Rais Samia anayajua ndio maana anayasema: Bila kubadili mtazamo kwanza kwa kutoa elimu, mabadiliko ya katiba ni kazi bure

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,603
Tukiwa na watu wenye mtazamo huu tulionao wa uzembe, kusukumwa na uvivu basi tusitegemee mabadiliko yoyote chanya kwa kubadili katiba maana watekelezaji wakubwa wa katiba ni watu.

Kwa mfano, mtazamo mkubwa wa wapinzani kwenye mabadiliko ya katiba ni kubadili vifungu vinavyoelezea mamlaka ya Rais na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi kitu ambacho ni tofauti kabisa na mtazamo wa mkulima, mfanyakazi au mwingine yoyote hivyo kwa tofauti ya mitazamo hii mabadiliko ya katiba itakuwa ni bure.

Katika kubadilisha mitazamo kwa kuwajengea uelewa wananchi juu ya katiba, Serikali ya Rais Samia imekuja na mpango kabambe wa kutoa elimu ya katiba. Mpango ambao unakubaliwa na kila mwanamabadiliko na mwanamageuzi.

Kwanza, kutoa elimu ya katiba itasaidia Kujenga mtazamo wa pamoja wa mabadiliko ya katiba. Kila mtu atafahamu umuhimu wa mabadiliko ya katiba kwa upande wake binafsi na sio kwa upande wa wanasiasa. CHADEMA inataka mabadiliko ya katiba wakiamini katiba mpya itawasaidia kushinda wakati mkulima anaamini katiba itamsaidia kwenye kilimo, mitazamo miwili tofauti.

Pili, kutoa elimu kutasaidia kutoandika katiba katika mtazamo wa kundi Fulani wakati katika ni Kwa ajili ya watanzania wote na ushiriki wa Kila mmoja unahitajika. Kwa Sasa mchakato wa katiba mpya umeshikiliwa sana na wanasiasa na kuna hatari kama wanasiasa wakaendelea kuhodhi mchakato huu katiba mpya itatatua matatizo ya kisiasa pekee.

Tatu, Baada ya elimu ya kutosha na Kila mtu kufahamu lengo la katiba Kwa upande wake baada ya hapo tutakuwa tumefanikiwa pakubwa kuwa na mtazamo wa pamoja.
 
Nafikiri mzee warioba alifanya hii kazi na mama alikua kinara kwenye bunge la katiba sasa sijaelewa shida iko wapi.Kama elimu ilishatolewa sanaaa
 
Hii inayotumika ni watanzania wangapi wanaijua??

Katiba ya sasa haijulikani kwa watanzania na bado inatumika Kwa nini Katiba mpya ndiyo mtake kwanza watanzania "wapewe elimu"?
 
Achana na mtazamo wa chama chako, wewe unataka mabadiliko ya katiba kwa lengo Gani?
Kwani hii iliyopo ilikuwa Kwa lengo gani??

Mnang'ang'ania katiba iliyotungwa Kwa mitizamo ya kijamaa nyakati hizi ambapo hata viongozi Wa chama chenu ni mabepari??

Katiba yenye chembechembe za kifalme inatufanya tulazimishwe kumuambudu Rais kwa lazima inatufalia nini??
 
Hakuna siku hata 20% ya wananchi watakuja kuijua Katiba.

Hizo nadharia za kusema eti watu wafundishwe kwanza ndiyo katiba mpya ipatikane ni utapeli Wa wasomi uchwara.
Mkapa alipokuja na KKK yaani kusoma, kuandika na kuhesabu mkasema haiwezekani lakini kulingana na takwimu kiwango cha kusoma, kuandika na kuhesabu ni 90%
 
Back
Top Bottom