Ijue Katiba ya JMT kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Wanabodi,

Kama kawa, kila nipatapo fursa

TUSISHABIKIE UHAINI.png

Kufuatia tishio la matamshi yenye viashiria vya uhaini dhidi ya serikali ya JMT kwa baadhi ya watu, na watu hao kushikiliwa na vyombo vya dola, waneibuka watu, mashirika, wanaharakati kupigia kelele kuna kesi ya uhaini, na hadi baadhi ya taasisi za kimataifa kutaka kuingilia kati mambo yetu ya ndani!, hivyo kufuatia mwandishi wa makala hizi kuwa pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, naomba kuitumia makala ya leo, kuanza mfululizo wa makala elimishi kuelimisha umma kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu kwa jicho la mtunga katiba.

Naomba nianze na elimu fupi kuhusu makosa mawili makubwa kuliko makosa yote kwenye katiba yetu. Makosa haya ni kosa la kuua, (murder), na kosa la uhaini, (treason), ambayo yote adhabu yake ni kifo, au "capital punishment", na kwa Tanzania adhabu hii inatekelezwa kwa kunyongwa hadi kufa, kwa nchi yetu tuna gereza moja tuu la kunyongea ni gereza la Isanga, liko Dodoma.

Mtu akihukumiwa kifo, adhabu hii haitekelezwi mpaka kwanza isainiwe na rais wa JMT, hati inayoitwa Hati ya Kifo, (death warrant), na baada ya kusainiwa, mfungwa huyo hupimwa na dakitari bingwa wa hospitali ya serikali kuthibitisha ni mzima na bukheri wa afya, ndipo hunyongwa!. Ikitokea mnyongwa nni mgonjwa wa ugonjwa wowote ikiwemo afya ya akili, adhabu hiyo haitekelezwi hadi mgonjwa atibiwe apone kabisa, apimwe tena, akikutwa ni mzima, ndipo atiwe kitanzi!. Na ikitokea ana maradhi yasiyopona, kama kifafa, au maradhi ya kuambukiza kama ukimwi , kifua kikuu na ukoma, mnyongwa huyo hanyongwi, hutengwa na kulishwa tuu na kulala, yaani kula kulala, mpaka...

Kwa Tanzania, awamu ya kwanza ya utawala wa Baba wa taifa hili wa Mwalimu Nyerere, uliodumu kwa miaka miaka 23, Mwalimu Nyerere asisaini death warrant 2.
Awamu ya pili ya Miaka 10 ya Rais Mwinyi, alisaini hati kadhaa. Awamu zilizofuata za Rais Mkapa, Rais Kikwete, na Rais Magufuli, hakuna death warrant yoyote iliyosainiwa na ndio maana sisi watetezi wa haki za binadamu, tunapendekeza adhabu hii ifutwe.

Sio kila mauaji yakifanyika ni kesi ya murder, kuna mauaji yanaweza kufanyika na ikawa sio kesi ya murder, bali inakuwa ni kesi ya manslaughter, yaani kuua bila kukusaidia. Ili kesi ya mauaji kuwa murder lazima kufanyike mambo mawili, jambo la kwanza ni kitu kinachoitwa "actus reus", kitendo cha mauaji, na "mens rea", nia ovu ya kutenda mauaji, yaani dhamira ya kuua au kukusudia kuua. Vivyo hivyo, uhaini hauwezi kutendeka kwa kauli tuu bila actus reus na mens rea!

Uhaini ni nini? Uhaini umetajwa kwenye sura ya Saba kifungu cha 39 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, yaani penal code kinasema Kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais.

Kwa mujibu wa sheria tuliofundishwa darasani, uhaini ni vitendo na sio kauli ni uchochezi!. Kwa vile mpaka sasa hakuna mashitaka yoyote ya uhaini yaliyofunguliwa katika Mahakama yoyote, nawaombeni Watanzania wenzangu tusishabikie uzushi wa uhaini, hili sio jambo la kheri hata kidogo.

