Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Hii video itawatesa sana naona mnajaribu kufanya cover up lakini ukweli huu wa vitendo vya utesaji ambao umekua ukifanywa na kitengo cha ulinzi na usalama ndani ya chadema utaishi muda mrefu sana.
Hizi mbinu za kitoto hazitaisaidia CCM mwisho wa siku zitakuja kuwaumbua viongozi wenu waliopanga na kuedit fake clip. Ze utamu walifikiri kama mnavyofiri nyie walidhani wamejificha lakini technologia ile ile waliyotumia ilikuja kuwaumbua so count your days.
 
Kama ndivyo basi wangefanya hivyo kwa viongozi maarufu wa CHADEMA kama Mbowe na Slaa na siyo huyu Lwakatare ambaye siyo maarufu kihivyo. Wacheni kukimbia kivuli chenu, unyama wa CDM sasa umewekwa hadharani na kila Mtanzania mwenye nia njema na afahamu hivyo. Tunaishi na wanyama
Labda hufwatilii matukio, ulishasikia ile ishu ya viongoz wa chadema kutuma sms za kutishia kuua kwa kutumia simu zao?? Ule mtambo uliingizwa nchin kwa lengo za kuchafua watu kwa propaganda za aina hii hii. Umesikia kesi ikiendelea hadi leo??? Tuizoee nchi yetu na vibweka vyake jaman.
 
Tatizo nyie mmeolewa na chadema hata ikifanya uozo mnautetea.

Siwezi kukulaumu maana akili yako ni ndogo kiasi kwamba huwezi ku-reason na pia kutambua video feki na halisia. Ungeweza kuingalia sekunde baada ya nyingine ungegundua ni video ya kutengeneza. Sisi tunaongea kitaalamu na sio kubwabwaja tu.

Hawa watu walikuwa wanaji-record na pia walikuwa wanaambizana kuwa "hapo tutairekebisha ikae sawa, haya endelea". Pia mwanza kabisa unaona wanahangaika ku-set microphone na mzungumzaji aliyetengenezwa yaani mfano wa Lwakatare anasubiri na huku akijua ana-rekodiwa. Hivi ni mtu mjinga kiasi gani anaweza kupanga mbinu ya hatari hivo huku watu wengine wakawa wanamsikiliza na wengine kuendelea na shughuli zao na wengine kusema "mambo vipi za masiku, tupo bwana" na wengine wanahudumia yaani wahudumu.

Kwa kuwa akili yako ni finyu endelea kupiga ramuli ya mchana kweupe. Polisi wampeleke mahakamani waone watakavyoumbuka.
 
nenda kasome nukuu ya maneno ya dr. Slaa gazeti la tz daima amenena km unavyonena......yaani km hio video ni ya kupika basi ccm wamekwisaha kabisa, na najua cdm lazima watafanya juu chini kucheza hii karata vizuri ili hata baadae ccm wakija na upuuzi mwingine watanzania wawadharau.........wapi ule mtambo wa kutuma sm za vitisho?

Naomba hii video iwe ya kweli.....vinginevyo hili ni kaburi la ccm mchana kweupeeeeee!!!!!!!
tupo pamoja mkuu sio kwa sababu ya chadema ni kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu,haya mambo kwa akili nyepesi ni mepesi tu lakini yanagusa usalama mzima wa nchi.hakika tutaiangamiza nchi hii.
 
wanajamv,
itakumbukwa kuwa hawa jamaa walishakuja na mtambo wa kugushi sms akina mwigulu hawa lakini kamanda mabere marando aliwaumbua wazi kwenye vyombo vya habari na hawajakanukanusha mpaka kesho kwa hii si ajabu kwa kwa wenye akili wanajua viva cdm
 
Kwa mtu mwenye akili timamu akiiona ile Clip mbona unajua tuu kuwa ni fake.
Huwezi ukawa unapanga mikakati sensitive kama ile mala secretary kapita mara huyu kapita kuchukua file mara kuna watu wanaongea pembeni.
Alafu msome usoni huwezi kuwa na muonekano kama ule kama umedhamilia kufanya jambo la kiharifu kama lile.
Magamba try to understand kuwa not all the Tanzanias are fool and you can fool some not all.
 
