Kampeni ya Ubunge Arusha Mjini - Batilda Burian Vs Lema

Kampeni ya Ubunge Arusha Mjini - Batilda Burian Vs Lema

KATI YA BATILDA NA LEMA YUPI ATIBUKA KIDEDEA?


  • Total voters
    52
Best ukiona video ya Mwl Nyerere leo kwenye tv utasema amefufuka? Kama ilikuwa live basi sawa lakini kama ni maktaba, waweza oneshwa hata ile alipokuwa akigraduate degree yake ya kwanza!
 
Hata misupu ameweka hewani, Hakuna cha marekani wala wapi. Dr Batilda izi in Dar, na sioni mimba yoyote...

MICHUZI
 
nimesoma heading ya hii thread nikafikiria mambo mengineeeeeeeeeeeee ..... MUNGU nisamehe. Mambo ya "kupanda miti" kwenye TV ilikuwa too much to handle
 
I only hope sio kweli anakwenda kujifungua Marekani! Yaani haiwezekani Waziri wa Tanzania, Mgombea Ubunge, Mbunge aliyemaliza muda wake juzi baada ya kutoa ahadi za maisha bora sasa anakimbilia kwenda kwa wakunga wa Marekani. Yaani kumbe wanaojifungulia (kiswahili hiki!) hapa Bongo wananyimwa huduma safi!? Ni nani atakayemlipia huko!? Yaani tumefikia kiwango cha chini kiasi hicho hata huduma ambayo kwa miaka nenda rudi ilikuwa inatolewa kijadi na wamama zetu, inabidi mwenzetu apande ndege akapate mtoto ughaibuni. Huyo mtoto atapewa utaifa gani! Kwa madaraka aliyokuwa nayo, kweli angeshindwa kuweka mazingira mazuri pale Arusha au hata kwenye cliniki za manispaa ili itoe huduma hizo anazoziendea!

Huku wanadai huduma za afya zimeboreka, hata mioyo tunapasua, halafu huyu aende kuzzaliwa Marekani, ahaaaaaaaaaaaaaaaa nimechanganyikiwa sasa. Something is not just right for my country!
 
Labda anataka mwanae aweze kupata karatasi mbeleni:smow::smow:
 
Awali ya yote, mimi siko Arusha na hata huyu dada tunayemzungumzia simjui. Mimi hapa najibu mada kama ilivyoletwa kuwa wananchi wa Arusha hawamtaki kwa sababu mbalimbali mojawapo ikiwa ya kuolewa na mzanzibari. Ninachokisema ni kuwa, kama hivyo ni kweli, basi ile sumu ya lugha za kibaguzi zinazotalwala uhusiano wetu na Zanzibar imewasili bara! Ndio maana nikasema kuwa inaelekea hao wapiga kura wanaiona Zanziba kama nchi adui hadi kuona yeyote mwenye mahusiano nako ni adui. Sidhmchango mkubwa katika kukataliwa kwake kama hilo la kuolewa na mtu kutoka nchi isiyo kubalika. Mimi nimeongelea dini kujibu hoja ya Kanda2 kuhusu Ana Komu ambae sikujua kuwa ni mngazija au mtu aliyeritadi.

Sikubaliani na wewe kuwa kisa cha wakristu kuwa adimu katika uongozi Zanziba ni kutokana na demographics peke yake! Na hata huko Rombo, Peramiho, Moshi vijijini hivyo hivyo. Ukweli ni kuwa watu wengi wanapiga kura kwa kuangalia dini ya mtu hasa inapokuja kwenye local politics. Nawajua wakristu wengi tu ambao wako tayari kupigia kura jiwe kuliko huyo ambae wanamuona kuwa ni "mswahili". Zanzibar nako ukweli ni kuwa wengi hawako tayari kumpigia kura "kafir". Ukweli huu, ndio unaofanya wale wanaotoka kwenye minority religions kutojisumbua kugombea nafasi za uongozi katika sehemu wanazoishi. Hizo hesabu zako zina mushkel kidogo maana hakuna connection kati ya idadi ya watu na mwamko wao kisiasa. Wayahudi wako wachache marekani lakini mbona wanamwamko wa kuongoza na wanakubalika. Kama mtu kugombea kunategemea wingi wa kundi analofanana nalo basi hiyo ni dalili ya ubaguzi kuwepo.