Vivyo hivyo kwenye jinai ya uhaini, sio kila matamshi ya uhaini ni uhaini, ili kuwepo kwa jinai ya uhaini, lazima kuwepo kwa zile sifa kuu mbili, actus reus na mens rea ya kupanga kufanya uhaini. Kitendo cha mtu ameghafilika tuu na hoja za Club House, akaanza kuhororoja kutoa matamshi ya kupindua serikali, haimaanishi ni uhaini wa kupindua kweli serikali, lakini matamshi hayo yanaweza kuwa ni matamshi ya uchochezi hivyo kusababisha watu wapange kweli kupindua serikali, lakini matamshi tuu kama matamshi bila ya kuwepo means rea ya kupindua serikali, watu hao watakuwa wamefanya kosa la sedition na sio treason.

Kitendo cha watu haswa wanaharakati kupiga kelele uhaini, kuiongopesha dunia na kufanya nchi yetu kuangaziwa vibaya kimataifa, wakati hadi ninapoandika hapa, hakuna kesi yoyote ya uhaini iliyofunguliwa popote, hivyo huku kushabikia na kushadadia uhaini sio jambo jema, ni kutaka kumchafulia bure huyu Mama wa watu ile sifa yake kuu ya kuliponya taifa!

Tanzania toka tumepata uhuru, tumewahi kuwa na kesi 5 za uhaini, kesi ya kwanza ni ile ya maasi ya jeshi ya tarehe 18 January 1964, siku 6 baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, jeshi la KAR liliasi, likavunjwa ndio likaundwa JWTZ. Kesi hii iliendeshwa kijeshi, hivyo wala sijui matokeo yake.

Kesi ya kwanza ya uhaini katika Mahakama ya wazi ni kesi ya kina Bibi Titi Mohamed, John Lifa Chipaka, Michael Kamaliza na wengine ya mwaka 1971.

Ikaja kesi ya uhaini inayomhusu aliyeitwa Juma Thomas Zangira.

Mwaka 1982 ndio kulifanyika kesi ya uhaini ya watu 38, wakiongozwa na Pius Lugangira na Hatibu Ghandi ambapo sterling wa kesi hiyo ni komandoo Martin Tamimu aliyeuwawa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

Hapa katikati kukatokea kesi ya mwisho ya uhaini Zanzibar ya kina Seif Sharrif Hamad, Shabani Mloo, Juma Duni Haji, Machano, Hamad Rashid na wengine 18 wa Chama cha Wananchi CUF, kesi hii ikatupiliwa mbali baada ya Mahakama Kuu kutamka kwamba Zanzibar sio nchi, hivyo jinai ya uhaini haiwezi kutendeka!.

Ili kuwasaidia Watanzania kuzijua haki zao, najitoelea kuelimisha umma kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu.

