TCCIA na TRIAS zanoa wafanyabiashara wa nyama, Bodi ya Nyama yajipanga kufungia mabucha yanayouza nyama hafifu

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
750
1,800
Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na Kilimo TCCIA, Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Shirika la TRIAS Tanzania wametoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa nyama katika jiji la Arusha ikiwa ni mpango wa kukuza mnyororo wa thamani katika sekta ya Nyama.

Akiongea katika warsha ya siku moja iliyowahusisha wadau wa Mnyororo wa thamani wa sekta ya Nyama jijini Arusha, afisa wa TCCIA, mkoani hapa, Charles Makoi alisema kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia wadau wa Nyama kulalamikia huduma isiyoridhisha inayotolewa kwenye mabucha ikiwemo Nyama isiyokidhi viwango na ubora unaohitajika.

"Tunachangamoto ya wafanyabiashara wetu wa Nyama kutofuata miongozo ya usalama wa chakula, miundo mbinu ya mabucha sio mizuri na ndio maana wafanyabiashara wa mahoteli wanalalamika na sisi kama chama cha wafanyabiashara tukaonelea ipo haja ya kutoa mafunzo haya."

Alisema kuwa kabla ya semina hiyo TCCIA ilifanya utafiti kwa kuwahoji wadau wa Nyama wapatao 325 kati ya watu 350 tuliokusudia na kubaini kuwa mabucha ya kawaida ndio yenye kuuza nyama hafifu.

Kwa upande wake mshauri wa mradi kutoka Shirika la Trias Tanzania, Neema Kimaro alisema kuwa Trias Tanzania ni shirika la kimaendeleo linalofanyakazi na nchi 15 duniani ikiwemo nchi za Afrika mashariki chini ya mradi wake wa husisha kwa maendeleo endelevu kupitia wadau wake, wakiwemo TCCIA Arusha.

Alisema utafiti wa nyama uliowezeshwa na Shirika hilo umepelekea kujua changamoto na fursa zilizopo katika sekta ya Nyama pamoja na kuboresha mnyororo wa thamani ya Nyama.

"Shirika la Trias Tanzania tunafanyakazi katika maeneo matatu ambayo ni ujasiliamali, Mazingira na masuala ua uhusishwaji."

Alisema katika utafili ukiofanywa Trias inapenda kuona zaidi uhusishwaji wa makundi mbalimbali unakuwepo katika mnyororo wa thamani wa nyama, pia wafanyabiashara wanafanyakazi zao katika mazingira rafiki, wanapata faida na kukuza biashara zao pamoja na masoko yanayofikika.

Alisema katika semina hiyo wadau walipendekeza mambo mbalimbali katika kuboresha mnyororo wa thamani ikiwemo matumizi ya teknolojia, usalama wa nyama pia kipengele cha ushirikishwaji wa wadau katika utungwaji wa sera za nyama.

Naye mwakilishi wa bodi ya Nyama Tanzania, kanda ya Kaskazini, Rose Kamundi aliwataka wafanyabiashara wa Nyama katika jiji la Arusha kizingatia sheria ya Nyama kwa kuuza nyama maeneo sahihi na yenye ubora unaohitajika kabla ya kumfikia mlaji.

Alisisitiza kwa wadau wa Nyama kuuza nyama bora iliyozingatia vigezo ikiwemo maeneo sahihi ambayo yameruhusiwa na bodi ya nyama kutoa huduma hiyo.

Alisema bodi ya Nyama ipo makini kuhakikisha usalama wa nyama kuanzia shambani hadi kwa mlaji na kwamba mabucha yasiyokidhi vigezo vya usajili yanafungiwa.
 
Back
Top Bottom