MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 713
- 1,136
Kumekuwa na movement na msukumo kutoka makundi mbali mbali ya kutetea haki za nimadamu, NGO na vyama vya siasa hasahasa vya upinzani kutaka katiba mpya. Ni jambo zuri sana japo kwa upande wa CCM hainekani kuwa ni ajenda wala kioaumbele chao.
Lakini kama tunavyojua nchi hii haijawahi kuwa na upungufu wa mipango mizuri,sera nzuri na sheria nzuri kiasi chake. Tatizo huwa ni implementation yake.
Nani asijejua kuwa Katiba yetu imetoa Uhuru wa kutoa maoni, kujiunga na vyama vya siasa, kujumuika pakoja, kuandamana kama kuna jambo mahsusi. Je yote haya huwa tunayakazania kwenye maisha yetu ya kila siku?
Katiba yetu japo ina mapungufu lakini imeweka bayana majukumu ya mihimili yetu ya dola kwa maana ya wajibu wa kila muhilimi yaani Serikali, Bunge na Mahakama. Lakini bado kama nchi na raia bado tumelala sana na hatujui wapi wajibu wetu kwa vyombo hivyo unaanzia wapi na kuishia wapi.
Wasomi wachache ndio wanaoweza kuona mapungufu ya katiba yetu.
Hivyo Nina wasiwasi sana tunaweza kuwa na katiba mpya nzuri sana lakini watekelezaji wake na utekelezaji wa katiba hiyo usionueshe tofauti ya katiba ya zamani na mpya.
Ni matumaini yangu kuwa kuna haja kwanza ta kuelimisha umma na vyama vyote kuwa na agenda hiyo ili kazi iwe nyepesi sana lakini pia utekelezaji wake uwe mwepesi kwa kila mtekelezaji wa katiba hiyo kwa nafasi zao