Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Kasoro kubwa katika video ya Lwakatare

Nawe ni wapi jamaa amesema kuwa Nepi na kaka yake mwanasha wameitaja Chadema
Ukiwa mnafiki uwe na kumbukumbu, na wewe umetumia teknolojia gani kumlisha maneno Riz wan na Nape kuwa wamesema Chadema wanahusika, Wengi wetu tulipitia Wall paper ya Ridh na Nape hakuna neno Chadema walipotaja, Alama za Mtu mnafiki ni 3 na moja wapo ni Uongo.Lwakatare kesha nasa kwenye mtego hateguliwi kwa manati mtazid kumuumiza! Yeye ndo atathibitisha sio kukimbilia kwenye Google Engine kutafuta namna ya kumtoa!
 
Maneno na vitendo vyenu vinafanana na ukweli wa haya anayosema mkuu wenu wa usalama
Nchii hii ina demokrasia ya kuchagua lakini wenzetu naaona mnachukua staili ya taliban


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
video ya rwakatare ni mbinu mpya za kelelectronic ambazo magaidi wanatumia kutimiza malengo yao. Mafunzo ya kigaidi huko somalia hayaishii kuua na kuchoma makanisa tu bali pamoja na wizi kwenye mabenki na utapeli wa ki-electronic. Hebu tazama hii!!! Ukiwa na akili timamu utaamini kwamba obama aliyasema haya? "inauguration 2013: A bad lip reading:

mkuu nimekupata ccm wajinga sana wanataka tuingie kwenye vita kwa ulafi wa madaraka
 
Ushabiki na mapenzi ya kisiasa hapa JF umefikia pabaya sana, hasa ukiangalia juhudi hapa jamvini za kukivisha Chama cha Chadema ngozi ya kondoo wakati ni mbwa mwitu wa kali!!!! Hivi kweli badala ya kulaani kilichofanywa na Rwakatare eti hapa mashabiki wanajitokeza na kujaribu kupotosha ukweli kwa kisingizio cha matumizi ya technolojia.....nasema huu ni uhuni wa ajabu...kwa huu unyama Chadema hamtoki...ni bora mtuambie ukweli kwanini mnapanga mauji wakati nyie ni Chama cha siasa?!!!
 
kama kweli amekamatwa kwa sababu ya hiyo video, ukombozi ukombozi ukomboziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii umefika Tanzania. Dr slaa
 
Hata Lusinde alikuwa atukani ni Techolojia tu ile.

Inanikumbusha John Terry wa Chelsea alimtakana mchezaji mwenzake uwanjani Lips zake tu zikamtia hatiani.

Vipi Lips za Rwakatare ukizima sauti bado unaona anachokisema.

Chadema mtaangaika sana.
 
Josephine Mshumbusi ni mjuzi katika IT karibu hapa utupe mtazamo wako katika hili. naipenda CHADEMA na nchi yangu hili lilinifanya jana nikose raha mbele ya mashabiki wa CCM, ilinifanya kuacha kazi zote na kuanza uchunguzi. Siasa yetu imefika kiwango kibaya na hizi ni dalili za Mwisho za utawala kuanguka. Mungu alishaibariki Tanzania na CHADEMA PIA. wataumbuka tu twende mahakamani muone.
 
Tunachezeana michezo ya kitoto sana na ndo maana unaona kundi kubwa la wanaccm walijifanya Manabii wa kutabiri anguko la cdm, kumbe walishaidhinisha uandaliwaji wa hii movie, kumbuka kuwa wanawatu wao nje wanaoweza kuwajulisha hali ya technologia huko nje na hivyo kutumia utaratibu kama huu kuchafua hali ya kisiasa nchini. 2015 tutaelewana tu.

Acha kabisa kudanganya watoto. Lip syncing ni kweli ipo. Lakini inatumia sauti na maneno ya msemaji. Lip syncing haitengenezi sauti. Tatizo lenu Chadema mnalazimisha kuingia Ikulu sana, hadi mnatutisha. Sasa ule mkakati wa nchi haitawaliki ndio umefikia huku?

Nilisema mwanzoni kabisa mwa hii ishu. GODBLESS LEMA NA FREEMAN MBOWE WANAJUA KILICHOMTOKEA KIBANDA.

