,husubiri kwanza umma utulie usikutane na heka heka, naona ndio haya!!
YAANI MBURURA MMOJA TU AISHINDE SERIKALI KLWELI??MNAJIDANGANYA HAPO HAKUNA KESI ISHJATUPILIWA MBALI VIGEZO HAVIJAKIDHI NA DP WORLD WANAENDELEA NA KAZI NYIE PIGENI KELELEEEE MPAKA MCHOKE
 
Itakuwa Jaji kapigiwa simu asionekane leo ili wahairishe

Atafutwe RC Juma Homera atuambie
Acha kuudogosha MUHIMILI wa mahakama....yaani mambo ya ndani ya mahakama aulizwe mkuu wa mkoa mh.Juma Homera?!!!

Yeye anahusika na kusimamia PROTOKALI ya ziara ya mpendwa Rais wetu SSH......
 
Tarehe 10 naamini utaona itatoka hukumu ya ajabu!! Chama na serikali nzima wanazunguka kupambana na Lissu na CHADEMA kuhusu Bandari.

Jambo zuri linajiuza,hapipigiwi debe!
Unataka kutolewa HUKUMU yenye kufurahisha MATAKWA ya nafsi yako ?!!

Hebu heshimu MIZANI ya muhimili huo wa dola.....
 
Umeona wapi jamii ikakaa kimya kupopolewa MAWE kwa kiongozi yeyote yule ?!!!!

Mh.Rais yuko Mbeya na haya mambo ya hukumu huvuta watu wengi maeneo ya mahakamani na mjini unataka watu wa PROTOKALI ya safari za Rais waridhie tu mchanganyiko wa majambo hayo mawili?!!!

Hivi shule tunakwenda kusomea "LGBT"?!!!
WANAFIKIRI RAIS NI MJOPMBA WO SHAME UPON THEM
 
Back
Top Bottom