Kampeni ya Ubunge Arusha Mjini - Batilda Burian Vs Lema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni ya Ubunge Arusha Mjini - Batilda Burian Vs Lema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngongo, Aug 9, 2010.

?

KATI YA BATILDA NA LEMA YUPI ATIBUKA KIDEDEA?

 1. *

  LEMA

  86.5%
 2. *

  BATILDA

  11.5%
 3. MAHAKAMA ITATENGUA MATOKEO

  1.9%
 4. SIJUI MATOKEO

  1.9%
 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Wakaazi na wenyeji wa mji wa Arusha nchi yetu iko kwenye matayarisho ya uchaguzi mkuu October 2010.Nimeona ni vyema na haki tukawajadili wagombea ubunge wa vyama vitatu ambavyo nini hakika wataleta ushindani mkali.  Mgombea ubunge wa CCM
  Mama Batilda Salha Buriani kazaliwa mwaka 1965
  chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1985 – 1988 B.A [Public Admin & International Relation ]
  Mwaka 1990 – 1991 alichukua shahada ya pili katika chuo kikuu Sussex M.A [Development Studies]
  mwaka 1992 – 1997 alichukua shahada ya uzamivu [Phd] chuo kikuu London .
  Bi Batilda mpaka sasa ni waziri wan chi makamu wa Rais mazingira.

  Mapungufu yaMama Batilda Salha Buriani ni mengi lakini nitajaribu kuyatupia macho machache wengine mnaweza kuongeza kadri mnavyomfahamu.
  Bi Batilda Salha Buriani wakati akiwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Bunge na uratibu [ chief Whip ]aliwahi kumlima barua ya onyo kali Mama Anna kilango Malechela kwa kosa kubwa la kuzungumzia mradi wa Richmond bungeni.Hili ni kosa kubwa sana kwani baadae ilikuja kujulikana mradi wa RICHIMOND ulikuwa wa kifisadi,kwa maneno mengine Mama Batilda ni miongoni mwa wabunge/ mawaziri waliokuwa wakitetea ufisadi ndani ya serekali,bungeni na chama .

  Mama Batilda Salha Buriani kampeni zake ziligubikwa na rushwa na nguvu ya ajabu nyuma yake ilikuwa ikihakikisha anashinda tiketi ya kugombea ubunge kupitia CCM.Vyombo vya dola hasa UWT/TAKUKURU vilihakikisha hakuna wa kumzuia kushinda.Wakaazi wengi wa mji wa Arusha wanajua Mama B Salha Buriani alisaidiwa sana na Mbunge wa Monduli Bwana E N Lowassa kwa faida za kisiasa siku za usoni.Mama Batilda alihudhuria uzinduzi wa nyimbo za kwaya KKKT mwanzoni mwa mwaka huu,wengi tulijua alikuwa akijiandaa kugombea ubunge wa Arusha mjini.E N Lowassa mara nyingi amekuwa akimtumia Askofu Thomas Laizer kwa manufaa yake ya siasa kitu ambacho tayari kimeanza kulalamikiwa na waumini wengi wa KKKT.

  Mradi wa ujenzi wa barabara Arusha – Musoma kupitia mbuga ya wanyama ya Serengeti ni udhaifu mkubwa wa Mama Batilda Salha Buriani kama waziri anae shughulikia mazingira.Mama Batilda kaamua kukaa kimya pengine kufunika kombe mwanaharamu apite lakini akae akijua wakaazi wengi wa mji wa Arusha wanapata mapato mengi kwasababu ya utalii.Ujenzi wa barabara kupitia mbuga ya wanyama ya Serengeti kutaharibu mazingira pia kunaweza kusababisha uhamaji wa nyumbu kukoma kabisa.Inashangaza mtu wa aina hii anataka kuwa mbunge wa mji unaongoza katika shughuli za utalii Tanzania.
  Ikiwa Mama Batilda Salha Buriani atachaguliwa kuwa mbunge wa Arusha,hakika utakuwa ni ushindi mkubwa wa wanamtandao bila shaka nguvu ya wanamtandao itaongezeka maradufu.Mama Batilda atakuwa ni mbunge wa aliyempachika na wala hataweza kuwakilsha vyema wapiga kura wa Arusha mjini.