Kuacha kuzungumzia udini, ukabila, ubaguzi wa rangi na maovu mengine yaliyo nchini yetu kwa kisingizio cha kuangalia "big picture" ni kuwa kama ostrich anaye fukia kichwa chake kwenye mchanga ili asionekane. Ingekuwa vizuri sana kama kila mgombea angeweza kupimwa kutokana na uwezo wake au ushawishi wake lakini bahati mbaya si hivyo. Jinsia ( uja uzito wa huyu dada ni moja ya ishu zilizoletwa hapa!), rangi, dini, uzawa bado zinachukua sehemu kubwa katika jamii yetu hata kama haipendezi. Kama alivyoandika Cornell West, " Race Matters". It still does. And religion and gender and all the rest of it!

Amandla.........

Umefanya utafiti wapi kudhihirisha haya? Kwamba ati watu wanapiga kura kidini? Au pengine wewe una mawazo hayo na unataka kuya-'generalize' kwa wote? Kama wewe ni fundi mchundo kweli (kama sio tu ID ya hapa JF) naamini utakuwa umefaulu hesabu kule O level, za kutosha kuelewa dhana rahisi ya 'probability', kwa hiyo sikutegemea upinge hili la probability. Nasisitiza kuwa sikubaliani na udini wako.
 
Hauwezi kuwazungumzia watu wote wa Arusha. Ushahidi ni wa huyu aliyeleta mada hii hapa ambayo anadai ni matokeo ya mazungumzo yake na watu wa Arusha. Ingawa si kitu tunachopenda kusikia lakini bado katika jamii yetu kuna wengi tu ambao watapiga kura kutokana na muangalio wa jinsia, dini, kabila na rangi. Si Arusha peke yake bali nchi nzima. Tunachoweza kufanya ni kuhakikisha kuwa mambo ya muhimu zaidi yanapewa kipaumbele lakini kujidanganya kuwa haya ya kipuuzi hayapo ni hatari mno. Hivi kweli, Mkuu, unataka kuniambia kuwa wabunge wote wanaokubalika ni kutokana na utendaji wao tu na hakuna chembe ya huyu ni wa kwetu? Huyu dada si the worst of the lot lakini bahati yake mbaya mambo mengi yamekutana kwake!

Amandla.........

Arusha mjini hatupigi kura kidini, hilo ushahidi upo. Hapo kabla mbunge wetu alikuwa Abdulrahman Kinana, mwislamu. Akafuatia Makongoro Nyerere, mkristo. Aliyemaliza muda wake majuzi ni Felix Mrema, mkristo. Wanaogombea sasa hivi wapo wa dini tofauti, na atachaguliwa mmoja mwenye dini mojawapo ambayo kwa ushahidi wa kihistoria wa hapa Arusha, dini haitamsaidia mtu kuchaguliwa. Kama watu wanamtaka mtu watampigia kura, kama hawamtaki atakosa bila kujali dini yake, tumekuwa tukifanya hivyo na tutafanya hivyo pia Oktoba 31 mwaka huu.
 
Sasa mimi nikajiuliza, kumbe mama akiwa mjamzito hafai kuwa mbunge? Lakini baadae nikagundua si suala la ujauzuto tuu, mama huyu wengi wa Arusha hawamtaki kwa sababu zifuatazo

1. Wanasema hawawezi kuongozwa na mtu aliyeolewa zanzibar
2. wengi kutokana na athari za mila hawataki kuongozwa na mwanamke
3. Tatu kuna habari zinazosambazwa kwamba mama huyu hafai kwa sababu si mtu aliye na historia ya kuwasaidia watu kama lowassa, na kuna upepo flani tuu unaolenga kuonesha mama huyu hafai.
Hiki ndio chama cha Demokrasia kinachoshikilia hoja za kibaguzi. Hii ni aibu. Tangazeni sera zenu-mtawafanyia nn Wanaarusha na sio kumkashifu mama wa watu. Kwani wewe mama yako asingeshika mimba ungezaliwa?Acheni mfumo dume.Hii inatufanya tufikiri mara mbili kuwapa kura niyi wahuni. Subirini mshangao Octoba 31.
 