Somo la kwanza ni katiba.
  1. Utangulizi: Hizi ni makala elimishi kutoa elimu ya uraia kwa watu wa kawaida kuijua katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977.
  2. Mtoa Mada ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea kutetea haki katiba na kujitolea kutoa bure elimu ya katiba kuelimisha umma kuhusu katiba kwa jicho, nia na dhamira ya mtunga katiba alidhamiria nini?
  3. Hivyo kupitia safu hii ya kwa maslahi ya Taifa, Ijue Katiba, hizi ni makala elimishi, kuwasaidia Watanzania sio tuu kuijua katiba ya JMT, bali pia kuelewa mtunga katiba alidhamiria nini alipoweka kifungu fulani.
  4. Hii ni makala ya kwanza ya Katiba ni nini?, katiba ni ya nani? na ni ya kazi gani?
  5. Katiba ni kama Biblia Takatifu au Msahafu yaani Quran Tukufu, imeandikwa law maandishi, hivyo kila anayejua kusoma na kuandika anaweza kuisoma Biblia au Msahafu, lakini kwa bahati mbaya sana, sio kila mtu ana uwezo wa kuisoma na kuielewa, hivyo kuna watu maalum ambao wanavisoma hivi vitabu vya dini na kuwaelimisha wengine, kwenye dini mara nyingi ni viongozi wa dini, lakini kwenye siasa ni viongozi wetu wa siasa.
  6. Kama ilivyotokea kwenye dini, sii wote wanaweza kuisoma Biblia/Msahafu na kuielewa, kuitafsiri, na kuwaelewesha wengine, ni kazi inayofanywa na wachache walijaaliwa uwezo huo, hawa huitwa wahubiri.
  7. Vivyo hivyo, sii wote wana uwezo wa kuisoma katiba, kuielewa, kuitafsiri, na kuwatafsiria wengine, sasa kwa vile mimi mwana JF mwenzunu nimejaaliwa kauwezo fulani kadogo tuu cha kuisoma katiba na kuielewa kwa jicho la mtunga katiba alidhamiria nini, hivyo sasa naitumia dhamira ya mtunga katiba kwa uelimishaji umma kuhusu katiba, na dhamira ya mtunga katiba, hivyo sasa naanzisha darasa rasmi la elimu ya Ijue Katiba ya JMT ya mwaka 1977 kwa jicho la mtunga katiba.
  8. Hivyo kupitia safu hii ya Ijue Katiba, hizi ni makala elimishi, itawasaidia Watanzania kuijua katiba ya JMT na mtunga katiba alidhamiria nini kwa vifungu mbalimbali vya katiba.
  9. Hii ni makala ya kwanza ya Katiba ni nini na katiba ni ya nani?.Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ndio katiba ya JMT.
  10. Katiba ni Nini?. Katiba ni kakitabu kadogo tuu chenye kurasa 43!. Kakitabu haka ndio kila kitu kuihusu Tanzania yetu, hakuna yeyote aliye juu ya Katiba.
  11. Katiba ni ya Kazi Gani. Katiba ndio msingi Mkuu na muongozo wa uendeshaji wa nchi yetu, ambapo sheria zote, taratibu zote na kanuni zote, za kufanya kila jambo, lazima zitokane na katiba.
  12. Misingi ya Katiba- Katiba yetu imeweka misingi mikuu 4 ya katiba ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani.
  13. Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.
  14. Katiba ni ya Nani? Katiba hii imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.
  15. Hivyo kwa mujibu wa katiba hii, kitu muhimu kabisa kwa Taifa la Tanzania, ni watu!, Watanzania, hawa ndio wenye katiba!, katiba ni mali ya Watanzania. Ni watu hawa Watanzania, walioweka misingi mikuu minne ya katiba yetu, uhuru, haki, udugu na amani. Msingi mkuu wa kwanza wa katiba yetu ni uhuru, wa pili ni haki. Hivyo vitu vitu viwili vikuu vya katiba yetu ni uhuru na haki.
  16. Hivyo viongozi wetu tukiisha wachagua kwa mujibu wa katiba katika uchaguzi huru na wa haki, ulioendeshwa na tume huru ya uchaguzi, tunawaapisha kwa katiba waape kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa katiba na kuilinda na kuitetea katiba ya JMT.
  17. It's very unfortunately baadhi ya viongozi wetu hawa nao wako kwenye kundi lile lile la wasoma katiba wasioielewa katiba, wanachaguliwa kwa mujibu wa katiba wasioifahamu!, na waapa kuilinda katiba wasioilewa na mwisho wa siku, badala ya kuilinda katiba, wao ndio kwanza wanakuja kuivunja katiba innocently kwasababu hawajui watendalo kuwa ni kinyumecha katiba!.
  18. Katika uendeshaji wa nchi, tuna mihimili 3 ya Dola inayoendesha nchi yetu, mihimili hii ni Serikali, Bunge na Mahakama. Ili kuendesha nchi kuna watu muhimu sana, ambao wanatajwa na katiba ili kuhakikisha katiba inafuatwa, hawa ni wanasheria.
  19. Tuna wanasheria serikalini, tuna wanasheria Bungeni na tuna wanasheria Mahakamani, ambao ndio walipaswa kuijua katiba!, lakini it's very unfortunately, baadhi ya wanasheria hawa nao pia hawaijui katiba!. Matokeo yake ni Serikali inatunga sheria batili na viongozi wa serikali wanavunja katiba, Bunge linavunja katiba kwa kutunga sheria batili.
  20. Mahakama nayo yenye jukumu la kutafsiri katiba na sheria, ambayo imeshehenezwa wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, baadhi yao ni just too blind to see, katiba inavunjwa, mahakama ipo inaangalia tuu!, kwa kusema "the court is not the custodians of the will of the people!" ... my foot!
Mwisho wa sehemu ya kwanza ya Ijue katiba ya JMT ya mwaka 1977 kwa jicho la mtunga katiba.
Sehemu ya pili ni maana ya Katiba ni sheria Mama, ina maana gani?.