Pole sana, kama unazani mimi
ni kama wewe, basi nikupe tu pole nyingine ya ziada! Naelemea kwetu
wapi?! si CCM, CUF wala CHADEMA wana mvuto kwangu!

Kweli mkuu wewe ni CHAUMA
 
Kama ndivyo basi wangefanya hivyo kwa viongozi maarufu wa CHADEMA kama Mbowe na Slaa na siyo huyu Lwakatare ambaye siyo maarufu kihivyo. Wacheni kukimbia kivuli chenu, unyama wa CDM sasa umewekwa hadharani na kila Mtanzania mwenye nia njema na afahamu hivyo. Tunaishi na wanyama

Watanzania wote siyo punguani huwezi kuwadanganya kirahisi hivyo. Ikiwa wewe unafuata upepo kila uelekeapo usitulazimishe na sisi. Kama wewe umehongwa uwe mjinga au ndiye uliyepanga mipango kivyako.
 
huh huhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! "RWAKATALE" anawanyima usingizi mkoani kagera na sasa ndo mbinu hii imeletwa ili kumpunguza kasi maana "M4C" inayoendeshwa kwa kasi mkoani humo chini ya uenyekiti wake wa mkoa ni dhahiri CCM haiwezi kubaki salama sku za usoni:::::::::::::::::::::::.
 
labda hufwatilii matukio, ulishasikia ile ishu ya viongoz wa chadema kutuma sms za kutishia kuua kwa kutumia simu zao?? Ule mtambo uliingizwa nchin kwa lengo za kuchafua watu kwa propaganda za aina hii hii. Umesikia kesi ikiendelea hadi leo??? Tuizoee nchi yetu na vibweka vyake jaman.
kwa akili yake haoni uzito wa lwakatare pale cdm,yeye hajui kwamba ukiugusa ulinzi ndio umekigusa chama kabisa kwamba akituhumiwa yule ndio cdm inavyoendeshwa.ila tunatofautiana kuelewa majambo tofauti tofauti
 
nenda kasome nukuu ya maneno ya dr. Slaa gazeti la tz daima amenena km unavyonena......yaani km hio video ni ya kupika basi ccm wamekwisaha kabisa, na najua cdm lazima watafanya juu chini kucheza hii karata vizuri ili hata baadae ccm wakija na upuuzi mwingine watanzania wawadharau.........wapi ule mtambo wa kutuma sm za vitisho?

Naomba hii video iwe ya kweli.....vinginevyo hili ni kaburi la ccm mchana kweupeeeeee!!!!!!!
yasijetokea ya mfamaji kukamata maji.
 
ha ha ha ha SAMAKI MTUNGONI.......................
 
Uko sahihi mkuu wangu. watu bado wako nyuma ya dunia hii sana pamoja na kumiliki ma laptop kwa sana. picha au video hiyo ni fake kwa asilimia zote may be wanaochangia kwa kushadidia ni wale wale waliotengeneza na wanafanya hivyo ili kuonyesha watu wanaisupport.
 
All in all..., hii nchi tumefika ambapo sipo.., watu waanze kutupwa ndani na tuache utani kwenye mambo serious.., uchunguzi ufanyike, ikigundulika kwamba watu walipanga mauaji, waliua au walisingizia wenzao (kugushi) basi wawekwe ndani huu sasa ushakuwa zaidi ya upuuzi (siasa mpaka kwenye maisha ya watu)

Ile ya Shehe Ilunga Polisi haikuwastua kabisa maana Uislam kwao sio tatizo kama Chadema ila mimi naogopa sana hapa tulipofikishwa watu tumeanza kuchinjana kwasababu ya utawala kutaka kutumia mbinu zozote wawezazo kubaki madarakani, wanatumia njia ya zamani ya devide and rule, nani alitegemea kungetokea chuki za namna hii kati ya Waislam na Wakristo? nani anajua kwamba CCM kwasasa inataka ihamishe mtazamo wa watu kuhusiana na mauaji ya Mwangosi na kuteswa kwa ulimboka waigeukie Chadema ilihali suala la Mwangosi ukweli woote usio na shaka uliandikwa na Mwanahalisi kwa kushirikiana na makampuni ya simu ambayo hayakufurahishwa na kitendo kilichofanywa na Ikulu
 
