Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

JESHI la Polisi nchini limemkamata Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya mashambulizi dhidi ya watu hapa nchini.
Taarifa kutoka Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA Kinondoni jijini Dar es Salaam zilieleza kwamba Lwakatare alikamatwa saa 7 mchana na watu wanne waliojitambulisha kama maofisa wa Jeshi la Polisi ambao walifika na gari aina ya Toyota Land Cruiser jeupe lenye namba za usajili T 140 BLA likiwa na chata ya kitalii.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alisema Lwakatare amekamatwa kwa tuhuma zilizosambazwa kwenye mtandao.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Hamad Yusufu Musa, ambaye alishuhudia tukio la kukamatwa kwake, aliliambia Tanzania Daima kuwa kiongozi huyo anatuhumiwa kupanga njama za matukio ya kushambulia raia yaliyotokea hapa nchini.
Hata hivyo Musa hakusema ni matukio gani yanayomhusisha kigogo huyo, lakini mtu aliyesambaza mkanda wa video katika mitandao ya kijamii jana aliandika chini yake maneno yasemayo: ‘Mikakati ya mateso ya Kibanda na mwandishi mwandamizi wa gazeti la Mwananchi, mhusika mkuu huyu hapa.' akimaanisha Lwakatare.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kukamatwa kwa Lwakatare na kuhusishwa na matendo hayo ya utekaji na kushambulia watu, kumedhihirisha kuwapo kwa njama chafu zenye lengo la kukichafua chama hicho mbele ya jamii.
Dk. Slaa alisema njama hizo zinaratibiwa na kigogo mmoja serikalini ambaye analitumia Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola kuidhoofisha CHADEMA.

"Ikiwa ni kweli wanamshikilia kutokana na hiyo video, ni furaha kwetu, kwa sababu ukombozi wa nchi umekaribia," alisema bila kufafanua.
Hata hivyo Dk. Slaa alisema ameshangazwa na uharaka wa polisi wa kumkamata Lwakatare siku moja tu baada ya video hiyo kuwekwa mtandaoni, na kuacha hata kumhoji mmoja wa mawaziri aliyetajwa na baadhi ya magazeti jana akihusishwa kutekwa na kuteswa kwa Kibanda.

"Waziri hajakamatwa wala kuhojiwa, alitekwa Ulimboka akamtaja ofisa wa Ikulu, lakini hajakamatwa wala kuitishwa gwaride la utambulisho.

"Aliuawa kinyama Mwangosi (Daudi Mwangosi), katikati ya kundi la maofisa wa polisi na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, lakini hakuna aliyechukuliwa hatua. Lakini kwa video ambayo haijulikani asili yake, polisi wameharakisha kumkamata na kumpekua nyumbani kwake, kulikoni?" alihoji Dk. Slaa.

Alisema ni wazi kwamba sasa lazima Watanzania wafumbue macho na wajue ukweli ulivyo na namna polisi wanavyotumika kuiangamiza CHADEMA, lakini akadai kuwa ukweli utajulikana muda si mrefu.
Wakili wa Lwakatare, Nyaronyo Kicheere, akizungumza na gazeti hili, alisema mteja wake majira ya saa 10 alikwenda kupekuliwa nyumbani kwake Kimara.
"Kwa sasa tumeshafika nyumbani kwa Lwakatare Kimara King'ong'o na maofisa wapatao saba wanaendelea na upekuzi katika nyumba yake," alisema mwanasheria huyo.
 
