Fundi Mchundo, hapa naona unalea udini tu. Unataka tumbague huyu mama kwa sababu ya dini yake, hii si haki hata kidogo. Kusilimu au kuritadi hayo ni maamuzi binafsi ya mtu kuendana na imani ambayo ameona imemshawishi akakubaliana nayo. Sisi tunachagua mgombea mmoja kati ya kadhaa waliojitokeza kutokana na watakvyotushawishi kwa sera, si kwa dini.
Hilo unalolisema la Zanzibar kutokuwa na wabunge wakristu, angalia demographic structure ya Zanzibar kwanza kabla hujaleta madai hayo. Mbona Peramiho, Moshi vijijini, Rombo, na Biharamulo hakujawahi kuwa na mbunge mwislamu tangu uhuru, huu nao ni udini? Ni hesabu rahisi tu za probability kuwa chance za kumpata mbunge zinategemea na chance kuwa atajitokeza kugombea, na kama watu wa kundi lake wapo 2 kati ya 100 ni kwamba chance za kujitokeza mgombea wa kundi hilo ni 2%. Kipi cha ajabu hapo.
Tuache udini hapa, tujadili jinsi huyu mama anavyofaa au asivyofaa kwa mujibu wa kile anachotaka kutushawishi kuwa atakifanya Arusha, kisha tufanye uamuzi wetu siku ya uchaguzi kwa msingi wa hoja za kisiasa na si za kidini.