Kati ya Samaki hawa wapi watamu zaidi?

Kati ya Samaki hawa wapi watamu zaidi?

Samaki wa maji chumvi watamu zaidi, unaweza kushindwa kuwajua majina
1. Tasi (watamu)
2. Kitoga (watamu)
3. Kibua (watamu)
4. Ngisi ( watamu)
5. Pweza watamu hasa upate na ugali
6. Jodari
7. Chuchunge
8.
Aah acha tuu mkuu
 
Hahaah mimi nimekula wote mkuu na sahii niko pwani jirani yako hapa, changu, mkundaji, jodari n.k na wa bara nimekula wa mitoni nimekula, nyie watu wa pwani tatizo mnataka samaki wote duniani wawe wa kwenu, kwahyo sisi kule ziwani tunavua mijusi au?.
Kiufupi labda ladha ila naona samaki ya maji baridi wamepooza kweli ...Yaani si unajua chakula lilichopooza sio kizuri.

Hao dagaa , wa mwanza na kigoma nimewapenda sana ..Ni wazuri sana .
 
Siyo unachokipenda wewe ndo kila mtu anapenda
Samaki wa bara wamepooza ,huo ni ukweli mchungu ... Baharini samaki wake sio unique ila wa bara ni wachache ndio maana wanakuwa na soko kweli huko kwenu .

Nilikuwa nanunua sato wale mmoja 10k ,sikuwahi kuhisi utamu na wenyeji walikuwa wanatuwekea Asubuhi tukinywa chai .

Bara kwenye mifugo sio siri mko vizuri ,naona mifugo yenu ina nyama nzuri hta supu sio huku kwetu.
 
Wasalamu.Tumsifu Yesu Kristo.Wapo samaki wa maji moto yani Bahari na hawa maji baridi yani ziwani.
Ila kwa leo naomba kujua Kati ya Sangara,Sato na vibua na kambale ni kundi gani ni watamu zaidi?
Watamu ni sato, then kibua kisha Sangara lkn kibua hapana

Ila kwa mafuta Sangara ni finest katika hao
 
Aisee...huyu mimi sili ukimleta hivi labda uwe umempika tayari. Kama nyoka!
Anakua mzuri pia akikaushwa juani na kuwa namna hii👇👇👇
f7ec47b060e7ff769d0f46fb642392d5~2.jpg
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣

We kwa mfano angalia umbile la huyo mdudu,eti wanamla ,huyo ana tofauti gani na mnyoo,kama sio uroho ni nini?

Eti wenye wanajifari wanawaita seafood

Mamamaaaaaaae
Seafood!
Kwani tupo japani sie?
Wanashangaza sana mkuu.
Kuna jamaa angu wa chuo kipindi hicho toka Mtwara 😂😂 anakwambia vyote vya baharini kwao kiimani ni visafi.
Mkuu🙌🙌😆
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣

We kwa mfano angalia umbile la huyo mdudu,eti wanamla ,huyo ana tofauti gani na mnyoo,kama sio uroho ni nini?

Eti wenye wanajifari wanawaita seafood

Mamamaaaaaaae
Mkuu kwani uzuri wa chakula ni muonekano wake kabla hakijaàndaliwa?

Hayo ni mattizo yako binafsi kwa kukariri kwamba kiumbe fulani ili kiliwe basi kiwe na umbo fulani na kikiwa tofauti na ulivyo kariri basi hakifai na ni uroho kukila
 
Mkuu kwani uzuri wa chakula ni muonekano wake kabla hakijaàndaliwa?

Hayo ni mattizo yako binafsi kwa kukariri kwamba kiumbe fulani ili kiliwe basi kiwe na umbo fulani na kikiwa tofauti na ulivyo kariri basi hakifai na ni uroho kukila
Eti eeeeh,huyu nilishajaribu kumuonja nikataka kukata roho
 
Back
Top Bottom