Ni ngumu kujadili jambo la kiusalama/kimafia kama hili kwenye public na mahali pasipo na usalama/utulivu. Ukiangalia hii clip utaona wanazungumza mahali pawazi sana ambapo watu wanaingia na kutoka na hata kupita karibu kabisa na mazungumzo yanpofanyika
Pili, kwa taratibu za usalama tena kwa high level ya mtu kama huyu ambaye ni kamanda wa kitaifa, ni ajabu kuwa wanajadili jambo senstive kama hili na watu hawajasachiwa kuhakiki hawana vifaa vya kurecord au kupiga picha. Otherwise kazi ya usalama imepewa the wrong person ambaye hata hajuni nini kinatakiwa
Ukitazama hiyo video kwa makini hapo mwanzoni, utaona kuwa kurekodiwa haikua jambo la siri. Ingawa video inaoneakana kama vile anarekodiwa bila kujijua lakini ukweli ni kuwa anajua. Utaona hata posisition ya kamera imekaa mahali sahihi kabisa na stable. Ila mwanzoni utasikia kabisa yeye mwenyewe akiongele kuweka mic vizuri kabla hajaanza kuongea
Swali linaloibuka alikua anaongea na kujirekodi au kurekodiwa ili apeleke wapi au atumie kama kumbukumbu ya kitu gani?
Unapomsikiliza pale anapoanza kusisitiza kwa nini huyo mwandishi anahitaji kushughulikiwa, utaona jinsi anavyolazimisha kulink wanachotaka kukifanya na matukio mengine ya Igunga na Morogoro...lakini huoni link hasa ya anachokisema na hayo matukio. Ambapo ukichunguza sana utaona kama vile analazimisha ionekana chama chao ndio kilihusika kutekeleza yaliyotokea. At the same time anachoagiza sasa ni kumtisha mtu bila kumdhuru
 
Ama kweli Magamba Mafia khaa!
Wamekisuka kitu utasema movie!
 
Yote yanawezekana tusubiri kauli ya Cdm.
Kufuatia suala la
Lwakatare kushika kasi humu jamvini, zimetokea hisia na mawazo tofauti
sana baina ya wachangiaji mbalimbali juu ya mada hii ya kurecordiwa
Lwakatare kupanga kumdhuru mwandishi. Wengi tulihoji sana uwezekano wa
hii ishu kama ni halisi/si halisi. Kutokana na kuwa gizani
kitechnologia, wengi hadi ninavyoongea hivi bado huwezi kuwabadilisha
mawazo kuwa technolojia inaweza ikahusika katika kufake ile clip. Na
kutokana na suala hili kugubikwa na propaganda za kisiasa, watu
wamesahau hata technologia rahiti tu ya kuifanya midomo ya Cartoon
icheze kulingana na maneno yanayotamkwa na cartoon/robot.

Kuweka kumbukumbu vizuri tarehe za mwanzon kabisa za mwaka huu mpya
Mwigulu Nchemba alitueleza kuwa alikuwa na mkanda unaoonyesha viongoz
(wengi) wa chadema kupanga mauaji. Mkanda umetoka tumeona kiongozi mmoja
tu ndo anayepanga mauaji, kupungua kwa washiriki kutoka kwa viongoz
hadi kiongozi, inahusishwa na ugumu uliopo wa kuinvolve watu wengi
kwenye kufake/kulisha maneno watu wengi kwenye clip moja.

Aidha, baada ya tukio la utekwaji wa kibanda, wameibuka Nape na
Ridhiwani hadharani na kuongea wakiwa na confinence ya 100% kuwa ''hawa
wenzetu wa upinzani''/na ''safari hii pia mseme kuwa Ikulu/Rama/Magogoni
ndio wanaohusika, kazi iliyopaswa kufanywa na vyombo vya dola. Siku
chache baadaye Single ya Lwakatale ikatambulishwa rasmi kupitia Youtube
na immediately ikatua jamvini na hata Polisi kuipata habari hii via
Jamvini/Youtube na sio kwa Mwigulu. Sasa ukiconnect
dots.......unaruhusiwa kabisa kufikiri kuwa tayari wenzetu wa upande wa
pili walisha preview hii clip waliyoshiriki kuiandaa na ndo mana
walikuwa na uhakika kuwa kwa level yetu ta technology, ni rahisi sana
kushawishika kwa hii clip kuwa ni halisi.

