Mkuu niwie radhi nimeanzisha meza hii kwa jicho makini baada ya kuidownload na kuipitsha kwenye softiware makini kuboost na picha hivyo tujadili.
Ni kweli mkuu aliye-record amechemka. Kwa mtu asiyefikiri vizuri ndo ataamini upuuzi huu. Kama kweli ni Great thinker utang'amua video ilivyo na makosa mengi ya kiufundi na kudhihirisha kuwa ni uwongo.
Ni vyema waandaaji wakajipanga kwa zile part wanazosema eti watazileta.
Mungu ni mwema sana na siku zote huwaumbua watu wenye nia mbaya. Hizi ni siasa za maji taka ambazo hazina tija na upepo utawapitia tu hata kama watatengeneza video mia moja na zaidi. Propaganda hizi ni za kitoto.
CCM na serikali yake wanapoteza muda badala ya kufikiri watawasaidiaje watanzania kuondokana na umaskini. Ni vigumu kuwadanganya na kuwaaminisha watanzania kwa video hii.
CHADEMA mtihani huu mtaushinda tu, mungu yuko nanyi na atawatia nguvu kuendelea na harakati za ukombozi.
Wewe ni mmoja wa walishiriki kuiratibu....
Nimekupata kiongoz, nilijua umeamua tu kuanzisha uzi mpya, kama kuna new findings, endelea tu kiongoz, tupo pamoja!
Namba mbili mkuu ndiomaana nasema wamechemka maana wangeishusha ubora hiyo video na kuiongezea picture noise kidogo ingeaminika. Mtanzania wa leo sio wa jana.
Kilichobaki kutoka CCM ni kuwachanga wapira kura kwa propaganda nyepesi.
Huu mpango wa magamba ni usanii wa hatari
kila mtu ni kuhangaika tu au huelewi? sisi cdm tunahangaika na video ya lwakatare kama unavyosema sawasawa tu na jinsi ninyi ccm mnavyohangaika na cdm
no need of CDM again in this country!
Hii video itawatesa sana naona mnajaribu kufanya cover up lakini ukweli huu wa vitendo vya utesaji ambao umekua ukifanywa na kitengo cha ulinzi na usalama ndani ya chadema utaishi muda mrefu sana.
Mtaona mengi safari hii. Mwl. kila mbinu chafu itatumika, ila itakapofika mahakamani ndipo mbivu na mbichi zitajulikana, huko hata suala la Dr. Ulimboka litaanikwa.