Na bado. Mtavuliwa nguo tu mwaka huu. Na nyie mashabiki wa Chadema msikubali kutumiwa tu kizembe zembe.
 
Kufuatia suala la Lwakatare kushika kasi humu jamvini, zimetokea hisia na mawazo tofauti sana baina ya wachangiaji mbalimbali juu ya mada hii ya kurecordiwa Lwakatare kupanga kumdhuru mwandishi. Wengi tulihoji sana uwezekano wa hii ishu kama ni halisi/si halisi. Kutokana na kuwa gizani kitechnologia, wengi hadi ninavyoongea hivi bado huwezi kuwabadilisha mawazo kuwa technolojia inaweza ikahusika katika kufake ile clip. Na kutokana na suala hili kugubikwa na propaganda za kisiasa, watu wamesahau hata technologia rahiti tu ya kuifanya midomo ya Cartoon icheze kulingana na maneno yanayotamkwa na cartoon/robot.

Kuweka kumbukumbu vizuri tarehe za mwanzon kabisa za mwaka huu mpya Mwigulu Nchemba alitueleza kuwa alikuwa na mkanda unaoonyesha viongoz (wengi) wa chadema kupanga mauaji. Mkanda umetoka tumeona kiongozi mmoja tu ndo anayepanga mauaji, kupungua kwa washiriki kutoka kwa viongoz hadi kiongozi, inahusishwa na ugumu uliopo wa kuinvolve watu wengi kwenye kufake/kulisha maneno watu wengi kwenye clip moja.

Aidha, baada ya tukio la utekwaji wa kibanda, wameibuka Nape na Ridhiwani hadharani na kuongea wakiwa na confinence ya 100% kuwa ''hawa wenzetu wa upinzani''/na ''safari hii pia mseme kuwa Ikulu/Rama/Magogoni ndio wanaohusika, kazi iliyopaswa kufanywa na vyombo vya dola. Siku chache baadaye Single ya Lwakatale ikatambulishwa rasmi kupitia Youtube na immediately ikatua jamvini na hata Polisi kuipata habari hii via Jamvini/Youtube na sio kwa Mwigulu. Sasa ukiconnect dots.......unaruhusiwa kabisa kufikiri kuwa tayari wenzetu wa upande wa pili walisha preview hii clip waliyoshiriki kuiandaa na ndo mana walikuwa na uhakika kuwa kwa level yetu ta technology, ni rahisi sana kushawishika kwa hii clip kuwa ni halisi.

Tulishasikia pia Wassira akitamka kuwa CDM lazima ife 2013, wengi hatukuelewa na hadi sasa hatujaelewa alikuwa anamaana gani kutamka maneno kama yale mtu wa makamo yulo. Sasa kauli za hivi za kumtamkia kifo mwenzio zinasignal kuwepo kwa mkakati wa maksudi wa kumuua mwenzio??Aidha, CCM katika vikao vyao vya CC/NEC, ccm walijadili kwa kina namna ya kudeal/kuisambaratisha CDM badala ya namna ya kutumikia umma wa watanzania waliowaweka madarakani. Hapa pia panazaa jambo.

Baada ya utanguliz huu naomba niimwage kwenu faked clip ya Barack Obama ili at least tujue tu kuwa suala la kulishwa maneno linawezekana. BOFYA A Bad Lip Reading of Barack Obama's Inauguration (Legendado PT-BR) - YouTube. Aidha, clip hii isikuzuie kuendelea kuamini unachokiamini, mimi nimeonelea tu niwafahamishe wale wote wenzangu ambao asubuh ya leo tulihisi sio kitu kinachowezekana hapa duniani.

Penye red: Hapo ndipo polisi lazima wajiulize, kama kweli hawafanyi kazi kimashine na kuendeshwa na makada wa CCM na siyo kupitia taaluma zao.

Pili sitashangaa iwapo usalama wa taifa imehusika katika utayarishaji wa kitu hiki. Mahakamani haitasimama kamwe, lakini ki-propaganda kwa wananchi walio wengi inaweza ikawa effective.
 
sitaki kuamini kuwa haya mazungumzo yana ukweli coz inaonekana yamefanyika sehemu yenye watu wengi. Hata kama ni kazi basi angepewa kiongozi wa kazi halafu yeye awape wenzie lakini hapa nasikia kina Rich wanasalimiwa SASA ADABU YA KAZI IKO WAPI? AU WALIKUWA BAR
 
Hata Lusinde alikuwa atukani ni Techolojia tu ile.