Tulishasikia pia Wassira akitamka kuwa CDM lazima ife 2013, wengi
hatukuelewa na hadi sasa hatujaelewa alikuwa anamaana gani kutamka
maneno kama yale mtu wa makamo yulo. Sasa kauli za hivi za kumtamkia
kifo mwenzio zinasignal kuwepo kwa mkakati wa maksudi wa kumuua
mwenzio??Aidha, CCM katika vikao vyao vya CC/NEC, ccm walijadili kwa
kina namna ya kudeal/kuisambaratisha CDM badala ya namna ya kutumikia
umma wa watanzania waliowaweka madarakani. Hapa pia panazaa jambo.

Baada ya utanguliz huu naomba niimwage kwenu faked clip ya Barack Obama
ili at least tujue tu kuwa suala la kulishwa maneno linawezekana.
BOFYA
A
Bad Lip Reading of Barack Obama's Inauguration (Legendado PT-BR) -
YouTube
.
Aidha, clip hii
isikuzuie kuendelea kuamini unachokiamini, mimi nimeonelea tu
niwafahamishe wale wote wenzangu ambao asubuh ya leo tulihisi sio kitu
kinachowezekana hapa duniani.
 
Kama polisi wameamini video za mtandaoni,kwa nini wasiende kwa mwigilu wakachukue na ile aliyonayo? Mwigilu alishasema anayo video sasa wanasubiri nini kumkamata na kuifanyia kazi hiyo video?
 
Technologia ni dynamic, watu wanakesha Lab kufanya kazi na kuimprove performance/accurace/precision etc ya hivi vitu. Mwanzo ilisemekana midomo kucheza sambamba na maneno, ni kitu kisichowezwa kuigizwa, nadhan kwa hilo clip hii imefanikiwa kuli prove wrong, mmebaki na point ya aina za sauti. Haya ngoja tuzame tutakuja na yenye sauti halisi kama hiyo wewe unaiona sio sauti inayotoka kwa muongeaji, Stay tuned!!

angalia iyo video apo chini uyu jamaa ni mchekeshaji bingwa wa kuiga sauti na utaona sauti pia sio issue watu wanaiga!!!!

Aries Spears - Arnold Schwarzenegger Impression (+ Pacino vs. DeNiro in "Heat") - YouTube
 
Asante Mkuu kwa kuwang'amua wenye akili nyepesi (wasiotaka kufikiri) kwa clip hii ya Obama. Nadhani sasa watatuelewa tunapowaambia kuwa video ya Lwakatare ni feki. Ukilinganisha ya Obama na ya kwao utaona utofauti wa quality, hata hivyo ya Obama nayo ina mapungufu lukuki ukianzia na sauti sio ya Obama japo waliweza sana hucheza na Mdomo wake.

Ridhiwani na Nape wanafanya mipango ya kitoto na kwamba wanataka kutuvulugia amani ya nchi yetu kwa kuchonganisha chadema na wananchi.

CCM na serikali yake wanatapatapa na kuhangaika kadri siku zinavyoenda na 2015 watakuwa wamemaliza uongo wote. Na hizi ni dalili za kushindwa
Kama ni kweli, binaadamu amefikia kiwango hiki? Basi dunia imekwisha, aliyetengeza hii vidio ameshalaanika, angoje matokeo ya laana. Kumbuka Mungu ni upendo, usipompenda binaadamu mwenzako, huwezi kumpenda Mungu.
 
All in all..., hii nchi tumefika ambapo sipo.., watu waanze kutupwa ndani na tuache utani kwenye mambo serious.., uchunguzi ufanyike, ikigundulika kwamba watu walipanga mauaji, waliua au walisingizia wenzao (kugushi) basi wawekwe ndani huu sasa ushakuwa zaidi ya upuuzi (siasa mpaka kwenye maisha ya watu)

Umesema sawa vema kabisa! Lakini kule ndago baada ya mkutano wa chadema kuna mtu aliuawa! Na kesi ipo mahakamani na mpaka polisi wametoa ushahidi mahakamani kuwa kuna mbunge mmoja anahusika. Jeee mbona hakamatwi??????
 
