Katiba bila elimu ni kazi bure haitatusaidia

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,683
22,270
Viongozi wa CCM wamekuwa wakitu elezea kuwa ili katiba iwe na manufaa kwetu inabidi wananchi tuelimishwe hiyo katiba, hilo ni jambo jema.

Elimu hiyo yenye viwango vya chuo itatolewa na viongozi wa CCM ambao hatujui waliwezaje wao kusoma wakatusahau wananchi, hata hivyo darasa ni darasa wapo watakaopasi na watakaofeli, idadi ya watakao feli ikiwa kubwa ina maana lengo la wananchi kuijua katiba litakuwa halijafikiwa hivyo itabidi darasa lirudiwe tena mpaka tutakapo pasi!

Ninamalizia kwa kusema CCM hawana nia ya uwepo wa katiba mpya kutokana na mambo wanayoyafanya hivi sasa kwani wengi wao wamegeuka kuwa wafanyabiashara na huenda katiba itawabana huko tuendako.
 
Kwahiyo tukimaliza kupewa elimu, tutafanyishwa mitihani na watakao feli wataendelea kurudia mitihani ya katiba hadi nchi nzima na wanao zaliwa wafaulu mtihani wa katiba ndio tupate KATIBA MPYA
 
Wamebanwa sasa wanataftiza visababu visivyo na maana, hilo darasa la wazee na watu wazima litafanyikia wapi! Katiba siyo lazima yote uijue kichwani bali unapokuwa na hitaji la kipengele fulani ndipo unachokitumia kutoka kwenye kitabu cha katiba kupitia wanasheria.
 
Ugali mezani ni udanganyifu
Sasa hawa wanaowashawishi watu kwa hoja mfu ndio tunaambiwa watatuelimisha kuhusu katiba! CCM wameishiwa sababu za kuikataa katiba ndicho kinachowafanya wakimbilie kuwa wanatukanwa, huku matusi hayapo na watukanaji hawawajui.
 
Viongozi wa CCM wamekuwa wakitu elezea kuwa ili katiba iwe na manufaa kwetu inabidi wananchi tuelimishwe hiyo katiba, hilo ni jambo jema.

Elimu hiyo yenye viwango vya chuo itatolewa na viongozi wa CCM ambao hatujui waliwezaje wao kusoma wakatusahau wananchi, hata hivyo darasa ni darasa wapo watakaopasi na watakaofeli, idadi ya watakao feli ikiwa kubwa ina maana lengo la wananchi kuijua katiba litakuwa halijafikiwa hivyo itabidi darasa lirudiwe tena mpaka tutakapo pasi!

Ninamalizia kwa kusema CCM hawana nia ya uwepo wa katiba mpya kutokana na mambo wanayoyafanya hivi sasa kwani wengi wao wamegeuka kuwa wafanyabiashara na huenda katiba itawabana huko tuendako.
Na ikumbukwe,kila siku wanazaliwa Watanzania wapya.Vilevile kuna wale waliokuwa wakiishi nje ya nchi au waombao uraia ambao bila shaka watakuwa hawajapata tuisheni ya katiba.Sasa sijui hilo darasa litachukua karne ngapi?
Jambo hilo halina tofauti na ndugu zangu hapa nyumbani wanaong'ang'ania watoto wetu wabatizwe(Wakristu)wafikishapo umri wa kujitambua.Niliwashauri,hata kunyonya na chakula tusiwape hadi wakue,wajitambue na wachague wanachotaka wao.Sikuishia hapo.Nilishauri,wasiwape mavazi wala wasiwapeleke shule hadi pale watakapokuwa watu wazima na kuchagua wakipendeleacho.
 
Viongozi wa CCM wamekuwa wakitu elezea kuwa ili katiba iwe na manufaa kwetu inabidi wananchi tuelimishwe hiyo katiba, hilo ni jambo jema.

Elimu hiyo yenye viwango vya chuo itatolewa na viongozi wa CCM ambao hatujui waliwezaje wao kusoma wakatusahau wananchi, hata hivyo darasa ni darasa wapo watakaopasi na watakaofeli, idadi ya watakao feli ikiwa kubwa ina maana lengo la wananchi kuijua katiba litakuwa halijafikiwa hivyo itabidi darasa lirudiwe tena mpaka tutakapo pasi!

Ninamalizia kwa kusema CCM hawana nia ya uwepo wa katiba mpya kutokana na mambo wanayoyafanya hivi sasa kwani wengi wao wamegeuka kuwa wafanyabiashara na huenda katiba itawabana huko tuendako.
TUME ya JAJI WARIOBA ilizunguka NCHI ZIMA na kutoa ELIMU na kugawa NAKALA za KATIBA na VIPEPERUSHI Kwa Wananchi
UKWELI USEMWE CCM HAITAKI KATIBA MPYA kwani DANADANA zimezidi
 
Anayeijua katiba anavunja katika, sasa hiyo elimu kwa asiyejua inamaana gani?
Watanzania mwalimu Nyerere alisema viongozi wa nchi wakiwa wafanyabiashara watawasahau wananchi, hiki ndicho kinatokea sasa ambapo viongozi wako bize kutafuta mipenyo ya kuendeleza biashara zao. Hii mipenyo ni kutengeneza namna za kujilinda na njia bora na yenye uhakika ni kuhakikisha nchi haina katiba inayoeleweka hivyo wananchi tunakosa nguvu ya kuwadhibiti.
 
Mbona kwenye kutunga sheria au kuzifanyia marekebisho huwa hawasemi hiyo elimu inahitajika kwanza?
 
CCM kama alivyosema mzee Msuya hivi sasa ina watu ambao hawajui kuweka hoja kama walivyo Chadema na amewashauri wajifunze toka Chadema.
 
TUME ya JAJI WARIOBA ilizunguka NCHI ZIMA na kutoa ELIMU na kugawa NAKALA za KATIBA na VIPEPERUSHI Kwa Wananchi
UKWELI USEMWE CCM HAITAKI KATIBA MPYA kwani DANADANA zimezidi
Bora wangechagua kukaa kimyaa kuliko hayo waliyoyasema.
 
Back
Top Bottom