Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio kila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Wanabodi,
  1. Utangulizi: Hizi ni makala elimishi kutoa elimu ya uraia kwa watu wa kawaida kuijua katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977.
  2. Mtoa Mada ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea kutetea haki katiba na kujitolea kutoa bure elimu ya katiba kuelimisha umma kuhusu katiba kwa jicho, nia na dhamira ya mtunga katiba alidhamiria nini?
  3. Hivyo kupitia safu hii ya Ijue Katiba, hizi ni makala elimishi, itawasaidia Watanzania sio tuu kuijua katiba ya JMT, bali pia kuelewa mtunga katiba alidhamiria nini alipoweka kifungu fulani.
  4. Hii ni makala ya kwanza ya Katiba ni nini?, katiba ni ya nani? na ya kazi na ni ya kazi gani?.
  5. Katiba ni kama Biblia Takatifu au Msahafu yaani Quran Tukufu, imeandikwa law maandishi, hivyo kila anayejua kusoma na kuandika anaweza kuisoma Biblia au Msahafu, lakini kwa bahati mbaya sana, sio kila mtu ana uwezo wa kuisoma na kuielewa, hivyo kuna watu maalum ambao wanavisoma hivi vitabu vya dini na kuwaelimisha wengine, kwenye dini mara nyingi ni viongozi wa dini, lakini kwenye siasa ni viongozi wetu wa siasa.
  6. Kama ilivyotokea kwenye dini, sii wote wanaweza kuisoma Biblia/Msahafu na kuielewa, kuitafsiri, na kuwaelewesha wengine, ni kazi inayofanywa na wachache walijaaliwa uwezo huo, hawa huitwa wahubiri.
  7. Vivyo hivyo, sii wote wana uwezo wa kuisoma katiba, kuielewa, kuitafsiri, na kuwatafsiria wengine, sasa kwa vile mimi mwana JF mwenzunu nimejaaliwa kauwezo fulani kadogo tuu cha kuisoma katiba na kuielewa kwa jicho la mtunga katiba alidhamiria nini, hivyo sasa naitumia dhamira ya mtunga katiba kwa uelimishaji umma kuhusu katiba, na dhamira ya mtunga katiba, hivyo sasa naanzisha darasa rasmi la elimu ya Ijue Katiba ya JMT ya mwaka 1977 kwa jicho la mtunga katiba.
  8. Hivyo kupitia safu hii ya Ijue Katiba, hizi ni makala elimishi, itawasaidia Watanzania kuijua katiba ya JMT na mtunga katiba alidhamiria nini kwa vifungu mbalimbali vya katiba.
  9. Hii ni makala ya kwanza ya Katiba ni nini na katiba ni ya nani?.Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ndio katiba ya JMT.
  10. Katiba ni Nini?. Katiba ni kakitabu kadogo tuu chenye kurasa 43!. Kakitabu haka ndio kila kitu kuihusu Tanzania yetu, hakuna yeyote aliye juu ya Katiba.
  11. Katiba ni ya Kazi Gani. Katiba ndio msingi Mkuu na muongozo wa uendeshaji wa nchi yetu, ambapo sheria zote, taratibu zote na kanuni zote, za kufanya kila jambo, lazima zitokane na katiba.
  12. Misingi ya Katiba- Katiba yetu imeweka misingi mikuu 4 ya katiba ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani.
  13. Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.
  14. Katiba ni ya Nani? Katiba hii imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.
  15. Hivyo kwa mujibu wa katiba hii, kitu muhimu kabisa kwa Taifa la Tanzania, ni watu!, Watanzania, hawa ndio wenye katiba!, katiba ni mali ya Watanzania. Ni watu hawa Watanzania, walioweka misingi mikuu minne ya katiba yetu, uhuru, haki, udugu na amani. Msingi mkuu wa kwanza wa katiba yetu ni uhuru, wa pili ni haki. Hivyo vitu vitu viwili vikuu vya katiba yetu ni uhuru na haki.
  16. Hivyo viongozi wetu tukiisha wachagua kwa mujibu wa katiba katika uchaguzi huru na wa haki, ulioendeshwa na tume huru ya uchaguzi, tunawaapisha kwa katiba waape kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa katiba na kuilinda na kuitetea katiba ya JMT.
  17. It's very unfortunately baadhi ya viongozi wetu hawa nao wako kwenye kundi lile lile la wasoma katiba wasioielewa katiba, wanachaguliwa kwa mujibu wa katiba wasioifahamu!, na waapa kuilinda katiba wasioilewa na mwisho wa siku, badala ya kuilinda katiba, wao ndio kwanza wanakuja kuivunja katiba innocently kwasababu hawajui watendalo kuwa ni kinyumecha katiba!.
  18. Katika uendeshaji wa nchi, tuna mihimili 3 ya Dola inayoendesha nchi yetu, mihimili hii ni Serikali, Bunge na Mahakama. Ili kuendesha nchi kuna watu muhimu sana, ambao wanatajwa na katiba ili kuhakikisha katiba inafuatwa, hawa ni wanasheria.
  19. Tuna wanasheria serikalini, tuna wanasheria Bungeni na tuna wanasheria Mahakamani, ambao ndio walipaswa kuijua katiba!, lakini it's very unfortunately, baadhi ya wanasheria hawa nao pia hawaijui katiba!. Matokeo yake ni Serikali inatunga sheria batili na viongozi wa serikali wanavunja katiba, Bunge linavunja katiba kwa kutunga sheria batili.
  20. Mahakama nayo yenye jukumu la kutafsiri katiba na sheria, ambayo imeshehenezwa wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, baadhi yao ni just too blind to see, katiba inavunjwa, mahakama ipo inaangalia tuu!, kwa kusema "the court is not the custodians of the will of the people!" ... my foot!
Mwisho wa sehemu ya kwanza ya Ijue katiba ya JMT ya mwaka 1977 kwa jicho la mtunga katiba.
Sehemu ya pili ni maana ya Katiba ni sheria Mama, ina maana gani?. Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama?

