Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 34,691
- 40,944
DC wa Wilaya ya Mjini Unguja amepiga marufuku kwa watu wa jamii ya kimasai kutembea na rungu na sime akiviita kama silaha.
View: https://youtu.be/W-xkQJRDO0c?si=AFIG5omTxVoCeNyZ
Kauli yake si tu inavunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali inakiuka mikataba mbali mbali ya kimataifa ambayo Tanzania imeiidhinisha inayolinda haki ya raia kushiriki katika mambo ya kitamaduni.
Rejea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 13.
Rejea, Universal declaration of Human Rights, 1948.
Rejea, International Covenant on Economic, Social and Cultural rights.
Sheria zote hizo zinaipa serikali wajibu wa kulinda na kutengeneza mazingira kwa raia wake kuishi wakiwa na uhuru wa kufuata tamaduni zao.
Rungu na sime ni moja wapo ya utambulisho wa tamaduni ya wamasai inayokwenda pamoja na vazi la Rubega.
Kuwapiga marufuku wamasai kufuata tamaduni zao si tu kwenda kinyume na haki za binadamu bali ni kukiuka misingi yote iliyowekwa na jamii za kistaarabu katika kuhakikisha kuwa binadamu anafurahia uwepo wake duniani bila kunyanyapaliwa na mwenzake.
Kauli hii ya DC si tu ya kibaguzi bali inahatarisha ustawi wa Muungano na amani katika nchi.
Ni jambo la kukemewa na kila mwenye nafasi ya kufanya hivyo.
Nakuomba Rais Mwinyi usiache kumchukulia hatua DC huyu au la itatafsiriwa kuwa haya ni maagizo yako na itaingia katika historia ya Taifa kuwa katika utawala wako uliwahi kukandamiza haki za wengine.
Usione aibu kuchukua hatua.