Mufindi: Afungwa Jela miaka 20 kwa kukutwa na kilo 32 za nyama ya Tandala

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemhukumu Mbogo Tinda (45), Mkazi wa Kijiji cha Ihoanza Tarafa ya Malangali, wilayani hapa, kutumia kifungo cha miaka 20 gerezani, baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili.

Makosa hayo ni lile la kukutwa na nyara za Serikali (nyama ya Tandala – Kudu, yenye uzito wa kilo 32), lakini pia kujihusisha nyara za Serikali bila kuwa na kibali.

Hukumu hiyo imetolewa jana September 4, 2023; na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Benedict Nkomola, ambapo imedaiwa mshtakiwa huyo alipatikana na nyama ya Tandala yenye thamani ya Sh7, 859, 136 milioni.

Akisoma shtaka hilo, hakimu huyo amesema mnamo August 26, 2023 katika Kijiji cha Idope, Kata ya Ihoanza, wilayani hapa, mshtakiwa huyo alikutwa na nyama ya Tandala ambayo alikuwa anaiuza bila kuwa na uhalali wa kufanya shughuli hiyo.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa alinunua na kuuza nyama ya Tandala kilo 32, yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha ambayo ni mali Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na vibali au leseni ya kuuza nyama hiyo.

Pia hakimu huyo amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 86(1) (2) (a) na kifungu (3) cha sheria ya uhifadhi wa wanyapori sura 283 rejeo la Mwaka 2022, ikisomwa pamoja na aya ya 14 Jedwari la kwanza la vifungu vya 57(1), na 60 (1) (2) vya sheria ya makosa ya uhujumu uchumi na makosa ya kupangwa, sura 200 rejeo la Mwaka 2022.

Aidha katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 11, 2023; mshtakiwa alikiri kutenda makosa hayo, ndipo mahakama ikamtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kwanza na pili ambapo adhabu hizo zitaenda sambamba.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ahmad Magenda, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa.

"Niombe mahakama yako itoe adhabu kali kwa washtakiwa wote ambao wanafanya makosa kama haya ya kuhujumu wanyapori ambao ni vivutio kwa watalii, sanjari na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla," amesema Magenda.

MWANANCHI
 
Kesi za kipuuzi hizi, law society muwe mnatembea nchi nzima kuwasaidia bure watu wanaofungwa kwa upuuzi kama huu.

Wanyama ni viumbe tumepewa na Mungu bure kutumia kwa kotoweo.
Mbaya zaidi yeye hakuhusika na kuwinda bali naye alinunua/alilangua tu ili auze. Sheria za nchi za kiafrika (shit hole countries in accordance to Trump) ni kwa ajili ya walalahoi.
 
Anaewinda apate kitoweo anasekwa jela 20 years. Wauza bandari na mbuga zetu wanakenua tu wakiendelea kula na kodi zetu huku wakitembelea V8 na kujenga partments huku pia wakiendelea kusinzia na kujambiana bungeni wakipulizwa na AC kwa jasho la walalahoi.

Shenzistan, nchi ya ajabu sana hii.
 
Mkuu unaniumiza mno kwa maneno hayo. Ila naona mwanga mbele. Nchi hii itakombolewa siku moja.
 
Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemhukumu Mbogo Tinda (45), Mkazi wa Kijiji cha Ihoanza Tarafa ya Malangali, wilayani hapa, kutumia kifungo cha miaka 20 gerezani, baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili.

Makosa hayo ni lile la kukutwa na nyara za Serikali (nyama ya Tandala – Kudu, yenye uzito wa kilo 32), lakini pia kujihusisha nyara za Serikali bila kuwa na kibali.

Hukumu hiyo imetolewa jana September 4, 2023; na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Benedict Nkomola, ambapo imedaiwa mshtakiwa huyo alipatikana na nyama ya Tandala yenye thamani ya Sh7, 859, 136 milioni.

Akisoma shtaka hilo, hakimu huyo amesema mnamo August 26, 2023 katika Kijiji cha Idope, Kata ya Ihoanza, wilayani hapa, mshtakiwa huyo alikutwa na nyama ya Tandala ambayo alikuwa anaiuza bila kuwa na uhalali wa kufanya shughuli hiyo.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa alinunua na kuuza nyama ya Tandala kilo 32, yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha ambayo ni mali Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na vibali au leseni ya kuuza nyama hiyo.

Pia hakimu huyo amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 86(1) (2) (a) na kifungu (3) cha sheria ya uhifadhi wa wanyapori sura 283 rejeo la Mwaka 2022, ikisomwa pamoja na aya ya 14 Jedwari la kwanza la vifungu vya 57(1), na 60 (1) (2) vya sheria ya makosa ya uhujumu uchumi na makosa ya kupangwa, sura 200 rejeo la Mwaka 2022.

Aidha katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 11, 2023; mshtakiwa alikiri kutenda makosa hayo, ndipo mahakama ikamtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kwanza na pili ambapo adhabu hizo zitaenda sambamba.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ahmad Magenda, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa.

"Niombe mahakama yako itoe adhabu kali kwa washtakiwa wote ambao wanafanya makosa kama haya ya kuhujumu wanyapori ambao ni vivutio kwa watalii, sanjari na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla," amesema Magenda.

MWANANCHI
Huu ni uonezi kabisa,hukumu hizi mbona zinatolewa Kwa wazawa tu,kila siku wageni wanakamatwa na hizo nyara ila wanalipa faini,yaani Mwananchi mwenye mali yake anahukumiwa kiasi hiki..... Mahakimu na Mahakama huu Muhimili lazima ujitafakari sana katika kutekeleza haki
 
Picha ya tandala tafadhali, aliyemfungisha mtu miaka 20.
Kwa msaada wa Wikipedia
Tragelaphus_strepsiceros.jpg
 
Back
Top Bottom