Wasalaam
Paskali
 
Inabidi TLS wawe wanatoa points kwa mawakili wanaotoa mada magazetini na mitandaoni/tv/redio.

Wakili atoe proof tu, anapata CLE points.
 
Ahsante sana Pasco kwa makala hii ya maana sana juu ya elimu ya Katiba. Hakika umenena yaliyo kweli. Hata pale ulipoingia ndani zaidi, umetaja utamu wa pera na embe dodo, mwisho umeitaja na asali na utamu wake ndio funga kazi. Watawala wengi husigina Katiba kwa utamu wa asali, wanasheria nguli hupindisha sheria mama kwa tafsiri zao mbovu kwa utamu wa asali. Tume ya uchaguzi huwekwa wanasheria na wao hulamba asali.

Wakuu wa majeshi yetu yote husigina Katiba kwa utamu wa asali. Je, Tulia naye kwa utamu wa asali yumo? Mdugayi je? Pia wengi tu unaowafahamu walipisha Katiba. Ubovu mkubwa huja pale wazee wa "deep state" wanapotuletea raisi asiyeielewa Katiba kama alivyo Mganguzi. Mganguzi, hakika ana reflect jina lake, kwani waganguzi wengi huwezi watenganisha na ramli chonganishi. Ramli chonganishi huwezi itenganisha na shetwani.

Shetwani hupenda mwanadamu awe ktk taabu, maonezi nk. Ndivyo walivyo watawala kama walikuwa akina Mdugayi, Tulia, na wengine wengi ktk taasisi mbali mbali. Je, tutakapoiandika Katiba mpya, kwa nini tusiweke kifungu cha kila aombaye uongozi kwa wananchi ni lazima aijue Katiba na vifungu vyake vyote, hii ni ktk kujenga taasisi imara. Iwe lazima kama tunazijua amri 10 za Mungu.

Kwako, wewe Pasco, umeikwepaje asali hadi sasa umemkimbia shetwani na kazi zake zote? Umejaribu mara kadhaa, nilikuona, lakini mkono wa Mungu ukakuvuta. Hakika ukiendelea hivi utaponywa na kuiona pepo. Sasa, sasa, nakuomba na nakusihi sana endeleza huu mpango wako wa kutufumbua macho sisi Watanzania juu ya elimu ya kuijua Katiba na faida zake kwa maendeleo ya nchi. Pengine tungekuwa mbali kama sii watu kama alivyo Mganguzi. Kwake yote sawa, mvua ama jusi, baridi ama joto!

