Dkt. Anna Henga adai kurejea mchakato wa kutoa elimu kuhusu katiba iliyopo ni kuchelewesha katiba mpya

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini (LHRC), Dk. Anna Henga amesema kitendo cha kufikiria kuanza kutoa elimu kuhusu Katiba (1977) inayotumika kwa sasa ambayo tayari kumekuwepo na michakato tofauti ya kuibadilisha ni kuchelewesha Katiba mpya kupatikana.

Akizungumza kwenye mjadala ulioandaliwa na LHRC kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo The Chanzo kwenye kurasa zao za X (awali ikitambulika kama Twitter) uliobebwa na mada isemayo "Kuanza kwa Mchakato wa Katiba Mpya; Je, wananchi wamejiandaa?", amesema kuwa baadhi ya watu wakihoji kuhusu Katiba mpya kumekuwepo na kauli za baadhi ya wanasiasa kuhoji kama watu wanaijua Katiba inayotumika kwa sasa.

"Wamekuwa wakisema wanasiasa wengi kwamba watu wanataka Katiba mpya iliyopo mnaijua? tumekuwa tukiulizwa hivyo lakini suala sio kuijua, suala ni kujua Nchi yetu inatakiwa kuendeshwa vipi sio lazima nijue kifungu cha kwanza cha kwanza hadi cha mwisho Mimi Anna Henga naweza kujua kwa kuwa ndio kazi nafanya kila siku…, lakini kuna mwingine hana haja ya kujua kila kifungu lakini anajua misingi ya hiyo katiba"

Ameongeza kuwa wakati wa kukusanya maoni kwenye mchakato wa katiba mpya (Katiba ya Warioba) walikuwa wanatoa elimu kwanza kuhusu Katiba ilivyo na changamoto zake harafu ndio wanaomba maoni kwa wananchi

"Tusirudishane nyuma kwamba ndio tuanze kutoa elimu tena ya Katiba iliyopo mimi naona kama ni kucheleweshana"

Aidha aliyewai kuwa Mkurugenzi wa TAMWA, Dk. Ananilea Nkya amesema kuwa mchakato wa kufanikisha Katiba mpya unahitaji siasa za kitofauti ikilinganishwa na siasa za kawaida zilizozoeleka.

"Mchakato wa kupata Katiba mpya unahitaji siasa lakini siasa hiyo ni tofauti na siasa za kawaida, nitofauti na siasa za kugombea uwenyekiti wa Kitongoji, ni tofauti na siasa za kugombea uwenyekiti wa Kijiji, Uenyekiti wa Serikali za Mtaa, Udiwani, nitofauti na siasa za vyama vya siasa kugombea Ubunge ni tofauti na siasa za kugombea Urais”

Ameongeza kuwa mchakato wa Katiba mpya umekuwa ukiodhiwa na wanasiasa jambo ambalo hata Dk. Anna Henga amesema kuwa jamii zote kwa ujumla zinatakiwa kuwa jumuishi katika mchakato mzima kwa kuwa Katiba inagusa watu wote katika jamii.

Itakubukwa Serikali kupitia Rais Samia Suluhu imeonesha dhamira ya kufufua mchakato wa Katiba mpya kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuunda kikosi kazi cha kupokea maoni ambacho kiliwasilisha ripoti, pia Rais Samia pamoja na Chama chake CCM wamelekeza mchakato huo kufanyiwa kazi.

Pia wadau wengine ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekuwa wakisisitiza kukamilishwa kwa mchakato huo kwa haraka, huku wakidai kuwa itakuwa muharobaini kwenye baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikiibuka na kuibua mijadala.

Kwa mara kadhaa baadhi ya viongozi wa juu kwenye Serikali na wakisiasa wamekuwa wakisisitiza utoaji wa elimu kuhusu Katiba inayotumika kwa sasa kabla ya kupata Katiba mpya.
 
Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za Binadamu nchini (LHRC), Dk. Anna Henga amesema kitendo cha kufikiria kuanza kutoa elimu kuhusu Katiba (1977) inayotumika kwa sasa ambayo tayari kumekuwepo na michakato tofauti ya kuibadilisha ni kuchelewesha Katiba mpya kupatikana.

Akizungumza kwenye mjadala ulioandaliwa na LHRC kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo The Chanzo kwenye kurasa zao za X (awali ikitambulika kama Twitter) uliobebwa na mada isemayo "Kuanza kwa Mchakato wa Katiba Mpya; Je, wananchi wamejiandaa?", amesema kuwa baadhi ya watu wakihoji kuhusu Katiba mpya kumekuwepo na kauli za baadhi ya wanasiasa kuhoji kama watu wanaijua Katiba inayotumika kwa sasa.

"Wamekuwa wakisema wanasiasa wengi kwamba watu wanataka Katiba mpya iliyopo mnaijua? tumekuwa tukiulizwa hivyo lakini suala sio kuijua, suala ni kujua Nchi yetu inatakiwa kuendeshwa vipi sio lazima nijue kifungu cha kwanza cha kwanza hadi cha mwisho Mimi Anna Henga naweza kujua kwa kuwa ndio kazi nafanya kila siku…, lakini kuna mwingine hana haja ya kujua kila kifungu lakini anajua misingi ya hiyo katiba"

Ameongeza kuwa wakati wa kukusanya maoni kwenye mchakato wa katiba mpya (Katiba ya Warioba) walikuwa wanatoa elimu kwanza kuhusu Katiba ilivyo na changamoto zake harafu ndio wanaomba maoni kwa wananchi

"Tusirudishane nyuma kwamba ndio tuanze kutoa elimu tena ya Katiba iliyopo mimi naona kama ni kucheleweshana"

Aidha aliyewai kuwa Mkurugenzi wa TAMWA, Dk. Ananilea Nkya amesema kuwa mchakato wa kufanikisha Katiba mpya unahitaji siasa za kitofauti ikilinganishwa na siasa za kawaida zilizozoeleka.

"Mchakato wa kupata Katiba mpya unahitaji siasa lakini siasa hiyo ni tofauti na siasa za kawaida, nitofauti na siasa za kugombea uwenyekiti wa Kitongoji, ni tofauti na siasa za kugombea uwenyekiti wa Kijiji, Uenyekiti wa Serikali za Mtaa, Udiwani, nitofauti na siasa za vyama vya siasa kugombea Ubunge ni tofauti na siasa za kugombea Urais”

Ameongeza kuwa mchakato wa Katiba mpya umekuwa ukiodhiwa na wanasiasa jambo ambalo hata Dk. Anna Henga amesema kuwa jamii zote kwa ujumla zinatakiwa kuwa jumuishi katika mchakato mzima kwa kuwa Katiba inagusa watu wote katika jamii.

Itakubukwa Serikali kupitia Rais Samia Suluhu imeonesha dhamira ya kufufua mchakato wa Katiba mpya kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuunda kikosi kazi cha kupokea maoni ambacho kiliwasilisha ripoti, pia Rais Samia pamoja na Chama chake CCM wamelekeza mchakato huo kufanyiwa kazi.

Pia wadau wengine ikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekuwa wakisisitiza kukamilishwa kwa mchakato huo kwa haraka, huku wakidai kuwa itakuwa muharobaini kwenye baasijui dhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikiibuka na kuibua mijadala.

Kwa mara kadhaa baadhi ya viongozi wa juu kwenye Serikali na wakisiasa wamekuwa wakisisitiza utoaji wa elimu kuhusu Katiba inayotumika kwa sasa kabla ya kupata Katiba mpya.
Sojui kwanini ccm wanaogopa katiba mpya?
 
Back
Top Bottom