Kufuatia suala la Lwakatare kushika kasi humu jamvini, zimetokea hisia na mawazo tofauti sana baina ya wachangiaji mbalimbali juu ya mada hii ya kurecordiwa Lwakatare kupanga kumdhuru mwandishi. Wengi tulihoji sana uwezekano wa hii ishu kama ni halisi/si halisi. Kutokana na kuwa gizani kitechnologia, wengi hadi ninavyoongea hivi bado huwezi kuwabadilisha mawazo kuwa technolojia inaweza ikahusika katika kufake ile clip. Na kutokana na suala hili kugubikwa na propaganda za kisiasa, watu wamesahau hata technologia rahiti tu ya kuifanya midomo ya Cartoon icheze kulingana na maneno yanayotamkwa na cartoon/robot.

Kuweka kumbukumbu vizuri tarehe za mwanzon kabisa za mwaka huu mpya Mwigulu Nchemba alitueleza kuwa alikuwa na mkanda unaoonyesha viongoz (wengi) wa chadema kupanga mauaji. Mkanda umetoka tumeona kiongozi mmoja tu ndo anayepanga mauaji, kupungua kwa washiriki kutoka kwa viongoz hadi kiongozi, inahusishwa na ugumu uliopo wa kuinvolve watu wengi kwenye kufake/kulisha maneno watu wengi kwenye clip moja.

Aidha, baada ya tukio la utekwaji wa kibanda, wameibuka Nape na Ridhiwani hadharani na kuongea wakiwa na confinence ya 100% kuwa ''hawa wenzetu wa upinzani''/na ''safari hii pia mseme kuwa Ikulu/Rama/Magogoni ndio wanaohusika, kazi iliyopaswa kufanywa na vyombo vya dola. Siku chache baadaye Single ya Lwakatale ikatambulishwa rasmi kupitia Youtube na immediately ikatua jamvini na hata Polisi kuipata habari hii via Jamvini/Youtube na sio kwa Mwigulu. Sasa ukiconnect dots.......unaruhusiwa kabisa kufikiri kuwa tayari wenzetu wa upande wa pili walisha preview hii clip waliyoshiriki kuiandaa na ndo mana walikuwa na uhakika kuwa kwa level yetu ta technology, ni rahisi sana kushawishika kwa hii clip kuwa ni halisi.

Tulishasikia pia Wassira akitamka kuwa CDM lazima ife 2013, wengi hatukuelewa na hadi sasa hatujaelewa alikuwa anamaana gani kutamka maneno kama yale mtu wa makamo yulo. Sasa kauli za hivi za kumtamkia kifo mwenzio zinasignal kuwepo kwa mkakati wa maksudi wa kumuua mwenzio??Aidha, CCM katika vikao vyao vya CC/NEC, ccm walijadili kwa kina namna ya kudeal/kuisambaratisha CDM badala ya namna ya kutumikia umma wa watanzania waliowaweka madarakani. Hapa pia panazaa jambo.

Baada ya utanguliz huu naomba niimwage kwenu faked clip ya Barack Obama ili at least tujue tu kuwa suala la kulishwa maneno linawezekana. BOFYA A Bad Lip Reading of Barack Obama's Inauguration (Legendado PT-BR) - YouTube. Aidha, clip hii isikuzuie kuendelea kuamini unachokiamini, mimi nimeonelea tu niwafahamishe wale wote wenzangu ambao asubuh ya leo tulihisi sio kitu kinachowezekana hapa duniani.

Asante Mkuu kwa kuwang'amua wenye akili nyepesi (wasiotaka kufikiri) kwa clip hii ya Obama. Nadhani sasa watatuelewa tunapowaambia kuwa video ya Lwakatare ni feki. Ukilinganisha ya Obama na ya kwao utaona utofauti wa quality, hata hivyo ya Obama nayo ina mapungufu lukuki ukianzia na sauti sio ya Obama japo waliweza sana hucheza na Mdomo wake.

Ridhiwani na Nape wanafanya mipango ya kitoto na kwamba wanataka kutuvulugia amani ya nchi yetu kwa kuchonganisha chadema na wananchi.

CCM na serikali yake wanatapatapa na kuhangaika kadri siku zinavyoenda na 2015 watakuwa wamemaliza uongo wote. Na hizi ni dalili za kushindwa
 
Back
Top Bottom