KASHFA: Polisi wa Buguruni Dar, wadaiwa kudhulumu kilo 800 za nyama na kugawana

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Mkoa wa Dar es Salaam, Adrew Majaliwa amezuia operesheni zote zinazofanywa na Bodi ya Nyama Tanzania kwa wafanyabiashara wa machinjio ya Vingunguti wanaouza nje ya machinjio pamoja na wasiokuwa na vifungashio maalumu vya kubebea.

Hatua hiyo imekuja baada ya wafanyabiashara hao kuilalamikia Bodi ya Nyama wakidai kuwa imechukua nyama zaidi ya kilo 600 na kuzipeleka katika kituo cha polisi cha Buguruni ambako pia wamedai polisi wa kituo hicho wamegawana nyama hizo.

Akizungumza hayo leo Jumatatu Machi 15 alipokuwa kwenye mkutano wa wafanyabiashara hao, Majaliwa amesema operesheni ya kuwakamata wafanyabiashara wanaouza nje ya machinjio hayo na wasiokuwa na vifungashio maalumu amesitisha hadi eneo lililotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao litakapokamilika.

Majaliwa ameiagiza bodi ya nyama waende kwenye machinjio hayo kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao jinsi ya kuhifadhi nyama hizo kwenye vifaa maalumu wanavyotakiwa kuwa navyo.
"Bodi ya nyama mnatakiwa kutoa elimu ili wafanyabiashara wajue vifaa gani vya kuhifadhia nyama hizo na vizimba 29 vya wauza nyama vinajengwa ambavyo vitakamilika baada ya miezi mitatu hivyo miezi hiyo ikiisha operesheni hivyo ifanyike,"amesema amajaliwa.

Hata hivyo, Mkuu wa Kituo cha Polisi Buguruni, Adamu Maro amekana polisi kugawana nyama hiyo, bali walichofanya ni operesheni baada ya kupewa taarifa kuwa kuna nyama ambazo ni kibudu zisiingizwa kwenye machinjio hayo

"Sisi tulifanya operesheni baada ya kupewa rasmi barua kuwa kuna nyama ya kibudu imeingizwa machinjioni haiwezekani polisi akachukua nyama ambayo haifai kuliwa,” amesema Maro
Naye Meya wa jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto amesema mkurugenzi wa jiji, mkuu wa wilaya, mtendaji wa kata na mwenyekiti wa mtaa huo hawakupewa taarifa kama kuna operesheni ya kuwakamata wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya machinjio hayo pamoja na wasiokuwa na vifungashio vya kuhifadhia nyama hizo.

MWANANCHI
 
Nimesikitishwa na taarifa ya kitendo cha uporaji wa nyama kule vingnguti.Ila nikaanza kujiuliza majukumu ya board ya nyama yanatofautiana vipi na majukumu ya afisa afya wa halmashauri.kwanini issue kama ya ubora wa nyama yasishughulikiwe na mamraka ya chakula na dawa au TBS kupia ofisi ya afya za Halmashauri.Najiuliza tuu kule lukuledi hawa board ya nyama wanafikaje kucheki ubora wa nyama.

Ni wakati muafaka sasa kuchunguza majukumu na uhitaji wa serikali kuwa na hii board kama seperate entity.Ili kupunguza gharama na kuleta ufanisi inawezekana majukumu yake yakaingizwa kwenye idara moja ya halmashuri lets say idara ya uvuvi na mifugo.Maana ndiyo nimeisikia leo hii board ya nyama kwa kweli. Sometimes wanakuwa hawana cha kufanya hata kufikia kufanya vituko kama hivi vya kiharifu.
 
Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Mkoa wa Dar es Salaam, Adrew Majaliwa amezuia operesheni zote zinazofanywa na Bodi ya Nyama Tanzania kwa wafanyabiashara wa machinjio ya Vingunguti wanaouza nje ya machinjio pamoja na wasiokuwa na vifungashio maalumu vya kubebea....
Polisi njaa sana....wamechoma MAKWASUKWASU kisha nyama wametambaa nayo.
 
Uonevu ..uonevu..uonevu...uroho na tamaa ya kupenda vya bure.... Uaskari ni kama kazi iliyolaaniwa... IGP na RPC tunangoja kusikia toka kwenu
Hapo kwenye kupenda vya bure u nailed it mkuu mshana yaani police wanapenda kitonga sijapata kuona, nina mshkaji wangu alikuwa njagu now ameacha ameingia kwenyw field nyingine lkn tabia hiyo hajaacha yaani qnagongea bia hadi wewe uliyenae unajisikia vibaya....hapo anqtereza kwako bado qnag8ngeq biq upande wa tatu kule....dah sijui ni moja ya somo lao huko chuo chao maana kama ni somo walahi wanalitendea haki!!!
 
hiki ni kituko cha mwaka kilo 800 watu wamesepa nayo doh 🤣🤣🤣
njaa hizi hawa watu ni zaidi ya mbwa mwitu yani kilo 800 yote saluti kwao
 
sijawi ona polis wapumbavu kama watz,sitosahau mwaka 2015 kwenye vulugu za uchaguz kiwira mbeya polis wilingia mgahawan kwa mama moja iv walikula msos wote kimabavu af wakaondoka bla kulipa,walienda kwa mzee mmoja walibaka mke na mabint zake mbele yake nilisikitika sana
wewe ulikwepo kushuhudia yote hayo?
 
Back
Top Bottom