Wasalaam
Paskali
 
Mwalimu Nyerere asisaini death warrant 2.
Awamu ya pili ya Miaka 10 ya Rais Mwinyi, alisaini hati kadhaa. Awamu zilizofuata za Rais Mkapa, Rais Kikwete, na Rais Magufuli, hakuna death warrant yoyote iliyosainiwa na ndio maana sisi watetezi wa haki za binadamu, tunapendekeza adhabu hii ifutwe.

Hivi toka huyu Rais wa awamu ya sita kuingia madarakani amesaini ngapi?
 
Wanabodi,
Kama kawa, kila nipatapo fursa
View attachment 2742341
Kufuatia tishio la matamshi yenye viashiria vya uhaini dhidi ya serikali ya JMT kwa baadhi ya watu, na watu hao kushikiliwa na vyombo vya dola, waneibuka watu, mashirika, wanaharakati kupigia kelele kuna kesi ya uhaini, na hadi baadhi ya taasisi za kimataifa kutaka kuingilia kati mambo yetu ya ndani!, hivyo kufuatia mwandishi wa makala hizi kuwa pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, naomba kuitumia makala ya leo, kuanza mfululizo wa makala elimishi kuelimisha umma kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu kwa jicho la mtunga katiba.

Naomba nianze na elimu fupi kuhusu makosa mawili makubwa kuliko makosa yote kwenye katiba yetu. Makosa haya ni kosa la kuua, (murder), na kosa la uhaini, (treason), ambayo yote adhabu yake ni kifo, au "capital punishment", na kwa Tanzania adhabu hii inatekelezwa kwa kunyongwa hadi kufa, kwa nchi yetu tuna gereza moja tuu la kunyongea ni gereza la Isanga, liko Dodoma.

Mtu akihukumiwa kifo, adhabu hii haitekelezwi mpaka kwanza isainiwe na rais wa JMT, hati inayoitwa Hati ya Kifo, (death warrant), na baada ya kusainiwa, mfungwa huyo hupimwa na dakitari bingwa wa hospitali ya serikali kuthibitisha ni mzima na bukheri wa afya, ndipo hunyongwa!. Ikitokea mnyongwa nni mgonjwa wa ugonjwa wowote ikiwemo afya ya akili, adhabu hiyo haitekelezwi hadi mgonjwa atibiwe apone kabisa, apimwe tena, akikutwa ni mzima, ndipo atiwe kitanzi!. Na ikitokea ana maradhi yasiyopona, kama kifafa, au maradhi ya kuambukiza kama ukimwi , kifua kikuu na ukoma, mnyongwa huyo hanyongwi, hutengwa na kulishwa tuu na kulala, yaani kula kulala, mpaka...

Kwa Tanzania, awamu ya kwanza ya utawala wa Baba wa taifa hili wa Mwalimu Nyerere, uliodumu kwa miaka miaka 23, Mwalimu Nyerere asisaini death warrant 2.
Awamu ya pili ya Miaka 10 ya Rais Mwinyi, alisaini hati kadhaa. Awamu zilizofuata za Rais Mkapa, Rais Kikwete, na Rais Magufuli, hakuna death warrant yoyote iliyosainiwa na ndio maana sisi watetezi wa haki za binadamu, tunapendekeza adhabu hii ifutwe.

Sio kila mauaji yakifanyika ni kesi ya murder, kuna mauaji yanaweza kufanyika na ikawa sio kesi ya murder, bali inakuwa ni kesi ya manslaughter, yaani kuua bila kukusaidia. Ili kesi ya mauaji kuwa murder lazima kufanyike mambo mawili, jambo la kwanza ni kitu kinachoitwa "actus reus", kitendo cha mauaji, na "mens rea", nia ovu ya kutenda mauaji, yaani dhamira ya kuua au kukusudia kuua. Vivyo hivyo, uhaini hauwezi kutendeka kwa kauli tuu bila actus reus na mens rea!.

Uhaini ni nini? Uhaini umetajwa kwenye sura ya Saba kifungu cha
39 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, yaani penal code kinasema
Kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais.

Kwa mujibu wa sheria tuliofundishwa darasani, uhaini ni vitendo na sio kauli ni uchochezi!. Kwa vile mpaka sasa hakuna mashitaka yoyote ya uhaini yaliyofunguliwa katika Mahakama yoyote, nawaombeni Watanzania wenzangu tusishabikie uzushi wa uhaini, hili sio jambo la kheri hata kidogo.

Vivyo hivyo kwenye jinai ya uhaini, sio kila matamshi ya uhaini ni uhaini, ili kuwepo kwa jinai ya uhaini, lazima kuwepo kwa zile sifa kuu mbili, actus reus na mens rea ya kupanga kufanya uhaini. Kitendo cha mtu ameghafilika tuu na hoja za Club House, akaanza kuhororoja kutoa matamshi ya kupindua serikali, haimaanishi ni uhaini wa kupindua kweli serikali, lakini matamshi hayo yanaweza kuwa ni matamshi ya uchochezi hivyo kusababisha watu wapange kweli kupindua serikali, lakini matamshi tuu kama matamshi bila ya kuwepo means rea ya kupindua serikali, watu hao watakuwa wamefanya kosa la sedition na sio treason.

Kitendo cha watu haswa wanaharakati kupiga kelele uhaini, kuiongopesha dunia na kufanya nchi yetu kuangaziwa vibaya kimataifa, wakati hadi ninapoandika hapa, hakuna kesi yoyote ya uhaini iliyofunguliwa popote, hivyo huku kushabikia na kushadadia uhaini sio jambo jema, ni kutaka kumchafulia bure huyu Mama wa watu ile sifa yake kuu ya kuliponya taifa!.

Tanzania toka tumepata uhuru, tumewahi kuwa na kesi 5 za uhaini, kesi ya kwanza ni ile ya maasi ya jeshi ya tarehe 18 January 1964, siku 6 baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, jeshi la KAR liliasi, likavunjwa ndio likaundwa JWTZ. Kesi hii iliendeshwa kijeshi, hivyo wala sijui matokeo yake.

Kesi ya kwanza ya uhaini katika Mahakama ya wazi ni kesi ya kina Bibi Titi Mohamed, John Lifa Chipaka, Michael Kamaliza na wengine ya mwaka 1971.

Ikaja kesi ya uhaini inayomhusu aliyeitwa Juma Thomas Zangira.

Mwaka 1982 ndio kulifanyika kesi ya uhaini ya watu 38, wakiongozwa na Pius Lugangira na Hatibu Ghandi ambapo sterling wa kesi hiyo ni komandoo Martin Tamimu aliyeuwawa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

Hapa katikati kukatokea kesi ya mwisho ya uhaini Zanzibar ya kina Seif Sharrif Hamad, Shabani Mloo, Juma Duni Haji, Machano, Hamad Rashid na wengine 18 wa Chama cha Wananchi CUF, kesi hii ikatupiliwa mbali baada ya Mahakama Kuu kutamka kwamba Zanzibar sio nchi, hivyo jinai ya uhaini haiwezi kutendeka!.

Ili kuwasaidia Watanzania kuzijua haki zao, najitoelea kuelimisha umma kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu.