Napata wasiwasi sana, na najiuliza mbona kama Tanzania tunaendekeza upuuzi namna hii? Watu wanauana Tarime kila siku hatuoni hata wanajeshi wakisema neno. Nakumbuka ulipoongezeka uharamia katika msitu uliopo kati ya Biharamulo na Kigoma wanajeshi walisema kazi yao si kulinda usalama wa raia bali mipaka ya nchi na waingilia kati kama jeshi la polisi litawaomba. sasa swali langu kwa sasa wameombwa na nani kuingilia mabo ya uchaguzi? yaani mwema na vibaraka wenzake wameshindwa kabisa? hata Tossi nlimuona amejikalia pembeni tuu anakodoa macho

Tossi atasema nini mbele ya mjeshi? Weee unataka apigwe makofi mwenzio!! au umesahau yaliyompata askari wa usalama barabarani kule Dar? wewe waache wanyamaze tu lakini mwisho wa yote ni tarehe 31 oktoba 2010. TUTAWASURUBU NA JAMAA YAO WASITUTISHE CHUKUA HATUA NDUGU!!!!!!! CHAGUA CHADEMA!!!!!!!!!!!!
 
batilda akalee familia, kutuongoza watu na akili zetu hawezi, haipati kura yangu na ya jamaa zangu kumi. kikwete naye alie tu.
 
Mazingira nchi nzima yanatia aibu.na yeye Batilda na NEMC wapo tu.sasa huyu leo anataka ubunge wa Arusha ili iweje.kuna taarifa za uhakika kwamba ile sekta ya mazingira imemzidi uwezo,anakurupuka tu na anawaogopa sana wahindi.Kwa ufupi mama huyu kama walivyo mawaziri wengi wa Vasco Da Gama hafai.
 
Magari yenye picha za JK akikaribiana na Dakitari Batilda huku yana vipaaza sauti yameteka jiji la Arusha katika hatua za purukshani za kumnadi kibosile huyu wa CCM ambaye yaeleka ataanguka vibaya kwenye chaguzi hii.

Wana-Arusha sasa hivi inabidi wavumilie sana uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na Waziri wa Mazingira wa kuchafua hali ya hewa kwa kelele za nyimbo za kukisifu chama cha CCM za John Komba pamoja na watangazaji wanaongea hovyo hovyo tu. Kelele ni uchafuzi wa mazingira wa hali ya juu na huko Kenya kuna sheria za adhabu ya kifungo au faini au yote mawili kwa kosa hilo lakini hapa bado ni "bora liende..."


Kama vile CCM hawajui kuwa "Chema chajiuza na kibaya chajitembeza" Mwanamama huyu kigogo katika wanamtandao wa EL anapambana kutetea ajira yake kwenye Baraza la Mawaziri bila ya kujua ya kuwa JK safari hii wanaishia wote mtaani.

Baadhi ya magari hayo ambayo kwa kawaida hujulikana kama "HIACE" yameacha kazi za kubeba abiria na kubuni shughuli hii mpya kinyume na leseni zao za biashara na hakuna lolote ambalo wamechukuliwa kwa kuwanyima abiria haki yao ya kimsingi ya usafiri.

Moja ya magari hayo limekuwa likiwalaumu wanawake kumtelekeza mwenzao Mama Batilda Buriani Salha wakati mpinzani wake Bw. Lema anamkashifu kwa kudai eti mimba yake inachezacheza tumboni. Mtangazaji adai Bw. Lema amefanya makosa ya kudhalilisha jinsia ya kike na wanawake ni vyema wakainuka na kumlalamikia!

Mtangazaji huyo ameendelea kulalama ya kuwa hivi umoja wa akina mama uko wapi kwanini hamshiki mabango na kumlalamikia Bw. Lema kwa kuwakashifu?

Nilimsikia mama mmoja akisema ..."hivi Batilda akipata yamaanisha wanawake wote tumepata au ni yeye na familia yake tu?"

Kwa kweli mtangazaji alipigwa butwaa na wala hakumjibu nafikiri hakutegemea ubishi mzito namna hiyo.

 
Kuanzia leo, Dakitari bingwa Mama yetu Batilda Buriani anayekiwania kwa udi na uvumba kiti cha ubunge Arusha mjini kupitia CCM, baada ya kuona sera zake haziuziki kama za bosi wake JK, naye sasa amekodisha kizazi kipya kutoka hapa nyumbani na majirani zetu wa Kenya ili kuvuta watu kwenye mikutano ya kampeni zake.

Tupo tunasubiri kuona kama na yeye atafunika kama bosi wake JK kule Songea mjini kwa kubebwa na kizazi kipya.
 
Chama kin a watu wapumbavu san a hiki...yaani mawazo Yao ni kuwa tunataka miziki
 
Wanadhani kuwa watanzania bado ni wale wa 47. Muziki watacheza ila kura wanajua watampa nani
 
ndio maana nasema , napata shida sana kuwaelewa watu wanaoiunga mkono ccm, huwa siwaelewi, kwakweli naona kukamtindio kaubongo kwa wengi kati ya wafuasi wao, nahisi tu jamani.
 
Back
Top Bottom