Kwa mtazamo wangu.Hii ni jinai.Kama ningekua ni spokesman wa CHADEMA ningesema hii ni ishu ya jinai mahakama ndo iamue ukweli ujulikane.Simple.Pia Mwigulu LAZIMA sasa ahojiwe apeleke hiyo clip aliyokua anadai anayo.Hakuna mtu aliye CHADEMA atakayependa ukweli kua chama kinatekeleza mateso kwa watu.Endapo ukweli huo upo
 
. Rwakatare anaonyesha yeye sio "right person" kwa issue za kiusalama, ndio maana amaweza kurekodiwa ki mburula kabisa!
Politics is a very "dirty game!".

Pasco.

They say, "When you pick up one end of the stick, you pick up the other"

Every choice we make has its consequences
 
ccm sasa inaelekea kwenye ufascist baada ya kushindwa kuweka utawala bora.
 
Wana mapinduzi wanaamini kuwa ukiona mambo kama haya tambua kuwa ukombozi upo karibu. Uhuru na Ruto walifanya kama haya na sasa wameingia ikulu, aibu kwa ICC na mafia wao. Nadhani ni muda wa kushangilia ushindi na mapinduzi ya kweli, watanzania wenye akili, na hasa hawa wanaotumia mitandao ya kijamii na forum makini kama JF watatumia akili zao kuchambua hili. Maana mengi yamesemwa kuhusu CHADEMA yameshindwa....walianza na ukanda ukashindwa, wakaja na dini wakashindwa, wakaja na kadi ya dokta Slaa wakashindwa, sasa wemeibuka na mauaji...hakika MUNGU ni yule yule jana, leo na hata milele, ataendelea kutupigania wana CHADEMA.

Tualianza na MUNGU, tunaendelea na MUNGU, tutamaliza na MUNGU
Ikiwa MUNGU, yupo upande wetu, nani atanyanyuka kinyume chetu?

umenena kweli kweli mkuu, na hakuna njia iliyo rahisi ktk kutafuta ushindi. Milima ni mingi sana na yote yatakiwa kuipanda ili kufika kileleni.
 
kwa akili yake haoni uzito wa lwakatare pale cdm,yeye hajui kwamba ukiugusa ulinzi ndio umekigusa chama kabisa kwamba akituhumiwa yule ndio cdm inavyoendeshwa.ila tunatofautiana kuelewa majambo tofauti tofauti
Kaliweka hivyo ili kupunguza umoja kati ya watendaji wa chama ili wamwachie suala hili Lwakatare afe nalo ili baadaye sasa ndio wakiingize chama matopeni baada ya kummaliza Lwakatare. Huyo jamaa ni kama afsa Propaganda wa magamba. Ndiye aliyezuia maandamano kwa kugeuka mtabiri wa matukio kuwa Al Shabaab wangeshambulia maandamano ya CDM. Siku chache baadaye akaruhusu kusanyiko kubwa siku ya kukumbuka Uhuru. Sasa huyo c mwanapropaganda tu???
 
Fubricated clip ya Lwakatare ndo silaha ya mwisho ya maangamizi waliyokuwa wamesalia nayo magambaz. Baada ya kuumbuka wameanza kutoweka mmoja baada ya mwingine.
 
jifunze kuwa makini umesema wameitaja hadharani Chadema thibitisha usianze style za kukwepakwepa, mwenzio kubenea walau alikuwa akitumia ' wachambuzi wa kisiasa au vyanzo vya kuaminika vinasema Nape/Ridhwan walikuwa WAKIMAANISHA........' badala ya style uliyotumia kuwalisha watu maneno ambayo sote nawe unajua hawakutamka kama unavyojifanya mtaalam wa kupima confidence zao kwa asilimia eti wakiwa na confidence 100%!

Heshima kwako mkuu Songolo. Hebu jaribu kupitia vizuri thread ya Patriote uone kama kuna sehemu amedai chadema kutajwa waziwazi. Amesema "Hawa wenzetuu wa upinzani". tatizo liko wapi hapo?
 
