Black Opal
JF-Expert Member
- Jan 22, 2023
- 304
- 543
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania mtu anayetuhumiwa au kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi hawezi kupata dhamana, kitu ambacho tulikitegemea kwa viongozi wa CHADEMA kina Lema, Heche, Boni Yai na Golugwa. Wawasumbue weee kama wanavyomsumbua Lissu, mwishoni DDP aseme hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Sasa imekuaje kwa viongozi wa CHADEMA waliokamatwa hivi karibuni? Imeakuaje wamepata dhamana kama kutuhumiwa na suala hilo hakuna dhamana?
Pia soma Polisi yawachia kwa DHAMANA viongozi wakuu wa CHADEMA waliokamatwa akiwemo Heche
Au kuna tobo ambalo wanasharia wanaliona sisi wengine ambao hatujui sheria hatuna elimu nalo? Embu mje mtusaidie hapa, hii imekaaje?
Kwa upande mwingine, ni presha ya maridhiano ndio imeleta yote haya baada ya Dunia nzima kusema uchaguzi haukuwa huru na haki? Sasa wanatafuta namna ya kuwapoza viongozi wa upinzani kukubali maridhiano?
Sitegemei Lissu akaja kukubaliana na haya maridhiano batili baada ya wenzetu zaidi ya elfu 2 kuuliwa! Akifanya hivi itakuwa ni usaliti mkubwa sana, yaani sitaki hata kufikiria.