Kesi ya Thadey Kweka: Utawala wa sheria, hauruhusu vyombo vya uchunguzi na mahakama, kuvunja haki za kikatiba na sheria, katika utoaji hukumu zake

Kesi ya Thadey Kweka: Utawala wa sheria, hauruhusu vyombo vya uchunguzi na mahakama, kuvunja haki za kikatiba na sheria, katika utoaji hukumu zake

Nia yako ni njema; kutaarifu wasomaji juu ya swala ulilozungumzia; lakini kwa bahati mbaya sana umetumia maneno meeengi mno, ambayo hayakusaidia kamwe kufikisha ujumbe.

Ni kama unaelezea jambo ambalo kila msomaji wa mada yako analifahamu tayari, na wewe ni kama unatoa ufafanuzi tu wa jinsi mambo yalivyoendelea.

Huyo Kweka anashtakiwa kwa kosa gani; kwa mfano??

Ungetumia mstari mmoja au miwili kuhusu taarifa hiyo ya awali ingesaidia wasomaji wako kupata pa kuanzia kuelewa unachokizungumzia kwenye mada.

Nimejitahidi sana kusoma andiko lako hilo refu nikiwa na matumaini kwamba labda nitakutana na taarifa muhimu huko katikati ya andiko. Nilipofika katikati na kuendelea na mizunguko, nikakata tamaa kuendelea huko chini!
Rudi darasani kidogo uongeze ufahamu
 
UPDATE 5: Kesi ya Thadei Kweka

December 31, 2025

1. Upande wa Jamuhuri wamepeleka Maombi (Ex-parte) Mahakaman kwa hati ya dharula na yamesikilizwa Upande mmoja bila Thadey Sabinus Kweka kuwepo Mahakaman ukizingatia kuwa yupo mikononi mwao.

2. ⁠Maombi hayo yanahusu kumtaka Thadey Sabinus Kweka kutoa Nywila (password) za simu yake ili Polis wafanye upelelezi.

3. Mahakama imetoa Amri kuwa Thadey Sabinus Kweka anatakiwa kutoa Nywila (password) za Simu yake ili Polisi wafanye uchunguzi.

4. Thadei ameshindwa kutoa password kwa sababu haikumbuki baada ya kupitia unyanyasaji wa kisaikolojia tokea akamatwe. Zoezi la kutoa password limeshindikana hadi kesho Thadei akikumbuka password yake.

5. Polis bado wamemkatalia Thadei dhamana na kusaini consent forms kutoka ubalozi wa Marekani ili America iwe involved.

6. Thadei anashtakiwa kuchapisha taarifa za uongo kwenye groups za ”what sup”. What sup hatujui ni Application gani haya Thadei mwenyewe haelewi!

Tutaendelea kuwapa taarifa.

#FreeThadeiKweka

AsanteView attachment 3523512
Ukisoma pleading zao hakuna maombi ya Exparte and for that sake it was inter-Parte iliyofantika Exparte ili kutimiza nia ovu ya wanaoshitaki
 
Tunasafari Ngumu ya Kujifunga Mkanda Kupata Katiba Mpya itayoweka misingi ya Uhuru wa Mhimili wa Mahakama. Unapoona Mahakama inashirikiana na Wakamataji na Washitaki kwa kupuuza haki za binadamu ni hatari sana
It's true, tuna safari ndefu, ila kwa vile kumetokea fursa ya katiba mpya, twende na upepo huo kuboresha haki
, wajibu na uwajibikaji.

P
 
Tatizo zaidi viongozi wa kitaifa hawaoni najisi waliyoifanya.

Saa zingine kuna mambo unayaachia fate.
Kuachia 'fate', hilo ndilo tumaini zima wanalolisubiri hawa watawala waovu kabisa!

Hakuna 'fate' isiyokuwa 'influenced' na utashi wa watu. Fate ya hawa waovu itapatikana kupitia kwenye juhudi za waTanzania wasiokubali upuuzi huu.
 
Uko sahihi.
Polisi kiutendaji ni kama vile wako juu ya sheria.
Ukiangalia hata taarifa ambazo ilistahili zitolewe na waziri wa mambo ya ndani zinatolewa na polisi.
Kwa sababu huyu waziri hapo ni pambo tu; wahusika hasa wanaoendesha jeshi hilo ni wengine.
 
