KASHFA: Polisi wa Buguruni Dar, wadaiwa kudhulumu kilo 800 za nyama na kugawana

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
42,889
2,000
Wafanyabiashara wa nyama za mafungu huko Vingunguti wamelalamikia kitendo cha Bodi ya nyama kukamata nyama zao na kuzipeleka kituo cha polisi Buguruni ambako badala ya kuiteketeza waligawana na kubakiza makongoro.

Akiongea katika eneo la tukio Meya wa Jiji la Dar es Salaam mh. Kumbilamoto alisema Bodi ya Nyama ilipaswa kuvuta subira kwani eneo la kuuzia nyama ujenzi wake bado haujakamilika.

Naye Kamanda wa polisi kituo cha Buguruni amekana askari wake kugawana nyama akisema haiingii akilini eti askari wagawane nyama iliyotakiwa kuteketezwa ambayo huenda ina kimeta.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

=====

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yalaani kitendo walichofanyiwa wafanyabiashara wa nyama Vingunguti.
img-20210315-wa0001.jpg

Halmashaur ya Jiji la Dar es Salaam imelaani kitendo kilichofanywa na Bodi ya Nyama kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Buguruni kuvamia wafanyabiashara ya machinjio ya Vingunguti na kuchukua nyama zao kwa madai ya kutokidhi vigezo vya kisheria kwa Afya ya mlaji.
img-20210315-wa0001.jpg

Akizungumza na wafanyabiashara wa machinjio hiyo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto amesema kuwa kitendo hicho si cha kiungwana kwani hakuna kiongozi yoyote waliemshirikisha katika oparesheni hiyo.

Amesema kuwa, bodi ya nyama walivamia machinjio hayo na kusema uwongo katika vyombo vya habari kwa wafanyabiashara hao wamekaidi kwenda eneo maalum ambalo wametengewa na Halmashaur ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili kuuza biashara zao jambo ambalo si kweli kwani eneo lililotengwa bado halijakamilika.
20210315_113533.jpg

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara wa Nyama na mazao yake, Joel Meshark amesema kuwa kitendo hicho si cha kiungwana hata kidogo kwani waliondoka na nyama hizo kwa madai ya nyama hizo ni vibudu.

“Walikuja kuchukua nyama na kuondoka nazo kwenda nazo Polisi Buguruni na kudai wamekwenda kuziteketeza lakini hakuna ukweli wowote kwani walichoma makongoro na hakuna nyama yoyote iliyoonekana”amesema Meshark.

Naye Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Segerea, Ruta amesema kuwa, Mbunge wa Jimbo hilo, amewataka wafanyabiashara hao kupitia mwanasheria wao wafike ofisi ya Mbunge kwa ajili ya taratibu ya kwenda kufungua kesi ili haki yao ipatikane.

Aidha amesema, amesekitishwa sana na kitendo hicho kwani lengo lao lilikua ni kuwachonganisha wananchi na Serikali yao, hivyo ofisi ya Mbunge haitalifumbia macho jambo hilo.

Jackson Matutu Miongoni mwa wafanyabiashara hao amesema kuwa, alipokonywa nyama yake na viongozi wa bodi kwa madai nyama yake haikua katika mazingira mazuri hivyo wakamtaka alipe faini shilling laki moja, lakini baada ya kulipa alifukuzwa nje kama jambazi na hakuna chochote alichokipata.

“Nyama yangu ilikua kwenye chombo nilifika pale kwa ajili ya kuipeleka sehemu inayohusika lakini Jeshi la Polisi Buguruni kwa kushirikiana na Bodi ya nyama waliichukua nyama yangu na kuondoka nayo, walidanya wameichoma Moto ila nimeshuhudia wakigawanyana pale Polisi”amesema Matutu.
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,781
2,000
Hii nchi ni ya ajabu sana. Tuliowaamini kusimamia sheria wamekuwa vibaka.

Wafanyabiashara wanasema polisi wamegawana nyama walizonyanganywa.

Mkuu wa kituo anasema askari hawawezi kuchukua nyama. Ziko wapi? /wanaonyesha makongoro mawili. Hivi huyu anafaa kuwa kiongozi kweli?? Tumuamini nani?

Kama hata polisi hawaaminiki tena?
 
babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
7,374

Huyo Bois wao ndio kimeta hapo,hao polisi buguruni ndo zao hizo.
Kuna siku sitasahau nimetoka mzigo usiku nataka nikaongee na maza Gongolamboto ili kesho nitokee huko kwenda job sa tano usiku nasubiri daladala hapo buguruni sokoni.
Jamaa hawa hapa wana kundi vibaka km 20 hivi.mzee mi niko busy napungia DCM zisimame aaah wakaniwai we unafanyaje hapa.
Nawaambia nasubiri usafiri aaah wapi we mzururaji nikafungua shati twende kituoni
Hapo wana Bunduki, mapanga, virungu, pisto
Dah,kufika kituoni na wale vibaka tukasachiwa
Nikakutwa nna laki na 80 hivi sasa ndo jamaa wakaanza urafiki.
Natolewa lockap, narudishwa wananambia "sasa we una hela zote hizi unakubali kulala humu?
Kha mi si nilisema sio mzururaji nimetoka kazi naenda home 🤔.
Wakanipora buku 60 wananambia ondoka haraka sana.
Dah,mpaka nafika Goms sa 12 asb maza ananiuliza we ulikua wapi unakuja likwili namna hii,namwambia selo haamini,
Ww umelazwa selo kosa gani?
Kumpa kisa chote
Hapo maza ndo huwa na machungu sana.
Yani alitaka hata tuwaibukie mda huo huo,(ni mjeshi wa zamani)
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
27,723

Shukuru Mungu hukuuwawa halafu maiti yako ingebambikiwa smg yenye kutu na maelezo ya Gaidi sugu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom