Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kama ni kweli then let the guy and his part face the consequences! Na Kama ni cloning ya video basi hii ni hatari sana kwa nchi yetu maana we are almost in a MAFIA state ambapo mbinu chafu kama hii hutumika ku- discredit na ku-hijack individuals, groups, and so forth. Hata hivyo kuna maswali yanayobidi kuulizwa na mojawapo: why on YouTube and not police source kama kweli it was intentionally taken! Hii mie inanipa feelings kwamba it looks more as a propaganda tools purposely prepared for a special purpose than a real issue ya utekaji, utesaji na hata mauaji. Ni vizuri na naamini polisi wetu wataliangalia kwa uhalisia wake ili kulipa sura yake halisi na kusaidia kutoa ufumbuzi wa uharifu bila kuingiliwa na michezo ya kisiasa.
 
Asubuhi hii nimemsikia Kova akisema Lwakatare amekamatwa kama 'LWAKATARE' au mtuhumiwa mwingine.Anasema wananchi watulie kwa kuwa upelelezi unaendelea na taarifa itatolewa kwa kuwa amekamtwa kwa nia njema na wala sio chuki yeyote kama watu wanavyofikiri..my take:kwa kuwa inaonekana jeshi la police linataka kujisafisha na pia cdm ina wanasheria makini tusubiri tutaujua ukweli wa jambo hili.
 
Teknolojia inafanya mpaka lips ziende sawa na maneno? Unajua kuna watu wanaweza kuzima sauti wakasoma lips tu hizo wakakwambia huyu kasema nini hapa?

Sasa lips nazo wamechakachua mwanzo mpaka mwisho? Sauti yake? Anavyoongea?

Au unataka kusema picha yote ni Lwakatare, ni avatar tu?

Muungwana akikosea kukubali kosa na kuomba msamaha ni ada.

Ama sivyo kukataa kosa wakati watu wamemnasa kwenye tape ni kuongeza kosa.

This is sheer thuggery and mischief. Hiki ndicho chama mbadala tunachokitegemea kije kuiondoa CCM?

Hii ni strategy inayokubalika kichama au uhuni wake huyu mmoja tu na vi underdogs vyake?

Usituletee ufia dini kwenye siasa.
Nafikiri ni mapema sana kuihusisha na kujiuliza kuhusu CHADEMA na suala hili. Ni vizuri tusubiri jibu la swali lako la pili (bolded) kwanza. Lwakatare yupo na aseme nini kimetokea.
 
All in all..., hii nchi tumefika ambapo sipo.., watu waanze kutupwa ndani na tuache utani kwenye mambo serious.., uchunguzi ufanyike, ikigundulika kwamba watu walipanga mauaji, waliua au walisingizia wenzao (kugushi) basi wawekwe ndani huu sasa ushakuwa zaidi ya upuuzi (siasa mpaka kwenye maisha ya watu)

Yanawezekana hayo kwa wakati tulio nao?
 
Kwa maelezo yako inaonekena unafahamu vizuri hii clip ilivyotengenezwa halafu kwa kutaka kupoteza watu unaweka clip ya Obama. Tusiwe washahabiki wa masuala ambayo si ya afya kwa Taifa letu.

Kufuatia suala la Lwakatare kushika kasi humu jamvini, zimetokea hisia na mawazo tofauti sana baina ya wachangiaji mbalimbali juu ya mada hii ya kurecordiwa Lwakatare kupanga kumdhuru mwandishi. Wengi tulihoji sana uwezekano wa hii ishu kama ni halisi/si halisi. Kutokana na kuwa gizani kitechnologia, wengi hadi ninavyoongea hivi bado huwezi kuwabadilisha mawazo kuwa technolojia inaweza ikahusika katika kufake ile clip. Na kutokana na suala hili kugubikwa na propaganda za kisiasa, watu wamesahau hata technologia rahiti tu ya kuifanya midomo ya Cartoon icheze kulingana na maneno yanayotamkwa na cartoon/robot.

Kuweka kumbukumbu vizuri tarehe za mwanzon kabisa za mwaka huu mpya Mwigulu Nchemba alitueleza kuwa alikuwa na mkanda unaoonyesha viongoz (wengi) wa chadema kupanga mauaji. Mkanda umetoka tumeona kiongozi mmoja tu ndo anayepanga mauaji, kupungua kwa washiriki kutoka kwa viongoz hadi kiongozi, inahusishwa na ugumu uliopo wa kuinvolve watu wengi kwenye kufake/kulisha maneno watu wengi kwenye clip moja.

Aidha, baada ya tukio la utekwaji wa kibanda, wameibuka Nape na Ridhiwani hadharani na kuongea wakiwa na confinence ya 100% kuwa ''hawa wenzetu wa upinzani''/na ''safari hii pia mseme kuwa Ikulu/Rama/Magogoni ndio wanaohusika, kazi iliyopaswa kufanywa na vyombo vya dola. Siku chache baadaye Single ya Lwakatale ikatambulishwa rasmi kupitia Youtube na immediately ikatua jamvini na hata Polisi kuipata habari hii via Jamvini/Youtube na sio kwa Mwigulu. Sasa ukiconnect dots.......unaruhusiwa kabisa kufikiri kuwa tayari wenzetu wa upande wa pili walisha preview hii clip waliyoshiriki kuiandaa na ndo mana walikuwa na uhakika kuwa kwa level yetu ta technology, ni rahisi sana kushawishika kwa hii clip kuwa ni halisi.

Tulishasikia pia Wassira akitamka kuwa CDM lazima ife 2013, wengi hatukuelewa na hadi sasa hatujaelewa alikuwa anamaana gani kutamka maneno kama yale mtu wa makamo yulo. Sasa kauli za hivi za kumtamkia kifo mwenzio zinasignal kuwepo kwa mkakati wa maksudi wa kumuua mwenzio??Aidha, CCM katika vikao vyao vya CC/NEC, ccm walijadili kwa kina namna ya kudeal/kuisambaratisha CDM badala ya namna ya kutumikia umma wa watanzania waliowaweka madarakani. Hapa pia panazaa jambo.

Baada ya utanguliz huu naomba niimwage kwenu faked clip ya Barack Obama ili at least tujue tu kuwa suala la kulishwa maneno linawezekana. BOFYA A Bad Lip Reading of Barack Obama's Inauguration (Legendado PT-BR) - YouTube. Aidha, clip hii isikuzuie kuendelea kuamini unachokiamini, mimi nimeonelea tu niwafahamishe wale wote wenzangu ambao asubuh ya leo tulihisi sio kitu kinachowezekana hapa duniani.
 
naomba kama kuna uwezekano uongozi wa juu wa chama chetu tukufu CDM uje hapa utoe briefing japo kiduchu tu kuwa ni nini kinaendelea mpaka sahvi
 
Ni kweli mkuu aliye-record amechemka. Kwa mtu asiyefikiri vizuri ndo ataamini upuuzi huu. Kama kweli ni Great thinker utang'amua video ilivyo na makosa mengi ya kiufundi na kudhihirisha kuwa ni uwongo.

Ni vyema waandaaji wakajipanga kwa zile part wanazosema eti watazileta.

Mungu ni mwema sana na siku zote huwaumbua watu wenye nia mbaya. Hizi ni siasa za maji taka ambazo hazina tija na upepo utawapitia tu hata kama watatengeneza video mia moja na zaidi. Propaganda hizi ni za kitoto.

CCM na serikali yake wanapoteza muda badala ya kufikiri watawasaidiaje watanzania kuondokana na umaskini. Ni vigumu kuwadanganya na kuwaaminisha watanzania kwa video hii.

CHADEMA mtihani huu mtaushinda tu, mungu yuko nanyi na atawatia nguvu kuendelea na harakati za ukombozi.

Tatizo nyie mmeolewa na chadema hata ikifanya uozo mnautetea.
 
Kitu cha ajabu hata mkubwa anafurahia propaganda kama hizi za kitoto na za kipuuzi kweli mabwepande wameishiwa mbinu

kama ni propaganda za kitoto kwanini bado yuko ndani.si angeshaachiwa?watu hadi wamekwenda kupekua kwake
 
Songoro, tutakesha hapa naimani umeelewa what I mean! kwa manufaa ya kuitendea haki hii thread na kwa kuweka kumbukumbu vizuri, naomba nichomoe neno chadema ila niliweke neno ''hawa wenzetu wa upinzani'' kwa upande wa Nape na kwa Ridhwani, alisema na this time waseme Magogoni/Ikulu/Rama wamehusika tena.

Ila it all mean the same. Thinking tu ndo itakuwa imetufautiana ktk suala hili, wewe unaanzia kushoto kuja kati, mimi naanzia kulia kuja kati ila mwisho wa siku sote tutakutana kati tu.

Nadhani hili swala liende polisi na then mahakamni ili tusiendelee kulumbana. Mwigulu ni shaihidi wa kwanza atoe video zote kwa polisi wachunguze.
 
Tunachezeana michezo ya kitoto sana na ndo maana unaona kundi kubwa la wanaccm walijifanya Manabii wa kutabiri anguko la cdm, kumbe walishaidhinisha uandaliwaji wa hii movie, kumbuka kuwa wanawatu wao nje wanaoweza kuwajulisha hali ya technologia huko nje na hivyo kutumia utaratibu kama huu kuchafua hali ya kisiasa nchini. 2015 tutaelewana tu.

mimi ninavyo fikiri kama hii kitu ni fake CDM watoa tamko rasmi kukanusha na Lwakatare atokee hadharani (kwenye media) akanushe, vilevile ili kundoa uchafu huu wataalam (hata kama watakua wa nje) kusoma clip watafutwe na watoe tamko lao kama hii kitu ni fake au sio otherwise as i see it tunaenda kubaya! ila ukweli siku zote upo pale pale hata kama unauma!
 
Lakini mwisho wa siku ukweli utajulikana, tuuwaache watu wachunguze kwa makini kabisa ili waje na vitu ambavyo vitaondoa maneno maneno na uvumi ili sheria ichukue mkondo wake, sidhani kama kuna mtu anapenda vitendo hivi vya mauaji vinavyoendelea sijui hii nchi hivi sasa inaelekea wapi? tufahamu kuwa katika haya kuna watu wanaona ufahari kudhamini makundi maovu kwa ajili ya kufanya vitendo ambavyo vinalengo la kutuvuruga sisi watanzania tuishi kwa hofu na mashaka ya uhai wetu, Serikali isione haya wala huruma wanapowakamata watu hawa wachache wenye lengo baya na watanzania kwa kutufanya tushindwe kuendelea na shughuli zetu kwa maslahi yao au ya waliowatuma, kama mtu akikamatwa na kitu kinachochea uvunjifu wa amani ama kupanga mkakati wa kufanya mauaji kwa ndugu zetu, kaka zetu baba zetu wafanyakazi wenzetu tumuache ahojiwe/wahojiwe ili waweze kuthibitisha ikibainika kama ni kweli basi Serikali imshughulikie kwa maana tusipo lidhibiti hili huko tunakokwenda hatuta kuwa salama.
 
Mkuu wangu Patriote,
Waingereza wana msemo wao kwamba "A BLACK CAT MAY BE A BAD LUCKY ONLY IF YOU ARE MOUSE!" Chambilecho wewe sio panya, yanini kuingiwa taharuki pindi umwonapo paka?! Naona wapwa mmekazana sana kulikanusha hili jambo....pamoja na post kadhaa za kukanusha, bado hivi sasa kuna new threads za kukanusha...!! Hofu ya nini? I believe Lwakatare is smart enough ku-prove beyond reasonable doubt kwamba ile video is just a fabricated material; sasa nyie hofu yenu nini mkuu wangu Patriote? Mnatutia mashaka sie wengine; a black cat may be a bad luck only if you're mouse! Wewe majani, hofu yako nini kuingizwa kwenye banda la mbwa wakati unafahamu mbwa hali majani?! Unakumbuka pale Uhuru Kenyatta alipojipeleka mwenyewe ICC? Kenyatta alifahamu he's not a mouse so he'd no reason to get scared of a balck cat ICC!! Wewe kama ni majani, pigana kufa na kupona, ikibidi kanusha kwa nguvu zote kwamba wewe si majani ikiwa umegundua unataka kupelekwa zizi la mbuzi, lakini kwenye banda la mbwa; aaaargh, hofu ya nini!!!


hatari sana,i am glad kwakatare is not a Muslim
tungeskia mengi sana katika hilo,
wala hatuskii akinyooshewa kidole kutokana na iman yake hapo..!
Kama kina shekhe ilunga,ila tutafika tuh
 
Kufuatia suala la Lwakatare kushika kasi humu jamvini, zimetokea hisia na mawazo tofauti sana baina ya wachangiaji mbalimbali juu ya mada hii ya kurecordiwa Lwakatare kupanga kumdhuru mwandishi. Wengi tulihoji sana uwezekano wa hii ishu kama ni halisi/si halisi. Kutokana na kuwa gizani kitechnologia, wengi hadi ninavyoongea hivi bado huwezi kuwabadilisha mawazo kuwa technolojia inaweza ikahusika katika kufake ile clip. Na kutokana na suala hili kugubikwa na propaganda za kisiasa, watu wamesahau hata technologia rahiti tu ya kuifanya midomo ya Cartoon icheze kulingana na maneno yanayotamkwa na cartoon/robot.Kuweka kumbukumbu vizuri tarehe za mwanzon kabisa za mwaka huu mpya Mwigulu Nchemba alitueleza kuwa alikuwa na mkanda unaoonyesha viongoz (wengi) wa chadema kupanga mauaji. Mkanda umetoka tumeona kiongozi mmoja tu ndo anayepanga mauaji, kupungua kwa washiriki kutoka kwa viongoz hadi kiongozi, inahusishwa na ugumu uliopo wa kuinvolve watu wengi kwenye kufake/kulisha maneno watu wengi kwenye clip moja. Aidha, baada ya tukio la utekwaji wa kibanda, wameibuka Nape na Ridhiwani hadharani na kuongea wakiwa na confinence ya 100% kuwa ''hawa wenzetu wa upinzani''/na ''safari hii pia mseme kuwa Ikulu/Rama/Magogoni ndio wanaohusika, kazi iliyopaswa kufanywa na vyombo vya dola. Siku chache baadaye Single ya Lwakatale ikatambulishwa rasmi kupitia Youtube na immediately ikatua jamvini na hata Polisi kuipata habari hii via Jamvini/Youtube na sio kwa Mwigulu. Sasa ukiconnect dots.......unaruhusiwa kabisa kufikiri kuwa tayari wenzetu wa upande wa pili walisha preview hii clip waliyoshiriki kuiandaa na ndo mana walikuwa na uhakika kuwa kwa level yetu ta technology, ni rahisi sana kushawishika kwa hii clip kuwa ni halisi.Tulishasikia pia Wassira akitamka kuwa CDM lazima ife 2013, wengi hatukuelewa na hadi sasa hatujaelewa alikuwa anamaana gani kutamka maneno kama yale mtu wa makamo yulo. Sasa kauli za hivi za kumtamkia kifo mwenzio zinasignal kuwepo kwa mkakati wa maksudi wa kumuua mwenzio??Aidha, CCM katika vikao vyao vya CC/NEC, ccm walijadili kwa kina namna ya kudeal/kuisambaratisha CDM badala ya namna ya kutumikia umma wa watanzania waliowaweka madarakani. Hapa pia panazaa jambo.Baada ya utanguliz huu naomba niimwage kwenu faked clip ya Barack Obama ili at least tujue tu kuwa suala la kulishwa maneno linawezekana. BOFYA A Bad Lip Reading of Barack Obama's Inauguration (Legendado PT-BR) - YouTube. Aidha, clip hii isikuzuie kuendelea kuamini unachokiamini, mimi nimeonelea tu niwafahamishe wale wote wenzangu ambao asubuh ya leo tulihisi sio kitu kinachowezekana hapa duniani.
ahaa, kumbe kwao kuibemenda ELIMU ni MTAJI ili watuburuze watakavyo!
 
Mkuu wangu Patriote,
Waingereza wana msemo wao kwamba "A BLACK CAT MAY BE A BAD LUCKY ONLY IF YOU ARE MOUSE!" Chambilecho wewe sio panya, yanini kuingiwa taharuki pindi umwonapo paka?! Naona wapwa mmekazana sana kulikanusha hili jambo....pamoja na post kadhaa za kukanusha, bado hivi sasa kuna new threads za kukanusha...!! Hofu ya nini? I believe Lwakatare is smart enough ku-prove beyond reasonable doubt kwamba ile video is just a fabricated material; sasa nyie hofu yenu nini mkuu wangu Patriote? Mnatutia mashaka sie wengine; a black cat may be a bad luck only if you're mouse! Wewe majani, hofu yako nini kuingizwa kwenye banda la mbwa wakati unafahamu mbwa hali majani?! Unakumbuka pale Uhuru Kenyatta alipojipeleka mwenyewe ICC? Kenyatta alifahamu he's not a mouse so he'd no reason to get scared of a balck cat ICC!! Wewe kama ni majani, pigana kufa na kupona, ikibidi kanusha kwa nguvu zote kwamba wewe si majani ikiwa umegundua unataka kupelekwa zizi la mbuzi, lakini kwenye banda la mbwa; aaaargh, hofu ya nini!!!

Sio kulikanusha, ila kuelimisha watu waelewe. Hauwezi kukaa kimya wakati unaona watu wanapotosha kwa maslahi ya taifa. Elewa hii ni mikakati ya kishenzi ya kisiasa.
 
mimi ninavyo fikiri kama hii kitu ni fake CDM watoa tamko rasmi kukanusha na Lwakatare atokee hadharani (kwenye media) akanushe, vilevile ili kundoa uchafu huu wataalam (hata kama watakua wa nje) kusoma clip watafutwe na watoe tamko lao kama hii kitu ni fake au sio otherwise as i see it tunaenda kubaya! ila ukweli siku zote upo pale pale hata kama unauma!
Kuna vitu vya kutolea matamko. shida ya magamba ni kuona CDM wanatoa tamko ndipo na wao waanzie hapo malumbano.