Endapo hata kama utaenda mbali zaidi, tutengenezee vipeperushi nasi hatutasita kukuchangia hela kidogo ya kunulia wino na kidau chake ili uandike vizuri, hata ikiwezekana tutakuwa na blotting paper ili wino usichuruzike. Wale wazee wa zamani tuliotumia fountain peni, vidau na blotting paper mpo? Mpeni heko Pasco.

Leo yatosha, M/Mungu na awajalie mema J2 njema!
 
  1. Katiba ni kama Biblia Takatifu au Msahafu yaani Quran Tukufu, imeandikwa law maandishi, hivyo kila anayejua kusoma na kuandika anaweza kuisoma Biblia au Msahafu, lakini kwa bahati mbaya sana, sio kila mtu ana uwezo wa kuisoma na kuielewa, hivyo kuna watu maalum ambao wanavisoma hivi vitabu vya dini na kuwaelimisha wengine, kwenye dini mara nyingi ni viongozi wa dini, lakini kwenye siasa ni viongozi wetu wa siasa.
  2. Kama ilivyotokea kwenye dini, sii wote wanaweza kuisoma Biblia/Msahafu na kuielewa, kuitafsiri, na kuwaelewesha wengine, ni kazi inayofanywa na wachache walijaaliwa uwezo huo, hawa huitwa wahubiri.
Asante kwa elimu hii ndugu Pascal Mayalla . Na kama hivi ndivyo kwann basi ninyi wanasheria kupitia TLS msitafute muda mkaandaa "mapendekezo mahususi"ya kukosoa mpango (plan) wa kutoa elimu kwa miaka 3?
 
Wanabodi,
  1. Utangulizi: Hizi ni makala elimishi kutoa elimu ya uraia kwa watu wa kawaida kuijua katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977
Paskali
Paschal Mayalla, niwie radhi kwasababu nilijibu maoni ya Lucas aliyokutag nikidhani ni maneno yako. Tena nilitaka kushangaa, mtu kama wewe kuwaza katika ule muelekeo ni ajabu.
Mkuu mbussi , usijali nimekuelewa na kukupiga darasa la mchakato wa utengenezaji katiba bora. Mchakato huu wa Katiba ni umasikini wetu. Tujikubali, tuukubali, tuupigie kura ya ndio

