Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,815
- 4,565
Bodi ya Sukari kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewanasa watu sita ambao ni Wafanyabiashara kwa kushindwa kuzingatia Bei Elekezi ya Sukari kama ilivyotangazwa na Serikali.
Watuhumiwa hao Sita wamekamatwa kufuatia Msako mkali iliyofanyika Jijini Dar es Salaam kwenye maeneo tofauti kwa lengo la Kubaini Wafanyabiashara wanaouza Sukari kinyume na Bei iliyopendekezwa.
Bahati Hakimu ni Meneja wa Ufuatiliaji, Ukaguzi na Uthibitishaji kutoka Bodi ya Sukari ambapo amesema Oparesheni za kuwafichua Wafanyabiashara Wadanganyifu itaendelea kufanyika kwenye maeneo yote ya Mkoa wa Dar es Salaam.
"Tutaendelea kufanya msako mkali tukishirikiana na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kuwa Bidhaa hiyo muhimu 'Sukari' inawafikia wananchi kwa Bei Pendekezwa, kwa Sababu Serikali imeruhusi Sukari kuingia nchini na imeondoa kodi na kurahisisha uingiaji wake hapa nchini ili watanzania wanufaike" amesema Bahati.
Pia soma:
- Serikali yatangaza Amri ya Bei Elekezi za Sukari Tanzania Bara