Kwa jinsi walivyopanga,ni kama vile hii camera iko ktk mavazi ya anayemsikiliza.sasa camera za aina hii haziwezi kuwa na quality kubwa kiasi hiki.pili camera isingetulia kiasi hicho.ingekuwa inatikisika.sasa kama haitikisiki,ni wazi ilikuwa juu ya kitu stationary.sasa huyu amekaa mezani,kwa lengo la kuzungumza na wageni wanaokaa kwenye viti mbele ya meza yake,how come kuwe na kitu stationary eneo ambalo palipaswa kuwa na viti wakae watu.hata tukisema kuna viti labda viwili,kimoja akakaa anaerekodi,cha pili akaweka labda begi au kitu kilichokuwa na camera,it's difficult to get that quality,utulivu na angle hiyo tena bila lwakatare mwenyewe kujua.hata useme aliweka kitu chenye camera kwa siri mezani bado ni ngumu kupata picha nzuri na iliyotulia na kwa angle iliyomjaza vizuri hivyo.tatu,ukimtazama usoni Lwakatare anaonekana kama mtu anayejitahidi kukwepesha macho yake kutoka camera ilipo.nne,angalia mkono wake muda wote unaandika eneo lile lile la karatasi.tano,ukiutazama uso na matendo yake,kwa sie tunaojua psychology,havioani na mwonekano wa mtu anayeelekeza wenzie kumuua binadamu seriously!haingii akilini!