KASHFA: Polisi wa Buguruni Dar, wadaiwa kudhulumu kilo 800 za nyama na kugawana

Dah, hao dawa yao mbon ni ndogo sana.!
Unajifanya unaendelea na utaratibu wako tena unawataarifu kabisa kwamba mm mtaji ninao mkubwa kesho naenda kuandaa Nyama nyingi zaidi.
Kwa hasira zao za kipumbafu watakufuatilia tena, na hapo ndo itakua mwisho wao wa kuliona Jua.

Nyama yote unatia sumu hatari ambayo ukila huombi hata maji ya kunywa.

Inaumiza sana hawa dogs.
asa si naww watakuua tu
 
Huyo msajili wa bodi ya nyama anaitwa Imani Sichalwe, namfahamu vizuri sana alikuwa mwalimu wangu chuo cha mifugo Tengeru, kwa kweli alikuwa katili tangu akiwa chuoni hapo, uliza mwananchi yeyote aliyepitia pale LITI TENGERU miaka ya 2000 na kadhaa atakupa habari! Ajirekebishe bwana gentleman kabisa unakuwa mpuuzi namna hiyo? Ni mtu anayeamini katika mabavu! Nafasi yenyewe kwanza kaipata kwa kubebwa, dadake alikuwa mkurugenzi hapo wizara ya mifugo ndiye aliyemmegea pande hilo!
Hata kama huyo Imma wenu ni katili lakini ifike wakati uchafu uliopo Vingunguti ukomeshwe> Imma hana dada aliyewahi kuwa mkurugenzi
 
Duuh makachero wamepotea na utumbo wa taulo na utumbo wa kitabu.Kweli alosto ya nyama sio mchezo.Mishahara iongezwe ndio suluhu.
 
Sote tunakubaliana kitendo kikichofanywa na askari hao ni cha kupingwa kwa nguvu zote.
Lakini pia ndugu zangu makosa ya askari wachache wasio na maadili hayalifanyi jeshi la polisi kuwa taasisi isiyo na maana (useless) ktk Nchi hii.

Tumekuwa na tabia ya kuliponda jeshi la polisi(kupitiliza)pale linapoibuka jambo lisilo la haki, ni kama vile tunaona polisi wote ni Wezi, wala rushwa, wauaji nk, sio sawa hilo.
Watu wapuuzi wapo ktk kila taasisi lakini haimaanishi taasisi husika ina nia ovu kama itendwavyo na wapuuzi wachache.

Jaribu kufikiria Kusiwepo na jeshi la polisi kwa mwezi mmoja tu uone Kama hata hiyo simu unayotumia kupost hapa Utathubutu kuitumia mchana.Tukemee wale wachache Tuache kulitukana jeshi na kuona halina faida.

Kwa upande wa Mayor amekosa cooperative management /leaderahip. Mayor na polisi wote ni serikali wanatawala kwa pamoja.
Naamini angeweza kulishughulikia jambo hili kwa mawasiliano na RPC ama IGP na likamalizwa kwa haki kabisa,kuliko kuliweka mbele ya camera na matamko yasiyo na tija.

Binafsi sijaona busara ya kiongozi kuweka nguvu kubwa ktk kuonesha umma changamoto zilizo ndani ya jeshi la polisi.Raia tukishachukia polisi itafaa nini ktk ustawi wa Nchi?
 
Wafanyabiashara wa nyama za mafungu huko Vingunguti wamelalamikia kitendo cha Bodi ya nyama kukamata nyama zao na kuzipeleka kituo cha polisi Buguruni ambako badala ya kuiteketeza waligawana na kubakiza makongoro.

Akiongea katika eneo la tukio Meya wa Jiji la Dar es Salaam mh. Kumbilamoto alisema Bodi ya Nyama ilipaswa kuvuta subira kwani eneo la kuuzia nyama ujenzi wake bado haujakamilika.