Inanikumbusha John Terry wa Chelsea alimtakana mchezaji mwenzake uwanjani Lips zake tu zikamtia hatiani.

Vipi Lips za Rwakatare ukizima sauti bado unaona anachokisema.

Chadema mtaangaika sana.

Wewe Riz wacha hizo. Wananchi waliwasikia akina lusinde live majukwaani, na siyo kupitia mikanda iliyotayarishwa na usalama wa taifa! Please shut up!
 
nilikuwa nataka kuja na hoja kama yako, angalia midomo ya rwakatare wakati anaongea, jamani hapa hakuna uhalisia kabisa, ni kama maneno anafaanya kuyafwatisha kwa kumung'unya ila hayatoki kwa midogo yake!! alafu huyu mtu anayeelekezwa inakuwaje mwanzo mwisho yeye ni ehe ehe ehe hana hata la kuchangia??

Tukitaka kujua video ya kutungwa tumsome mtu wa pili anayepewa maelekezo.
 
Wanasheria toeni ushauri wenu. Sheria inasemaje kuhusu kushitakiwa kwa jeshi la polisi kwa ajili ya mauaji na ugaidi wanaoufanya na kisha kuwafanya wa Tanzania wajinga nasana?

CDM haitakufa kwa sababu ina watu wengi wanaoelewa na wenye uwezo wa kutambua hofu na mikakati inayofanywa na serikali ya ccm.
 
Sasa na sisi chadema tutengeneze za matukio ya ccm halafu wafanye kazi ya kukanusha na wao...
 
Naapa chini ya Mbingu na Ardhi kamwe Shetani hatamshinda Mungu.

Kama Daudi alimuua Goliathi kwa jiwe katu Mashetani hawa wanaotaka kuichafua Chadema hawatafanikiwa na wataangamia.

Naapa kwa Mungu aliye hai yeyote aliyeshiriki kutunga mpango huu mchafu hatabaki salama.

Naapa kwa Mungu Mkuu muumba kila kitu kwamba kila aliyeshiriki kutunga uchafu huu lazima ataumbuka siku si nyingi na ataiomva radhi hadharani.

Naapa kwa Mungu aliyemwangamiza Anania akapasuka matumbo mbele ya madhabahu kwamba wahalifu hawa watafuata njia hiyo hiyo.

Naapa kwa Mungu aliyemwangamiza Herode akadondoka juu ya kiti cha kifalme na mwili wake kuliwa na siafu kwamba waovu waliotunga mbinu hii watafuata njia hiyo hiyo.

Naapa kwa Mungu wa Abraham,Isaka na Yakobo kwamba watu hawa hawataweza kuendelea kuharibu Taifa letu kwa uchochezi wao bali watakipata sawasawa kile kiwapatacho watu wasiomjua Mungu.

Naapa kwa Mungu ambaye jina lake ni NIKO AMBAYE NIKO kwamba Shetani kamwe hatajitwalia utukufu.

Wao wana Baali na Chadema wana Mungu kamwe Baali hawezi kumshinda Mungu.

Mkuu Molemo pole sana naona umeguswa kweli na hii habari yaani umekaribia kuimaliza Biblia yote, nadhani wakati unaandika Roho Mtakatifu alikushukia na ukanena kwa lugha!

Poleni. Juzi mmewashughulikia Msalia leo linaibuka hili sijui mtamshughulikia nani!

 
Last edited by a moderator:
Ni kweli mkuu aliye-record amechemka. Kwa mtu asiyefikiri vizuri ndo ataamini upuuzi huu. Kama kweli ni Great thinker utang'amua video ilivyo na makosa mengi ya kiufundi na kudhihirisha kuwa ni uwongo.

Ni vyema waandaaji wakajipanga kwa zile part wanazosema eti watazileta.

Mungu ni mwema sana na siku zote huwaumbua watu wenye nia mbaya. Hizi ni siasa za maji taka ambazo hazina tija na upepo utawapitia tu hata kama watatengeneza video mia moja na zaidi. Propaganda hizi ni za kitoto.

