Utafiti kwa kusoma Hukumu za Divorce Tanzania Ndoa nyingi zina migogoro sababu ya Dharau, Financial reasons ( Pesa) Na extended Family hasa mama wakwe

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
habari wadau

nilikuwa na utafiti binafsi wa mambo ya ndoa kwa ajili ya kukamilisha research thesis for academic reasons.

nilifika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke na kufanikiwa kuomba nakala za hukumu mbali mbali za kesi za ndoa ili zinisaidie utafiti wangu.

katika kusoma kwangu hukumu za ndoa zaidi ya 200. nimegundua ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu zinazofanana.

sababu kuu ni ya kwanza ni Pesa, yaani mapato na matumizii ya wanandoa, wanawake wengi wanaodai divorce wanalalamika wanaume zao kutotimiza jukumu lao la kipesa kutunza mke na familia nzima. na wanaume wengi wanalalamika kwamba wake zao wana matumizi mabovu ya pesa na wana demand za ajabu ajabu. kulazimisha familia iishi maisha fulani. na pia wake zao wamewaletea dharau za wazi wazi hasa pale mwanaume anapokosa pesa mfano anapokosa kazi na kuwa benchi. mke analeta dharau na kejeli ambazo zinafikia talaka

sababu nyingine ya kipesa ni wanandoa kuwa na Maoni yanayopingana kuhusu Pesa mfano mmoja anapenda kuinvest na mwingine anapenda kuspend kama kula bata. ndoa inaishia divorce.

MADENI pia yanavunja sana ndoa . ndoa yoyote ambayo ina wana ndoa wana madeni ya kipesa huwa inakuwa na migogoro mingi sana. madeni tu yaliyotokana na harusi tu huwa yanavunja ndoa nyingi sana

2. sababu ya pili extended family hasa mama wakwe. kwenye kesi nyingi za divorce nilizozisoma mama wakwe wametajwa. hasa mama wa mke kumfanyia maamuzi mwanae ya ndani ya ndoa yake. mke kaolewa ila bado anaongozwa kila kitu na mama yake mzazi. pia mama wa wanaume na wao wamelalamikiwa sana kwenye kesi nyingi.

3. sababu ya tatu ni Uzazi. mwanamke asiposhika mimba, wanaume wengi hasa wa kikristo wanazaaa nje ya ndoa huku hairuhusiwi hapo ndoa zinafikia divorce

NILICHOJIFUNZA KUCHEPUKA HAKUVUNJI NDOA. KAMA HIZO SABABU TATU NILIZOZITAJA HAZIWASUMBUI HAO WANANDOA. MWANAMKE HAVUNJI NDOA KWA SABABU MUMEWE KACHEPUKA KAMA MAMBO YA PESA KWENYE FAMILIA YAMENYOOKA, MAMA MKWE WAKE NI MTU POA KWAKE, UZAZI UPO POA KAZAAA WATOTO. HAPO NDOA HAIVUNJIKI HATA MUME AKICHEPUKA MARA MOJA MOJA SANA SANA ATAPAMBANA NA MCHEPUKO.


NIna hukumu za ndoa zaidi ya 300. bado naendelea kuzisoma hukumu zake. kwa wanandoa wapya hayo machache myafanyie kazi mkitaka ndoa zenu zidumu
 
Ni sahihi!

Nlicheka sana siku nliona jamaa kaanzisha uzi humu eti “nipate mwanamke wa kusaidiana nae maisha”
Nkacheeka nkasema ihiiiiiih(in Magufuli voice)

Seriously?
Mwanaume tafuta pesa
Kazi ya mkeo ni kutunza na kuviangalia vile unavyovimiliki
Na sio kukaa kizembe kumtegemea yeye
Nothing kitu mwanamke akafanya kikawa na matokeo mazuri kisilete mgogolo au namna yoyote ya dhihaka kwenye maisha yako(unless awe kakulia maisha ya kitajili
Ila hawa wa kajamba nani ni wabinafsi sana!

2 now kila kitu jamii imekigeuza kua normal
Mambo tuliona ajabu zamani now ni kawaida tu
Kuvunja ndoa sio kitu chakustaajabu tena
Matatizo ya leo sio hayatofautiani na yazamani
Ila kwanin hazikuvunjika kama leo? Ni kwakua uvumilivu hakuna
Watu wanaishi kwenda na wakati

Kuna mambo ya 50/50 nayo humohumo
Yaan kifupi a inaishia na z
Afu z inaishia na a

Usipoelewa soma tena
#nahapanmechokakuandika
 
Kuhusu fedha,

Marriage as an institution, needs Financial Management Skills applicable in any other institution. When it comes to finances, it's all about budgeting and brutal austerity, No debate!

