Mpinzire
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 7,223
- 12,943
Nimekuwa nikisikia mara nyingi kuwa kauli ya Rais ni sheria! NImejaribu kupekua Katiba yetu ya Tanzania ya mwaka 1977 na marekebisho yake ya mwaka 2008 sijaona ibara yoyote ya katiba yetu kuwa atakacho zungumza Mh Rais ni sheria!
Leo Waziri Mkuu anaibuka anakazia maneno ya Mh Rais kuwa TRA waachane na madeni ya malimbikizo ya kodi ya miaka ya nyuma kama Mh Rais alivyokasema huko nyuma! TRA wao wanapoenda kwa Wafanyabiashara wanadai madeni ya miaka ya nyuma bado! mfanya biashara akiuliza anajibiwa hizo ni kauli za majukwaani tu mi nafuata sheria.
Kwanini Serikali haioni haja ya kupeleka muswada Bungeni ili ipitishwe sheria ya kufuta malimbikizo ya madeni ya huko nyuma? Utawala Bora msingi wake si kufuata Katiba na Sheria?
Tamko la Rais linalindwa na sheria hipi au ibara hipi katika Katiba yetu?
Wanasheria kazi kwenu