CCM na serikali yake wanapoteza muda badala ya kufikiri watawasaidiaje watanzania kuondokana na umaskini. Ni vigumu kuwadanganya na kuwaaminisha watanzania kwa video hii.

CHADEMA mtihani huu mtaushinda tu, mungu yuko nanyi na atawatia nguvu kuendelea na harakati za ukombozi.

CCM na Serikali yenu, endeleeni na hizi Katuni zenu na uharamia wenu mwingi. Lakini mjue kwamba "there is no evil plan which is free from mistkes'. Mtazidi kuumbuka na mwisho wake matokeo yake takuwa juu ya vichwa vyenu.
 
Mkuu patriote,
mi naamini ni yeye lwakatare, isipokuwa amechezewa mtego na anaowaamini. Mambo haya ya kutafutana na kuwindana kujua nani mbaya na nani adui wa chama ni ya kawaida kwenye siasa na hata kwenye biashara kubwa..

Kilichomtokea Lwakatare ni imani kupita kiasi kwa vijana wake wa upelelezi. Haonekani kuzungumzia mauaji wala kupiga mtu lakini inavyoônyesha alitaka kumtisha huyo adui yake. Walichokifanya watu wake ni kumchokoza tu nae akaingia mkenge kwa kudhani ni ishu ya kawaida ya mazungumzo ya kirafiki.

kudeal na Ccm ni kudeal na wakubwa, kwa ukuaji wa Chadema wa spidi ya namna hii Ccm wako radhi kutoa pesa yoyote wapate information za kukivuruga chama. Hawa vijana wamemuuza Rwakatare kwa vipande vya fedha.

lakini pia kwa kuisikiliza clip hii ni wazi Rwakatare hajui chochote kuhusiana na masuala ya utekaji au mauaji., nasema hivyo kwa sababu hajuihata dawa za usingizi au spray zinauzwaje, nadhani ndo kwanza anajifunza. Pili hakuwatuma kuua bali kumteka kwa lengo la kumtisha. Hatahivyo muda utatupa picha kamili

Mkuu hapo umenena.

Hapo kwenye wekundu inaweza kuwa sawa ila tindikali anaijua!

 
Hao jamaa wamechemsha ile mbaya,hozo pesa wanazotumia kuandaa huo ujinga kwanini wasipeleke kwa watu wenye mahitaji kuliko kujidharirisha kwa kuandaa vitu vilivyokosa quality kabisa.

Waongeze bajeti wizara ya elimu
 
All in all..., hii nchi tumefika ambapo sipo.., watu waanze kutupwa ndani na tuache utani kwenye mambo serious.., uchunguzi ufanyike, ikigundulika kwamba watu walipanga mauaji, waliua au walisingizia wenzao (kugushi) basi wawekwe ndani huu sasa ushakuwa zaidi ya upuuzi (siasa mpaka kwenye maisha ya watu)

tabu moja hata upande ccm ukishindwa utaona tu kimya kinatawala, hakuna hatua itakayochukuliwa, ila kama inahusu upinzani na ikawa kweli au ya kutengenezwa utashuhudia hiyo heke heka ya polisi, uwt, wanasheria n.k lakini ifike mahali ccm waone aibu, kupika kitu ambacho si halisi mtu mzima mi huwa naona ni jambo la aibu sana, hawaonei aibu watoto wao wala raia kwa sababu dhamira zao ni mfu, wala hawajitambui tena, kisa wasitoke madarakani. kuna siku tutashuhudia wakijipaka mavi, kwa kuamini ni dawa ya kuwafanya wabaki madarakani, tunangoja tu tujionee vituko kadri siku zinavyokwenda
 
Sasa na sisi chadema tutengeneze za matukio ya ccm halafu wafanye kazi ya kukanusha na wao...
Mkuu wangu Crashwise naunga mkono hoja! Tena u know wht buddy, anzeni na video ile ile ya Lwakatare na sasa tumuone ni Wassira au Nchemba wakitoa hayo maagizo!! Kila kitu, including sauti viwe exactly the same! For how long should I wait for the video SIR?
 
Back
Top Bottom