  Mgombea Ubunge wa CHADEMA
  Godbless Lema elimu yake haijulikani kabisa na ni moja ya mambo yaliyochangia kupunguza kura zake katika uchaguzi wa mwaka 2005.Anadai anacheti cha Computer lakini hatakia kutaja jina la chuo alichosoma wala mwaka aliomaliza.Anadai alimaliza kidato cha sita lakini hataki kutaja jina la shule aliyosoma wala mwaka na alama alizopata ??????????.
  Godbless Lema haijulikani anafanyakazi gani haswa, mara nyingi anapenda kujiita mfanyabiasha za madini na wakati mwingine anadai kununua vitu mbali mbali Dubai & Japan.Hana ofisi ya biashara inayojulikana muda wake mwingi anapenda kukaa mitaani kuzungumzia mambo asiyoyajua vyema kwa kujidai anayajua kuliko mtu mwingine.

  Godbless Lema ni dalali mzuri wa siasa za upinzani anajua kucheza karata zake vizuri sana huku akiyatanguliza maslahi yake binafsi.Bwana Lema anahusika bila shaka yoyote alifanikisha deal ya kumuondoa Diwani wa TLP Sombeti Bwana Mawazo na kumpeleka CCM kwa ujira wa pikipiki za mafisadi na kiwanja.Baada ya kutimuliwa TLP akakimbilia CHADEMA na amefanikwa kujinyanyua hadi akapitishwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA .wanamageuzi bado wanakumbuka jinsi alivyoiondoa kesi ya kupinga ushindi wa Mheshimiwa Felex Mrema mahakamani bila kuwashirikisha viongozi wa chama wakati chama kilitoa fedha za kugharamia kesi.Ilikuja kubainika Bwana Lema alipewa kitu kidogo ili kuiondoa kesi mahakamani.

  Godbless Lema akifaniwa kuwa mbunge wa Arusha mjini ataongeza idadi wa viti vya wabunge wa upinzani jambo ambalo ni jema na afya kwa demokrasia ya Tanzania lakini hatakuwa na mchango wa maana bungeni kama akina Dr Slaa na Zitto Kabwe sana sana ataongeza idadi tu.
  Godbless Lema anategemea zaidi umaarafu wa CHADEMA kuchaguliwa anatamani sana wapiga kura wasahau alivyorubuniwa na CCM mara mbili.
  [1] Kumpeleka Mawazo CCM.
  [2] Kufuta kesi ya kupinga ushindi wa Felex Mrema .
  [3] Atapenda wapiga kura wasihoji elimu yake.
  [4] Atapenda wapiga kura wasihoji kazi yake.
  [5] Atapenda wapiga kura wampigie kura kwasababu ya umaarafu wa CHADEMA na Dr Slaa.  Mgombea ubunge wa TLP
  Bwana Max Lyimo kazaliwa mwaka 1964
  Bachelor of Science Degree Chuo kikuu cha Dar
  Masters of Business Administration Chuo kikuu huria Tz

  Kuingia kwa Bwana M Lyimo kugombea ubunge wa Arusha mjini ni changamoto ambayo CCM na CHADEMA hawakutarajia hasa ikizingatiwa TLP katika chaguzi zote imekuwa ikileta upinzania mkubwa kwa CCM.

  Udhaifu pekee wa Bwana Lyimo ni kutojulikana na wakaazi wengi wa mji wa Arusha na vitongoji vyake,chama chake kinatakiwa kutilia mkazo mkubwa kumtambulisha hasa ikizingatiwa kuongezeka kata za Moshono,Olkeriani na nk pia cha cha TLP ambacho kilikumbwa na mgogoro tofauti na cha CHADEMA ambacho muda mwingi walikuwa wakikijenga chama kupitia operesheni Sangara.

  Bwana M Lyimo akichaguliwa kuwa mbunge wa Arusha ataongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni.Bwana Lyimo hatategemea umaarufu wa chama chake ambao haupo kwasasa.Nimemsikiliza Bwana Lyimo mara moja tu katika mkutano wake wa kujitambulisha eneo la soko kuu.Ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kujenga hoja.Anaweza kuwa mpambanaji kama akina Dr Slaa na zitto Kabwe.