Somo la kwanza ni katiba.
  1. Utangulizi: Hizi ni makala elimishi kutoa elimu ya uraia kwa watu wa kawaida kuijua katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977.
  2. Mtoa Mada ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea kutetea haki katiba na kujitolea kutoa bure elimu ya katiba kuelimisha umma kuhusu katiba kwa jicho, nia na dhamira ya mtunga katiba alidhamiria nini?
  3. Hivyo kupitia safu hii ya kwa maslahi ya Taifa, Ijue Katiba, hizi ni makala elimishi, kuwasaidia Watanzania sio tuu kuijua katiba ya JMT, bali pia kuelewa mtunga katiba alidhamiria nini alipoweka kifungu fulani.
  4. Hii ni makala ya kwanza ya Katiba ni nini?, katiba ni ya nani? na ni ya kazi gani?.
  5. Katiba ni kama Biblia Takatifu au Msahafu yaani Quran Tukufu, imeandikwa law maandishi, hivyo kila anayejua kusoma na kuandika anaweza kuisoma Biblia au Msahafu, lakini kwa bahati mbaya sana, sio kila mtu ana uwezo wa kuisoma na kuielewa, hivyo kuna watu maalum ambao wanavisoma hivi vitabu vya dini na kuwaelimisha wengine, kwenye dini mara nyingi ni viongozi wa dini, lakini kwenye siasa ni viongozi wetu wa siasa.
  6. Kama ilivyotokea kwenye dini, sii wote wanaweza kuisoma Biblia/Msahafu na kuielewa, kuitafsiri, na kuwaelewesha wengine, ni kazi inayofanywa na wachache walijaaliwa uwezo huo, hawa huitwa wahubiri.
  7. Vivyo hivyo, sii wote wana uwezo wa kuisoma katiba, kuielewa, kuitafsiri, na kuwatafsiria wengine, sasa kwa vile mimi mwana JF mwenzunu nimejaaliwa kauwezo fulani kadogo tuu cha kuisoma katiba na kuielewa kwa jicho la mtunga katiba alidhamiria nini, hivyo sasa naitumia dhamira ya mtunga katiba kwa uelimishaji umma kuhusu katiba, na dhamira ya mtunga katiba, hivyo sasa naanzisha darasa rasmi la elimu ya Ijue Katiba ya JMT ya mwaka 1977 kwa jicho la mtunga katiba.
  8. Hivyo kupitia safu hii ya Ijue Katiba, hizi ni makala elimishi, itawasaidia Watanzania kuijua katiba ya JMT na mtunga katiba alidhamiria nini kwa vifungu mbalimbali vya katiba.
  9. Hii ni makala ya kwanza ya Katiba ni nini na katiba ni ya nani?.Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ndio katiba ya JMT.
  10. Katiba ni Nini?. Katiba ni kakitabu kadogo tuu chenye kurasa 43!. Kakitabu haka ndio kila kitu kuihusu Tanzania yetu, hakuna yeyote aliye juu ya Katiba.
  11. Katiba ni ya Kazi Gani. Katiba ndio msingi Mkuu na muongozo wa uendeshaji wa nchi yetu, ambapo sheria zote, taratibu zote na kanuni zote, za kufanya kila jambo, lazima zitokane na katiba.
  12. Misingi ya Katiba- Katiba yetu imeweka misingi mikuu 4 ya katiba ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani.
  13. Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.
  14. Katiba ni ya Nani? Katiba hii imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.
  15. Hivyo kwa mujibu wa katiba hii, kitu muhimu kabisa kwa Taifa la Tanzania, ni watu!, Watanzania, hawa ndio wenye katiba!, katiba ni mali ya Watanzania. Ni watu hawa Watanzania, walioweka misingi mikuu minne ya katiba yetu, uhuru, haki, udugu na amani. Msingi mkuu wa kwanza wa katiba yetu ni uhuru, wa pili ni haki. Hivyo vitu vitu viwili vikuu vya katiba yetu ni uhuru na haki.
  16. Hivyo viongozi wetu tukiisha wachagua kwa mujibu wa katiba katika uchaguzi huru na wa haki, ulioendeshwa na tume huru ya uchaguzi, tunawaapisha kwa katiba waape kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa katiba na kuilinda na kuitetea katiba ya JMT.
  17. It's very unfortunately baadhi ya viongozi wetu hawa nao wako kwenye kundi lile lile la wasoma katiba wasioielewa katiba, wanachaguliwa kwa mujibu wa katiba wasioifahamu!, na waapa kuilinda katiba wasioilewa na mwisho wa siku, badala ya kuilinda katiba, wao ndio kwanza wanakuja kuivunja katiba innocently kwasababu hawajui watendalo kuwa ni kinyumecha katiba!.
  18. Katika uendeshaji wa nchi, tuna mihimili 3 ya Dola inayoendesha nchi yetu, mihimili hii ni Serikali, Bunge na Mahakama. Ili kuendesha nchi kuna watu muhimu sana, ambao wanatajwa na katiba ili kuhakikisha katiba inafuatwa, hawa ni wanasheria.
  19. Tuna wanasheria serikalini, tuna wanasheria Bungeni na tuna wanasheria Mahakamani, ambao ndio walipaswa kuijua katiba!, lakini it's very unfortunately, baadhi ya wanasheria hawa nao pia hawaijui katiba!. Matokeo yake ni Serikali inatunga sheria batili na viongozi wa serikali wanavunja katiba, Bunge linavunja katiba kwa kutunga sheria batili.
  20. Mahakama nayo yenye jukumu la kutafsiri katiba na sheria, ambayo imeshehenezwa wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, baadhi yao ni just too blind to see, katiba inavunjwa, mahakama ipo inaangalia tuu!, kwa kusema "the court is not the custodians of the will of the people!" ... my foot!
Mwisho wa sehemu ya kwanza ya Ijue katiba ya JMT ya mwaka 1977 kwa jicho la mtunga katiba.
Sehemu ya pili ni maana ya Katiba ni sheria Mama, ina maana gani?.