Suala hili ni la kijinai, acha liende kwa mkondo wa kisheria kuliko kutoa matamko ya kisiasa.

Chadema msitoe tamko kwenye huu upuuzi
 
Nadhani wenye maamuzi ya mwisho ni polisi, pamoja na kwamba mtuhumiwa ametokea upinzani, nitawaomba polisi wetu wasitumie upinzani kama kigezo cha kumhukumu mtuhumiwa. Lwakatare apewe haki yake kama Lwakatare na kama raia mwingine yeyote wa nchi hii.. Nadhani aliyeweka hii video alikuwa na mawazo hasi na upinzani ndiyo maana anawauliza wa "CHADEMA, hapa Lwakatare anamaanisha nini?.. Kwa uelewa wangu huyu mtu hana dhamira njama kwa Nchi yetu ya Tanzania, anaweza kuwa mtu hatari sana katika mipango na mikakati yote ilyokwisha ripotiwa ya mauaji, utekaji na uumizwaji wa raia, waandishi na wanaharakati mbalimbali hapa Tanzania. Nadhani Polisi wangeanza na huyu mtu angeweza kuwasaidia sana katika utekelezaji na upelelezi wa makosa yanayofanana na haya. Nachoona hapa ni hiki,.

  1. Mweka video alishiriki katika kuiandaa clip hii kikamilifu.
  2. Anatumiwa na watu wasiyoitakia mema Nchi yetu ya Tanzania,
  3. Ana mtandao ambao huratibu uchafu wote unaofanywa na hawa magaidi ndiyo maana anahisisha mambo ya utekaji yanayoendelea hapa nchini na vyama vya upinzani hususani CDM.
  4. Anaweza kuwa ni mtu wa system mwenye dhamana ndiyo maana hakupeleka hii clip sehemu husika kama kituo cha polisi akiogopa atatoa ushirikiano ambao utamfanya ajulikane..
  5. Anaweza akawa anajua ukweli wa mambo mengi sana maovu yanayotokea hapa nchini ya kihalifu na kigaidi, na kama ni mwandishi wa habari, anafaa zaidi katka upelelezi.
Rai yangu njema, nawaaomba polisi wamsake huyu mtu atawasaidia sana katika kubaini njama mbalimbali za uovu zinazoendelea hapa nchini.. Kama ni mtu mwenye nia njema atajitokeza ili awasaidie polisi katika kufahamu mambo yafuatayo.
  1. Hizo video nyingine za mikakati ya mauaji
  2. Sehemu ilitumika katika kurekodia video hizi,
  3. Mtu/taasisi iliyo nyuma yao katika kufadhili mpango huu,
  4. mbinu nyingine chafu ambazo wameshafanikisha na ambazo ziko kwenye pipeline.

Nawasilisha...
 
Mkuu patriote,
mi naamini ni yeye lwakatare, isipokuwa amechezewa mtego na anaowaamini. Mambo haya ya kutafutana na kuwindana kujua nani mbaya na nani adui wa chama ni ya kawaida kwenye siasa na hata kwenye biashara kubwa..

Kilichomtokea Lwakatare ni imani kupita kiasi kwa vijana wake wa upelelezi. Haonekani kuzungumzia mauaji wala kupiga mtu lakini inavyoônyesha alitaka kumtisha huyo adui yake. Walichokifanya watu wake ni kumchokoza tu nae akaingia mkenge kwa kudhani ni ishu ya kawaida ya mazungumzo ya kirafiki.

kudeal na Ccm ni kudeal na wakubwa, kwa ukuaji wa Chadema wa spidi ya namna hii Ccm wako radhi kutoa pesa yoyote wapate information za kukivuruga chama. Hawa vijana wamemuuza Rwakatare kwa vipande vya fedha.

lakini pia kwa kuisikiliza clip hii ni wazi Rwakatare hajui chochote kuhusiana na masuala ya utekaji au mauaji., nasema hivyo kwa sababu hajuihata dawa za usingizi au spray zinauzwaje, nadhani ndo kwanza anajifunza. Pili hakuwatuma kuua bali kumteka kwa lengo la kumtisha. Hatahivyo muda utatupa picha kamili

Hakika akili ni nywele. Ukizaliwa mbishi unaweza kubishana na technology huku ukiweka kando akili ya kawaida ambayo ingesaidia japo kidogo kudadavua issues.

Time will tell
 
Back
Top Bottom