Wiki ya wanandoa: Talaka ya Davis Mosha, hukumu ya mauaji wifi wa mke wa Bilionea Msuya

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
Mfanano wa kesi:
Zote ni za kaskazini
Zote zinahusu mabilionea wakubwa Tanzania
Zote zinahusiana na utajiri, chuki, visasi.. No more

Utofauti
Moja ni talaka, wanandoa wote bado wako hai japo kuna tuhuma za kujaribu kuwekeana sumu
Nyingine ni ya mauaji, mwenye mali kafa, ndugu wanaona mke si halali kurithi utajiri wa brother.. Chuki na visasi vinaanza mpaka mauaji na hatimaye hukumu tata

Ni wiki ya mvurugano wa hisia mixer..furaha, huzuni, uchungu, ubabe, harufu ya rushwa, uchawi, ukengeufu wa sheria na mitanziko ya kila aina
Kwenye hizi kesi mbili huu sio mwisho bali ni safari nyingine mpya ya visasi na chuki kutokana na hukumu zake.. Na haya yatadumu kwa vizazi! Dunia ya mola hii
Kesi ya kwanza, kesi ya talaka mwanamke hajaambulia hata mia.. Maisha ya miaka 28 ya ndoa! Tangu first meeting, zile hisia za mapenzi motomoto, ndoa familia ... Struggle za maisha, kufanikiwa, mwisho wa hisia za upendo chuki, tuhuma za usaliti, tuhuma za kutaka kupeana sumu, kutengana na hatimaye talaka yenye maumivu makubwa! What's love!

Kesi ya pili
Mwenye mali hayupo kafa.. Zimejiinua roho tena za jinsia moja.. Vita imeanza baada ya mwenye mali kufa.. Pengine chuki zulikuwepo muda mrefu kimyakimya.. Ila watu walizihifadhi moyoni.. Kuna vifo ni hasara kubwa cha Msuya my home boy ni kimojawapo

Kuna familia hazipendani kwa tofauti za ndani ya familia.. Kuna familia zilipendana mpaka zilipokaribisha wageni.. (Wake na waume) sometimes waliowaza kuoana ndugu pengine walihofia maingizo mapya wasiyoyajua vema! Mengine ni Baraka lakini mengine ni laana!

Mali na utajiri.. Ndoa na ndugu
Vyote ni vizuri sana na vyote ni vibaya sana.. Inategemea utavitumiaje... Tembe ni tiba ya magonjwa ulitumia kwa usahihi..ni sumu ulitumia vibaya

Moto ni mzuri na wenye msaada mkubwa lakini moto huohuo umeleta maafa makubwa.. Mifano ni mingi sana!

ILA kuhusu utajiri
Kuna utajiri uliojaa baraka na kuna utajiri uliojaa maana
Utajiri uliojaa baraka huleta ndoa na familia za furaha zinazounganisha ndugu wote na kukosekana kabisa mapooza.. Utajiri uliopatikana kwa kuumiza wengine umejaa laana

Ni hukumu zenye mijadala mingi hasi na chanya lakini kiroho zinatufundisha mambo makubwa sana!
 
haya mambo sio mageni,yanatokea toka zama na zama,na hayazui chochote kuwa ndoa ni muhimu sana kwa wanadamu
 
ukiwa na pesa shida na usipo kuwa nazo shida
Biggiemomoneymoproblems.jpg
 
Kipindi cha JPM Wanawake walikuwa wanaishi Kwa furaha .

Kipindi cha SIR-100 Kila kona Wanawake wanamwaga machozi!!

Ni nini tafsiri yake?
 
Angekuwa anafuatilia crime documentaries zinazohusiana na mapenzi na mali..angetambua hili ni tatizo la dunia nzima..
Na ulaya liko waziwazi mno.. Mtu anafunga ndoa nawe kwa mahaba yote kisha anakukatia life insurance halafu anakutengenezea mchongo wa kifo ili alipwe mamilioni ya dola
 
JE, MUNGU YUKO UPANDE GANI KATIKA KESI YA MJANE WA BILIONEA MSUYA?