Wasalaam
Paskali
Good! Hii imeenda, kwahiyo genge lile lilitupotosha?
 
Mipango na matendo yote si inaanza Kwa maneno na kauli, Kwa mfano nikisema nitakupiga maana yake kauli si ina kitendo ndani yake?

Kama Uhaini ni matendo na mipango, je uhaini utaonekanaje na utadhibitiwaje kabla ya kufanyika ilhali kitendo halisi ndio kinaonesha ni uhaini?

Je kukiwa na mpango wa kufanya uhaini lakini kitendo kikashindikana ,je na huo utahesabika ni uhaini?

Kama utahesabika ni uhaini mbona umesema uhaini ni matendo na mipango na wakati inajulikana mipango mara nyingine ni kauli au maneno tu?
 
Ikitokea mnyongwa nni mgonjwa wa ugonjwa wowote ikiwemo afya ya akili, adhabu hiyo haitekelezwi hadi mgonjwa atibiwe apone kabisa, apimwe tena, akikutwa ni mzima, ndipo atiwe kitanzi!. Na ikitokea ana maradhi yasiyopona, kama kifafa, au maradhi ya kuambukiza kama ukimwi , kifua kikuu na ukoma, mnyongwa huyo hanyongwi, hutengwa na kulishwa tuu na kulala, yaani kula kulala, mpaka...
Asante Nimepatq kitu kipya hapa
 
Mipango na matendo yote si inaanza Kwa maneno na kauli, Kwa mfano nikisema nitakupiga maana yake kauli si ina kitendo ndani yake?
Mkuu KARLO MWILAPWA , kwanza asante sana kwa maswali yako yako very objective, kwenye makosa, kuna makosa ya civil na kuna makosa ya criminal yaani jinai. Kwa makosa ya civil, lazima actus reus uwepo ila sio lazima mens rea uwepo, lakini kwenye jinai, ili mtu ushitakiwe kwa jinai, lazima actus reus na mens rea zote ziwepo!.

Nikikutamkia kuwa "nitakuua", hilo tamko lina criminal liabilities kama nikikutukana, unaweza kuniripoti police na kunishitaki ila huwezi kunishitaki kwa murder kwasababu ni matamshi tuu ya murder, hakuna actus reus ya murder.