  Nategemea michango na mijadala ya kujenga ili jimbo la Arusha mjini lipate mbunge makini,mwadilifu,mbunifu na zaidi ya yote mwenye kuangalia maslahi ya taifa bila kujali jimbo analoliwakisha.
  Naomba kuwasilisha
   
 2. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Acha kupiga kampeni kwani muda bado haujafika
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Nani kakwambia muda bado ????.kutafuata wadhamini ni sehemu ya kampeni,jaribu kuangalia TBC1 utakubali mwenyewe Muungwana kashaanza kampeni.Isitoshe nataka wakaazi wa Arusha na vitongoji vyake wawafahamu vizuri wabunge wao watarajiwa.
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Itakuwa mara ya kwanza jimbo la Arusha kuongozwa na mwanamke. Ikitokea basi, bila shaka Waarusha atakuwa wamebadili mila na desturi zao.
   
 5. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hongera Ngongo umeleta hoja ya maana sana.

  umesahau jambo moja muhimu sana kuhusu udhaifu wa batilda salha.kwanza kabadili dini ukubwani kwasababu ya mwanaume,huu nao udhaifu angekuwa na mtu wa msimamo asingebadili dini eti kwasababu ya kuolewa tu.Tumeshuhudia akina mama kibao wakiolewa na wakristo au waislam wakiendelea kuabudu dini zao.

  batilda ameolewa na kuachika mara tatu.Huu nao ni udhaifu kuachwa mara tatu ni doa kubwa sana.

  Batilda kaolewa Zanzibar ni kwanini asigombee huko alikoolewa au anataka kujifanya Anna kilango.

  Batilda ana uhusiano wa karibu usikuwa wa kawaida na lowassa
   
 6. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  CCM wamecheza karata mbovu sana hawajui jiji la Arusha kata za waarusha wa Arumeru zenye wakaazi wengi waarusha watapiga kura
   
 7. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  chadema wajinga sana wamekosa mtu wa kumsimamisha hadi kuangukia kwa tapeli Lema.Lema anajulikana ni mbabaishaji hana maana kabisa watu na akili zao hawawezi kumchagua mtu kwwasababu ya umaarufu wa chama.Nilitegemea operesheni sangara ingetupatia watu wasafi badala yake mnakimbilia magarasha ya Tlp
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Bahati nzuri nimefanikiwa kuonana na mdau wa mkubwa CHADEMA Arusha muda mfupi uliopita.Baada ya kumuuliza kulikoni kumteua mgombea mwenye shaka kibao.majibu aliyonipa yalinishagaza na kuniacha kinywa wazi.Kifupi anasema hata wao CHADEMA mkoa na wilaya wanashagaa jinsi Bwana Lema alivyojipenyeza kwa viongozi wa taifa na kuwaaminisha wamempata mtu makini {mtaji wa siasa].

  Wanajaribu kumweka mgombea wao wa mwaka 2005 ingawa bado wana wasiwasi wanaweza kuzua mgogoro kwasababu Lema tayari ameadvance sana.
   
 9. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,344
  Trophy Points: 280
  Thanks Ngongo for unbiased analysis, worth it to read.
  Tunaomba watu wengine kwenye majimbo walete tathmini zao bila upendeleo. Makala hii imejibu swali langu muhimu sana
  kuhusu Batilda, na sasa najua nguvu yake kisiasa ina back up gani.
   
 10. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0


  Kwa kampeni ya aina hii tayari umeshatuonyesha njia.......ujanjaujanja mwengine kwa jina la maslahi ya taifa!!!
   
 11. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi neno UNBIASED lina maana tofauti na ninayoijua mimi. Ni wazi hii ni propaganda ya mgombea mmoja dhidi ya wengine. This can even fit katika ushahidi wa kampeni chafu tunazopigia kelele, ofcourse pale wanapoguswa "watu wetu"....
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,344
  Trophy Points: 280
  Unbiased kwa sababu ametoa wasifu wa Matilda, elimu yake na nguvu zake kisiasa huku akiweka wazi uhusiano wake na EL.kwa mimi ninayeijua Arusha, sikuamini Felix kushindwa na Batilda. Ameeleza jinsi alivyomlima Kilango barua na ni kweli kwasababu wana ''bifu'' na sikujua bifu ilikuwa ni ya nini.
  Ameeleza elimu na uwezo wa mgombea wa CUF.
  Huyu wa Chadema hatujaona credentials zake, na kama yupo mtu anazo basi wekeni hapa tumfahamu, otherwise nisingependa chadema iweke mtu sehemu kama Arusha, mtu tusiyejua background yake.
   