Mahakama Kuu imemuachia huru mjane wa Bilionea Msuya katika kesi ya mauaji iliyokuwa ikimkabili. Kwa upande wake, Mahakama Kuu imetenda haki. Lakini dada wa Bilionea Msuya na yeye ameibuka na kuilalamikia Mahakama Kuu kuwa haikutenda haki. Yeye anadai kuwa kabla ya hukumu hiyo, nyumba kule Upareni na Arusha zilikuwa zinapakwa rangi na wakisema kuwa atatoka kwa gharama yeyote ile.

Kama forensic investigation itafanyika kuhusu upakaji rangi wa nyumba na kama maneno yao yatakuwa yamerekodiwa na kuchunguzwa juu ya nani aliyeyasema inaweza kufubaza nguvu ya kimaadili ya hukumu hiyo kama kutakuwa na ukweli wowote? Je, watu waliokuwa wakisema maneno hayo walikuwa na maana gani kusema kuwa atatoka kwa gharama yeyote? Je, walijua kabla maudhui ya hukumu hiyo na ndio maana wakaanza kupaka rangi nyumba? Je, mawakili wa utetezi walijua kuwa hoja zao zilishinda na hata kabla ya jaji hajaanza kuiandika hukumu hiyo na wakaenda kuwaeleza ndugu wa mteja ndio maana wakaanza kupaka nyumba rangi?

Je, maneno ya dada huyo ni ya kupuuzwa? Je, kama yatapuuzwa wakati yameibua tuhuma nzito dhidi ya mahakama kwa kuihusianisha hukumu na mambo yaliyokuwa yakiendelea nje ya mahakama juu ya upakaji rangi wa nyumba kule Arusha na Upareni, taswira ya mahakama itakuwaje katika jamii?

Je, mahakama ina fursa ya kujitetea endapo watu wataituhumu nje ya mahakama kufuatia hukumu inazotoa? Ikitokea kuwa tuhuma hizo zina mashiko lakini walalamikaji wakaamua kutokukata rufaa kwa sababu mbalimbali kama kukosa imani na mahakama au kukosa fedha za kuendeshea kesi; mahakama inao ujasiri na uwezo wa kuamua kuipitia upya hukumu?

Je, maneno ya huyo dada yanaweza kuwaibua TAKUKURU kwenda Arusha na Upareni kwa ajili ya kuchunguza mazingira ya upakaji rangi hizo nyumba? Lakini kuna kosa gani kupaka rangi nyumba hata kama mhusika yu gerezani kama ndugu zake wanaweza? Lakini kuna kosa kwa ndugu wa mtuhumiwa kuamini kuwa mtu wao atatoka kwa gharama yeyote?

Je, kusema mtu atatoka kwa gharama ye yote ni kosa? Nini maana ya neno gharama ye yote? Je, dada wa Bilionea Msuya ndiye aliyekuwa ni mlalamikaji katika kesi hiyo au ni Jamhuri? Je, Jamhuri inaposhindwa katika kesi ya mauaji na ikaamua kuishia hapo, ndugu wa marehemu kama wao hawajaridhika watafanya nini?

Je, kuna mapungufu ye yote katika sheria zetu kwa kuacha dhamana ya kulalamika katika kesi ya mauaji mikononi mwa Jamhuri pekee bila ya familia au ndugu kuwa ni wadau pacha au hata walalamikaji wa moja kwa moja? Kama Mungu yuko upande wa wanaoonewa, unafikiri katika hili yuko upande gani? Je, yuko upande wa mke wa Bilionea Msuya au yuko katika upande wa dada wa Bilionea Msuya? Je kwa nini unafikiri hivyo? Unadhani haki haina gharama ye yote?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 24 Februari 2024; 1:07 usiku
 
Back
Top Bottom