Na nikikushambulia kwa silaha yoyote kwa nia ya kukua utanishitaki kwa kosa la attempted murder, hata ukitaka kujiua ni kosa la attempted murder lakini sio murder. Kutamka kupindua serikali sio treason ni seditious speech tuu!.
Kama Uhaini ni matendo na mipango, je uhaini utaonekanaje na utadhibitiwaje kabla ya kufanyika ilhali kitendo halisi ndio kinaonesha ni uhaini?
Sasa hapa ndipo palitakiwa kufanyika kazi, kiukweli tuna wale "jamaa zetu" wenye kazi zao, ambao kiukweli wa kwetu ni hamna kitu!, zero kabisa!, tena ni ma goigoi ya ajabu!.

Baada ya kauli ile, vijana wa kazi sasa ndio walipaswa kuingia kazini ili kujiridhisha kama ile ni kauli tuu au kuna mipango?, na sio kukurupuka kukamata watu for nothing!.

Mimi nimebatika kutoka familia ya baba na mama ni wale "jamaa" kwanza ile tuu kujua ni nikiwa darasa la 4!, tena kwa kusoma gazetini, gazeti la Mzalendo, unasoma jina la Baba yako ana kesi ya mauaji!, you are shocked!, then ndio unakuja kujua Dingi alikuwa nani!.

Hivyo nimejikuta nimezaliwa na straits za pua za kunusa nusa hiyo, nikiwaangalia hawa jamaa wa sasa ni zero kabisa!, hakuna kitu pale ni completely nill!.

Tungekuwa tuna watu, yule Blaza wangu home boy wangu asingefika pale alipofika!, ile siku naletewa taarifa hii Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli nikawatumia ujumbe kwa codes, walivyo mazuri, they did nothing mpaka Blaza akawa!. Tungekuwa na Idara makini, ilikuwa ni jambo la dakika sifuri kufanya background search kuijua orgin halisi na kuweka pembeni!, lakini hakuna kitu pale!.

Hata shambulio la Lissu, nilifika wakati nikashauri WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? sasa based on kushindwa huku, nimeamua kujitolea kumsaidia huyu Mama asishindwe!, kuna majitu mazima ya hovyo yanampotosha!.
Je kukiwa na mpango wa kufanya uhaini lakini kitendo kikashindikana ,je na huo utahesabika ni uhaini?
Yes utahesabika ni uhaini, kitu cha kwanza ni kwa wazee wakazi kufanya implants ya watu wao, ile kesi ya uhaini ya 1982, baada ya jamaa kuunyaka mpango huo, wakagundua kiongozi wa mpango huo anatumia Taxi, wakamsetia dereva Taxi wao anaitwa Abdallah. Pia ni mtu wa totoz, wakamsetia mrembo mmoja anaitwa Hope, ni binti wa next door kwetu pale Drive in flats. Jamaa ana kata mpunga wa maana, Hope akamtambulisha jamaa kwa wazazi wake, hivyo vikao vikawa vinafanyika kwa jirani yangu next door. Wale wa kule jeshini, kila mmoja akasetiwa mtu, hivyo the group was big kumbe half ni jamaa zetu!. Siku ya utekelezaji ulipangwa ufanyike siku ya Krisimasi tarehe 25 December 1982 Mwalimu Nyerere wangemalizana nae wakati wanatoka kanisani, ana mtindo wa kusalimiana na watu pale nje.

Tarehe 24 usiku kazi ya kuwadakua mmoja mmoja ikaanza, waliwasomba wote wale jamaa na wahusika hivyo kesi ilipoanza walikuwa watu 49, baada ya kuwachuja wakabaki 23, wale jamaa wakawa ndio mashahidi wakuu na ma boss wao Mr. X Mr. Y na Mr. Z wakaja kuwa ma DGIS wa Tiss!.
Sasa hawa wa sasa mtu anahororoja tuu kule Club House majinga haya yana panic!, wanamchafulia sana Mama!.
Kama utahesabika ni uhaini mbona umesema uhaini ni matendo na mipango na wakati inajulikana mipango mara nyingine ni kauli au maneno tu?
Kupanga uhaini ni uhaini lakini kusema uhaini sio uhaini ni uchochezi!. Kupanga kuua ni murder lakini kesi ya kupanga kuua sio murder case ni an attempted murder!.
P
 
Back
Top Bottom