Rudi darasani kidogo uongeze ufahamu
Kwa bahati nzuri ninao ufahamu mzuri sana, mkuu 'Emekha Ikhe'; kwa hiyo ushauri wako huu unaonyesha bado huelewi nilichokieleza kwako.
Ukitulia na kutofakari vizuri ushauri niliokupa, utaona ukweli ulipo.

Haikuwa maana yangu ya kudharau ulichowasilisha; maana yangu ni kukustua uone upungufu katika uwasilishaji wako, jambo ambalo najuwa unaweza kulimudu.
 
UPDATE 6: Kesi ya Thadei Kweka

January 1, 2026

1. Mawakili wa Thadei wame—file Habeas corpus ili afikishwe mahakamani haraka. Matarajio Jumatatu kesi itasikilizwa

2. ⁠Pia, Mawakili wame—file revision (marejeo) ya maamuzi kumtaka Thadei atoe password ya simu yake kwani kuna suala la kukiuka haki ya kimsingi ya privacy.

3. Bado Thadei ameshindwa kutoa password kwa sababu haikumbuki baada ya kupitia unyanyasaji wa kisaikolojia tokea akamatwe. Zoezi la kutoa password limeshindikana hadi hapo Thadei akikumbuka password yake.

5. Polis bado wamemkatalia Thadei dhamana.

6. Leo Thadei amesaini form kutoka Ubalozi wa Marekani baada ya pressure kubwa kutoka Ubalozi wa Marekani.

7. Thadei anashtakiwa kuchapisha taarifa za uongo kwenye groups za ”what sup”. What sup hatujui ni Application gani haya Thadei mwenyewe haelewi!

8. ⁠Thadei yupo kwenye spirit nzuri na anawashukuru diaspora kwa kusimama naye na anatambua hii sijui vita dhidi yake, bali ni vita dhidi ya diaspora wote.

Tutaendelea kuwapa taarifa.

#FreeThadeiKweka

Asante
1767401070406.jpg
 
Waja hawana wema wanadai video ya hotuba ni AI generated inawezekana hata mukulu hakuongea kabisa
 
Nimesoma HUKUMU ya Kesi ya THADEY KWEKA ambayo imetolewa jana kinyemela hata bila yeye mwenyewe kujitetea au kutetewa na Mawakili wake tangu kukamatwa kwake, Ninasikitika Kuona kwamba hata Mahakama kupitia Hakimu imejielekeza Vibaya Kutoa HUKUMU husika

Raia Wanategemea Mahakama itende Haki na sio kushirikiana na Vyombo Vya Ukamataji na Uchunguzi kuminya Haki za KIKATIBA za Mtuhumiwa kama ambavyo nitaeleza Juu ya Sakata la THADEY KWEKA kama nyaraka zinavyojifafanua, binafsi nitaandika kwa ufupi na straight to the point

Kitendo cha Ofisi ya DPP kufungua kesi dhidi ya Mtuhumiwa (Thadey Kweka) ya kuitaka Mahakama kutoa Amri dhidi ya KWEKA ili atoe Nywila(Password) yake ili Polisi na Ofisi ya DPP kufanya Uchunguzi, na kesi Kusikilizwa na Mahakama hata bila Mtuhumiwa kupewa wito ili kuwepo kwa utetezi au kutetewa na Wakili wake, Kunaibua maswali Mengi ya kisheria dhidi ya Vyombo Vya Uchunguzi pamoja na Mahakama yenyewe

Mosi, Kesi umesikilizwa Upande mmoja kwa hati ya dharura bila mtuhumiwa wala Wakili wake kujulishwa kwa wito wa Mahakama huku kesi iliyofunguliwa ikiwa Inter-Parte Application (Kwamba Mtuhumiwa alipaswa kupewa wito kwa utetezi) na sio Exparte Application (Kwamba kesi isikilizwe Upande mmoja kulingana na nyaraka zilizofailiwa

Ukisoma Wito wa Mahakama( Chamber summons) hauonyeshi kwamba kesi hii ilikuwa ya Kusikilizwa Upande mmoja (Exparte Application) hivyo, Thadei alipaswa kuwakilishwa na Wakili au kujiwakilisha katika utetezi wake ili Kutekeleza Haki ya Asili ya Kusikilizwa inayolindwa na Katiba ya Nchi kabla ya Mahakama Kuja na Uamuzi uliotolewa