Naye Kamanda wa polisi kituo cha Buguruni amekana askari wake kugawana nyama akisema haiingii akilini eti askari wagawane nyama iliyotakiwa kuteketezwa ambayo huenda ina kimeta.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

=====

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yalaani kitendo walichofanyiwa wafanyabiashara wa nyama Vingunguti.
img-20210315-wa0001.jpg


Halmashaur ya Jiji la Dar es Salaam imelaani kitendo kilichofanywa na Bodi ya Nyama kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Buguruni kuvamia wafanyabiashara ya machinjio ya Vingunguti na kuchukua nyama zao kwa madai ya kutokidhi vigezo vya kisheria kwa Afya ya mlaji.
img-20210315-wa0001.jpg

Akizungumza na wafanyabiashara wa machinjio hiyo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto amesema kuwa kitendo hicho si cha kiungwana kwani hakuna kiongozi yoyote waliemshirikisha katika oparesheni hiyo.

Amesema kuwa, bodi ya nyama walivamia machinjio hayo na kusema uwongo katika vyombo vya habari kwa wafanyabiashara hao wamekaidi kwenda eneo maalum ambalo wametengewa na Halmashaur ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili kuuza biashara zao jambo ambalo si kweli kwani eneo lililotengwa bado halijakamilika.
20210315_113533.jpg

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara wa Nyama na mazao yake, Joel Meshark amesema kuwa kitendo hicho si cha kiungwana hata kidogo kwani waliondoka na nyama hizo kwa madai ya nyama hizo ni vibudu.

“Walikuja kuchukua nyama na kuondoka nazo kwenda nazo Polisi Buguruni na kudai wamekwenda kuziteketeza lakini hakuna ukweli wowote kwani walichoma makongoro na hakuna nyama yoyote iliyoonekana”amesema Meshark.

Naye Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Segerea, Ruta amesema kuwa, Mbunge wa Jimbo hilo, amewataka wafanyabiashara hao kupitia mwanasheria wao wafike ofisi ya Mbunge kwa ajili ya taratibu ya kwenda kufungua kesi ili haki yao ipatikane.

Aidha amesema, amesekitishwa sana na kitendo hicho kwani lengo lao lilikua ni kuwachonganisha wananchi na Serikali yao, hivyo ofisi ya Mbunge haitalifumbia macho jambo hilo.

Jackson Matutu Miongoni mwa wafanyabiashara hao amesema kuwa, alipokonywa nyama yake na viongozi wa bodi kwa madai nyama yake haikua katika mazingira mazuri hivyo wakamtaka alipe faini shilling laki moja, lakini baada ya kulipa alifukuzwa nje kama jambazi na hakuna chochote alichokipata.


“Nyama yangu ilikua kwenye chombo nilifika pale kwa ajili ya kuipeleka sehemu inayohusika lakini Jeshi la Polisi Buguruni kwa kushirikiana na Bodi ya nyama waliichukua nyama yangu na kuondoka nayo, walidanya wameichoma Moto ila nimeshuhudia wakigawanyana pale Polisi”amesema Matutu.
View attachment 1726931
Askari kwa sasa hivi wana njaa sana.
Walimuweka meko ila na wao wamepigika sana mpka wanaanza kuiba nyama za wananchi.
Wananchi hawana pesa ya kutoa rushwa.

Kiufupi mishahara ya askari haiwatoshi wanaishi kwa wizi rushwa kubambikia watu makosa etc.


Wananchi hawana pesa ukidai rushwa hana pesa anakupa buku 2
Wakome!
 
Nchi za ulaya wanatushangaa sana wanaposikia 'Polisi wamedhulumu Nyama' huenda hata huwa wana hamu waje watupasue ubongo ili wafanye ugunduzi kwenye mafuvu yetu ya viumbe hafifu wa "Homopolisiensis tanzaninses" huenda ndio tukafanywa kuwa the living missing link.
 
Asante mkuu twende Polepole!
Sawa, endelea kwwenda polepole peke yako, si na mimi. maana eleimu yako ndogo tu ya Tengeru tayari ushajua wakurugenzi wote na nmna makaimu wanavyoteuliwa kwa kubebwa. Endelea na mwendo wako.
 
Back
Top Bottom