Kufuatia suala la Lwakatare kushika kasi humu jamvini, zimetokea hisia na mawazo tofauti sana baina ya wachangiaji mbalimbali juu ya mada hii ya kurecordiwa Lwakatare kupanga kumdhuru mwandishi. Wengi tulihoji sana uwezekano wa hii ishu kama ni halisi/si halisi. Kutokana na kuwa gizani kitechnologia, wengi hadi ninavyoongea hivi bado huwezi kuwabadilisha mawazo kuwa technolojia inaweza ikahusika katika kufake ile clip. Na kutokana na suala hili kugubikwa na propaganda za kisiasa, watu wamesahau hata technologia rahiti tu ya kuifanya midomo ya Cartoon icheze kulingana na maneno yanayotamkwa na cartoon/robot.

Kuweka kumbukumbu vizuri tarehe za mwanzon kabisa za mwaka huu mpya Mwigulu Nchemba alitueleza kuwa alikuwa na mkanda unaoonyesha viongoz (wengi) wa chadema kupanga mauaji. Mkanda umetoka tumeona kiongozi mmoja tu ndo anayepanga mauaji, kupungua kwa washiriki kutoka kwa viongoz hadi kiongozi, inahusishwa na ugumu uliopo wa kuinvolve watu wengi kwenye kufake/kulisha maneno watu wengi kwenye clip moja.

Aidha, baada ya tukio la utekwaji wa kibanda, wameibuka Nape na Ridhiwani hadharani na kuongea wakiwa na confinence ya 100% kuwa ''hawa wenzetu wa upinzani''/na ''safari hii pia mseme kuwa Ikulu/Rama/Magogoni ndio wanaohusika, kazi iliyopaswa kufanywa na vyombo vya dola. Siku chache baadaye Single ya Lwakatale ikatambulishwa rasmi kupitia Youtube na immediately ikatua jamvini na hata Polisi kuipata habari hii via Jamvini/Youtube na sio kwa Mwigulu. Sasa ukiconnect dots.......unaruhusiwa kabisa kufikiri kuwa tayari wenzetu wa upande wa pili walisha preview hii clip waliyoshiriki kuiandaa na ndo mana walikuwa na uhakika kuwa kwa level yetu ta technology, ni rahisi sana kushawishika kwa hii clip kuwa ni halisi.

Tulishasikia pia Wassira akitamka kuwa CDM lazima ife 2013, wengi hatukuelewa na hadi sasa hatujaelewa alikuwa anamaana gani kutamka maneno kama yale mtu wa makamo yulo. Sasa kauli za hivi za kumtamkia kifo mwenzio zinasignal kuwepo kwa mkakati wa maksudi wa kumuua mwenzio??Aidha, CCM katika vikao vyao vya CC/NEC, ccm walijadili kwa kina namna ya kudeal/kuisambaratisha CDM badala ya namna ya kutumikia umma wa watanzania waliowaweka madarakani. Hapa pia panazaa jambo.

Baada ya utanguliz huu naomba niimwage kwenu faked clip ya Barack Obama ili at least tujue tu kuwa suala la kulishwa maneno linawezekana. BOFYA A Bad Lip Reading of Barack Obama's Inauguration (Legendado PT-BR) - YouTube. Aidha, clip hii isikuzuie kuendelea kuamini unachokiamini, mimi nimeonelea tu niwafahamishe wale wote wenzangu ambao asubuh ya leo tulihisi sio kitu kinachowezekana hapa duniani.

Thanks mkuu.
 
Asante kwa kutuelimisha mkuu, naomba message hii uwatumie pia clouds fm maana wanaendelea kuitangaza ile video clip fake.
 
Kwa mtazamo wangu.Hii ni jinai.Kama ningekua ni spokesman wa CHADEMA ningesema hii ni ishu ya jinai mahakama ndo iamue ukweli ujulikane.Simple.Pia Mwigulu LAZIMA sasa ahojiwe apeleke hiyo clip aliyokua anadai anayo.Hakuna mtu aliye CHADEMA atakayependa ukweli kua chama kinatekeleza mateso kwa watu.Endapo ukweli huo upo
Jana ulisema utarudisha kadi ya chadema, umesharudisha?
 
Back
Top Bottom