Bahati Mbaya sana Hakimu aliyetoa Uamuzi anakili kwamba kesi hii ilikuwa kwa hati ya dharura ili isikilizwe Upande mmoja kinyume na nyaraka zilizowasilishwa Mahakamani na Hakimu anaamua kesi husika bila kutii Katiba ya Nchi na Sheria zake kama nitavyofafanua hapa;

Mahakama hazina Mamlaka ya ku-dis regard Haki za Msingi za Kikatiba mathalani haki ya Faragha (Right to privacy) bila Kutoa Haki ya Kusikilizwa kwa Mtuhumiwa (Principle of Natural Justice) kama ambavyo Hakimu alivyojielekeza vibaya katika Uamuzi wake unaopswa kukatiwa Rufaa haraka iwezekanavyo

Pia Kifungu cha 32 cha Sheria, Cyber Crime Act, licha ya kwamba Kifungu hiki kimeipa Mamlaka Mahakama Kutoa Amri husika, Sheria husika haijaipa Mamlaka Kufanya Maamuzi kwa KUVUNJA Sheria na Katiba ya Nchi, hususani kukinzana na matakwa ya Katiba juu ya Haki ya Kusikilizwa (Fair hearing) kabla ya uamuzi

Ifahamike kuwa, Polisi na DPP hawezi Kumkamata Mtuhumiwa kwa tuhuma hewa za jinai ( kupublish Taarifa za UONGO (False nformation) bila kuzitaja in specific kama Kifungu cha 32 cha Sheria ya Cyber crime Act kinavyotaka

Ni Bahati mbaya sana Hakimu huyu wa Mahakama(RMC) ametoa HUKUMU ya Amri ya Mtuhumiwa Kutoa nywila zake bila kujua ziitwazo Taarifa za UONGO ni zipi ambazo zilipelekea Mtuhumiwa kukamatwa kama Sheria inavyotaka

Ni takwa la Sheria zetu kwamba,Mahakama katika Kutoa HUKUMU au Uamuzi wake haswa katika kesi ya Jinai inapaswa kuongozwa kanuni ya kuthibitisha bila Shaka (Prove Beyond Reasonable drought), kwenye hili Mahakama imejielekeza Vibaya hivyo Uamuzi husika unapaswa kukatiwa Rufaa haraka

Hatuwezi tukawa na Mahakama ambazo Hakimu anaamua kesi ya Jinai bila kujua in specific( details za kosa (criminal offence), bila kumpa Haki Mtuhumiwa kujitetea au kutetewa na Wakili wake (Fair hearing) na Kutoa Maamuzi

Hii ruling inapaswa kukatiwa Rufaa haraka, Ni Muhimu Mahakama zetu kujiongoza vyema katika Kulinda Haki za Binadamu ambazo zinalundwa na Katiba ya Nchi yetu
Kwa hiyo umekuwa ni hakimu
 
#UPDATE_ISSUE_THADEI_KWEKA

Anaandika Liberatus Mwang'ombe

January 3, 2026

1. Mwanzoni December 28, 2025 alipo kamatwa aliambiwa ana kesi ya kuingia nchini sio kihalali.

2. Jumatatu, December 29, 2025, Thadei alichukuliwa hadi uwanja wa ndege KIA kwa escort ya polis. Record za airport zikaonyesha Thadei aliingia kihalali December 20, 2025

3. Thadei alitolewa Boma Ng’ombe akiwa na tuhuma za kuingia bila kibali. Akahamishiwa Central Polis Moshi mjini na kuambiwa anatuhuma za kuchapisha habari za uongo “What sup”

4. Muda wote huu hakukuwa na proper charges.

5. Leo, Jumamosi, January 3, 2025 Thadei amepewa dhamana baada ya siku 7 kuwa ndani.

6. Jumatatu, kesho kutwa, kesi ya marejeo ya hukumu ya upande mmoja ili Thadei atoe Password inatarajia kusikilizwa. Pia, kesi ya dhamana.

7. Thadei hadi sasa ameshindwa kufungua simu yake kwa sababu haikumbuki password baada ya stress zilizosabaishwa na kukamatwa bila utaratibu. Simu yake bado ipo polis.

8. Thadei yupo kwenye spirit nzuri na anawashukuru diaspora kwa kusimama naye na anatambua hii siyo vita dhidi yake, bali ni vita dhidi ya diaspora wote.

#FreeThadeiKweka
1767487720268.jpg
 
Back
Top Bottom