Maana haiwezekani mmoja atafute hela kwa nguvu halafu mwingine aamini kwamba anaweza kuzitumia hovyo kana kwamba zinachumwa kwenye miti.
 
Na sio kukaa kizembe kumtegemea yeye
Nothing kitu mwanamke akafanya kikawa na matokeo mazuri kisilete mgogolo au namna yoyote ya dhihaka kwenye maisha yako(unless awe kakulia maisha ya kitajili
Ila hawa wa kajamba nani ni wabinafsi sana
This is very true......Wanaume wengi wameishia kuwa Kondoo tu na kuugulia Maumivu.

Pesa ya mwanamke hainaga maana kwenye maisha ya Mwanaume zaidi ya kuleta migogoro tu.
 
Marriage as an institution, needs Financial Management Skills applicable in any other institution.

Lessons on Financial Management should be made compulsory, starting frome Middle-School al the way up to College.

Maana haiwezekani mmoja atafute hela kwa nguvu halafu mwingine aamini kwamba anaweza kuzitumia hovyo kana kwamba zinachumwa kwenye miti kisa tu ni mwanandoa.
Maana haiwezekani mmoja atafute hela kwa nguvu halafu mwingine aamini kwamba anaweza kuzitumia hovyo kana kwamba zinachumwa kwenye miti kisa tu ni mwanandoa. Hii kitu isikie kwa watu tuuu. Na ndo mtindo wa leo. Ila cha ajabu,wanawake hawajiulizi unapoachika na kwenda kuolewa,unakuwa na thamani gani! Mwanaume anaejitambua,ataishi na wewe kwa tahadhali kubwa,huwezi kuwa huru. Na wengine,atahakikisha kwanza unachakaa,af unaishia kuwa single maza, ukibahatisha kijumba home,unarithishwa,af unaishia kupigia majirani taarabu.
Ila mbona hata wakimkimbia asiye na baiskeli kumtafuta mwenye gari,hawampati na yeye, wanaishia kupiga misele na kuwa vyombo vya kusuuzia mashine tu?!!!

Zamani walifundwa wakafundika. Siku hizi,balaa. Siku mwanamke aliyeanza kukaa na kuweka mguu mmoja juu ya mwingine,ndo uanamke wa kweli uliishia huko.
 
Halafu kuna mijitu inasema oa ukiwa maskini

Wee, thubutu
Hata ukiwa tajiri mkuu. Bora uishi kama ulivyozaliwa,una watoto,wahangaikie. Kumhangaikia mtu ambae hujamzaa! Utakoma.
Siku moja uamke unalalamikia kupigwa na kitu kizito. Kuna vibaka tofauti na hivi vya mtaani vilivyozoeleka. Huwezi kuvijua kama hujajichanganya. Bebi, gari haina mafuta. Bebi,nimekumiss. Bebi,nipo na marafiki zangu utatukuta Hotel flani tumemiss kuku.
Huyo huyo uanze kulalamika kwamba mkeo kashindikana.
 
FRESHMAN , binafsi siwezi kukubali kwamba wanawake wanachangia kuvunja ndoa.

Ndoa zinavunjwa na wanaume wenyewe. Niongeze,wasiojielewa.
Sasa hivi,unajua mwanamke unaemtaka, ni chuma chakavu. Atakuheshimu kwa lipi? Kwa kipi asichokijua toka kwa wengine? Kwa kipi hajapewa! Unakuta aliwahi nunuliwa Toyota Fortuner, wewe unakuja na ki Vitz au IST! Kila aina ya pombe alikunywa, wewe unaleta sijui Redds na King Fisher.
Wanaume walishatambulishwa ukweni kama kumbikumbi,wewe una nini?! Kubwa anaijua,ndefu anaijua,nene anaijua,nyembamba anaijua, mimba alitoa kama zote,bado tu kizazi; Af sasa,wanataka wale akipita tu,watu wote wageuke kwamba fulani ana demu mkali.
My friendo!!! Wale wameumbiwa kutumiwa kwa starehe tuuuu. Si yo wa kuoa. Sasa,wa kuoa,wanaonekana washamba,hawajielewi,hawana hela,hawana mvuto. Unakuta lijitu lina mikucha kama ya kenge,unategemea msaada gani?! Wewe hapo hata ukiugua,litakuacha ndani umuite mama yako akusaidie.

Zamani,wanaume walikua wanaoa wanawake wanaostahili kuolewa. Siku hizi,zama zimebadilika, wanaokota tu. Mtu hata kwao hupajui, hujui ndugu yake hata mmoja,kisa ana makalio makubwa,eti unaoa! Acha yawakute.
Unakuta lijitu limesomeshwa kwa mikopo na wazazi,kuliko liwajengee hata chumba na sebule visafi,linanunua gari la kuhonga.

Mreta mada, acha waachwe tu. Wanataka wenyewe
 
Back
Top Bottom