 13. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Mkuu unajua kuna aina ya watu wasiotaka kuelewa wanapenda ligi ya ubishi utadhani kuna kikombe kinatolewa.

  Bwana / Bibi ngongo kaeleza kila kitu bila kuingiza ushabiki.Masahihisho kidogo ya Bwana Lema amemaliza kidato cha nne div 4 ya point 31
   
 14. R

  Ramos JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hebu acha kampeni za kitoto...

  Kwani nani haelewi kuwa Ngongo, Kabonde na Nguruvi3 wote mtu mmoja anajitahidi kuonyesha kuwa anaungwa mkono...
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Ramos,

  kwanza naomba nikupongeze kwa kuwa mtabiri mzuri,sijui lini umechukua kazi ya Sheck Yahaya ?????.
  Nilitegemea ungesoma niliyoeleza na kuja na mchango wa maana badala yake unaleta utoto hapa jamvini kuwa mtu mzima wacha ushabiki jadili hoja.
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sauti na makoti yao yanafanana, ama kweli duniani watu watatu watatu!
   
 17. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  unaelekea una chuki binafsi either na mama Batilda au CCM Chma kubwa
   
 18. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Imenisikitisha sana kusikia CHADEMA wamemsimamisha LEMA kama mgombea ubunge hapo Arusha.

  Hilo ni kosa kubwa kwa chadema katika mji huu wa Arusha..... NOOOOO PLZZZZZZZ... I think I can cry for this !!!
  Kama kuna muda changes ni muhimu sana la sivyo Chadema iunge mkono mgombea mwingine wa upinzani let say TLP Mr Lyimo !!!!
   
 19. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Nyuki,

  Mkuu wangu nyuki sina chuki na Mama Batilda wala CCM,nilichokifanya nikujaribu kuelezea wasifu wa wagombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini pamoja na vyama vyao.Hakuna mahali nilipomsingizia Mama Batilda zaidi ya kuonyesha jinsi alivyoshindwa kumudu majukumu yake alipokuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Bunge na uratibu alishiriki kwa nguvu na akili zake zote kuzima mjadala wa RICHMOND.Uliza wana CCM wenzake hawakatai sana sana watakwambia alishikizwa au tembelea hansad za bunge ujionee mwenyewe.

  Mradi wa ujenzi wa barabara Arusha - Musoma unapigiwa kelele na wanamazingira Tanzania na dunia nzima Mama Batilda ni waziri mwenye dhamana ya ulinzi wa mazingira lini na wapi ulimsikia akikataa ujenzi wa hii barabara inayokatiza ndani ya mbuga ya wanyama ya Serengeti.ujenzi wa Lodges & Hotels lazima upate kibali cha Mama Batilda leo hii mbuga zetu za wanyama ujenzi wa mahotel ni holela kuliko kipindi cha nyuma.

  Naomba tujikite kujibu hoja badala ya viroja.
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Lubaluka,

  Mkuu taratibu na keyboard yako angalia wasijekukwambia wewe na ngongo,kabonde na nguruvi3 ni mtu mmoja.

  JF ina baadhi ya watu hawataki kusikia wasiyoyapenda.Hakuna ubishi CHADEMA wamechemka kumsimamisha mgombea ubunge mwenye ??? kibao.Leo jaribu kuwauliza hata viongozi wa CHADEMA najua wapo kibao hapa watuambie elimu ya G Lema.Nakumbuka mwaka 2005 wakati Lema anagombea ubunge kwa mara ya kwanza ulifanyika ujanja wa kuweka picha kubwa bila maelezo ya uzoefu wa kazi na elimu CCM walipostukia Lema hana elimu waliamua kumshikia bango kwamba mtu asiekuwa na elimu atawezaje kuleta maendeleo ya elimu !.

  CHADEMA bado inaweza kumbadili Bwana Lema na kutuletea mtu mwingine anaefaa kama Bwana Mallah ambae nina hakika angeweza kuokoa jahazi kama haiwezekani basi hakuna haja ya kuendelea na udhaifu unaofahamika wazi kwa wapiga kura CHADEMA imuunge mkono mgombea wa TLP Bwana Lyimo ambae nyota yake inaanza kuchomoza vizuri.
   
Loading...