Pia humu JF, najihesabu ni mmoja wa self made teachers wa katiba
P
 
Wanabodi,
  1. Utangulizi: Hizi ni makala elimishi kutoa elimu ya uraia kwa watu wa kawaida kuijua katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977.
  2. Mtoa Mada ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea kutetea haki katiba na kujitolea kutoa bure elimu ya katiba kuelimisha umma kuhusu katiba kwa jicho, nia na dhamira ya mtunga katiba alidhamiria nini?
  3. Hivyo kupitia safu hii ya Ijue Katiba, hizi ni makala elimishi, itawasaidia Watanzania sio tuu kuijua katiba ya JMT, bali pia kuelewa mtunga katiba alidhamiria nini alipoweka kifungu fulani.
  4. Hii ni makala ya kwanza ya Katiba ni nini?, katiba ni ya nani? na ya kazi na ni ya kazi gani?.
  5. Katiba ni kama Biblia Takatifu au Msahafu yaani Quran Tukufu, imeandikwa law maandishi, hivyo kila anayejua kusoma na kuandika anaweza kuisoma Biblia au Msahafu, lakini kwa bahati mbaya sana, sio kila mtu ana uwezo wa kuisoma na kuielewa, hivyo kuna watu maalum ambao wanavisoma hivi vitabu vya dini na kuwaelimisha wengine, kwenye dini mara nyingi ni viongozi wa dini, lakini kwenye siasa ni viongozi wetu wa siasa.
  6. Kama ilivyotokea kwenye dini, sii wote wanaweza kuisoma Biblia/Msahafu na kuielewa, kuitafsiri, na kuwaelewesha wengine, ni kazi inayofanywa na wachache walijaaliwa uwezo huo, hawa huitwa wahubiri.
  7. Vivyo hivyo, sii wote wana uwezo wa kuisoma katiba, kuielewa, kuitafsiri, na kuwatafsiria wengine, sasa kwa vile mimi mwana JF mwenzunu nimejaaliwa kauwezo fulani kadogo tuu cha kuisoma katiba na kuielewa kwa jicho la mtunga katiba alidhamiria nini, hivyo sasa naitumia dhamira ya mtunga katiba kwa uelimishaji umma kuhusu katiba, na dhamira ya mtunga katiba, hivyo sasa naanzisha darasa rasmi la elimu ya Ijue Katiba ya JMT ya mwaka 1977 kwa jicho la mtunga katiba.
  8. Hivyo kupitia safu hii ya Ijue Katiba, hizi ni makala elimishi, itawasaidia Watanzania kuijua katiba ya JMT na mtunga katiba alidhamiria nini kwa vifungu mbalimbali vya katiba.
  9. Hii ni makala ya kwanza ya Katiba ni nini na katiba ni ya nani?.Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ndio katiba ya JMT.
  10. Katiba ni Nini?. Katiba ni kakitabu kadogo tuu chenye kurasa 43!. Kakitabu haka ndio kila kitu kuihusu Tanzania yetu, hakuna yeyote aliye juu ya Katiba.
  11. Katiba ni ya Kazi Gani. Katiba ndio msingi Mkuu na muongozo wa uendeshaji wa nchi yetu, ambapo sheria zote, taratibu zote na kanuni zote, za kufanya kila jambo, lazima zitokane na katiba.
  12. Misingi ya Katiba- Katiba yetu imeweka misingi mikuu 4 ya katiba ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani.
  13. Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu.
  14. Katiba ni ya Nani? Katiba hii imetungwa na Bunge maalum kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia.
  15. Hivyo kwa mujibu wa katiba hii, kitu muhimu kabisa kwa Taifa la Tanzania, ni watu!, Watanzania, hawa ndio wenye katiba!, katiba ni mali ya Watanzania. Ni watu hawa Watanzania, walioweka misingi mikuu minne ya katiba yetu, uhuru, haki, udugu na amani. Msingi mkuu wa kwanza wa katiba yetu ni uhuru, wa pili ni haki. Hivyo vitu vitu viwili vikuu vya katiba yetu ni uhuru na haki.
  16. Hivyo viongozi wetu tukiisha wachagua kwa mujibu wa katiba katika uchaguzi huru na wa haki, ulioendeshwa na tume huru ya uchaguzi, tunawaapisha kwa katiba waape kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa katiba na kuilinda na kuitetea katiba ya JMT.
  17. It's very unfortunately baadhi ya viongozi wetu hawa nao wako kwenye kundi lile lile la wasoma katiba wasioielewa katiba, wanachaguliwa kwa mujibu wa katiba wasioifahamu!, na waapa kuilinda katiba wasioilewa na mwisho wa siku, badala ya kuilinda katiba, wao ndio kwanza wanakuja kuivunja katiba innocently kwasababu hawajui watendalo kuwa ni kinyumecha katiba!.
  18. Katika uendeshaji wa nchi, tuna mihimili 3 ya Dola inayoendesha nchi yetu, mihimili hii ni Serikali, Bunge na Mahakama. Ili kuendesha nchi kuna watu muhimu sana, ambao wanatajwa na katiba ili kuhakikisha katiba inafuatwa, hawa ni wanasheria.
  19. Tuna wanasheria serikalini, tuna wanasheria Bungeni na tuna wanasheria Mahakamani, ambao ndio walipaswa kuijua katiba!, lakini it's very unfortunately, baadhi ya wanasheria hawa nao pia hawaijui katiba!. Matokeo yake ni Serikali inatunga sheria batili na viongozi wa serikali wanavunja katiba, Bunge linavunja katiba kwa kutunga sheria batili.
  20. Mahakama nayo yenye jukumu la kutafsiri katiba na sheria, ambayo imeshehenezwa wanasheria manguli, wabobezi na wabobevu, baadhi yao ni just too blind to see, katiba inavunjwa, mahakama ipo inaangalia tuu!, kwa kusema "the court is not the custodians of the will of the people!" ... my foot!
Mwisho wa sehemu ya kwanza ya Ijue katiba ya JMT ya mwaka 1977 kwa jicho la mtunga katiba.
Sehemu ya pili ni maana ya Katiba ni sheria Mama, ina maana gani?.

Wasalaam
Paskali
Asante mkuu Paskali kwa kujitolea kutoa elimu hii kwa raia bila malipo. Nadhani tume ya Warioba wataona juhudi zako na kukuunga mkono. Tupo pamoja.
 
Back
Top Bottom