Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,373
- 37,910
- Thread starter
- #181
Nadhani ile ya ujauzito aliiongeza kuonesha chuki aliyokuwa nayo yule Bwana, Angalau nafurahi kwamba watu wa Arusha wameona wanahitaji mabadiliko japo sina uhakika na watakachofanya October 31. Jana nilikuwa terrat simanjiro, hali ni mbaya,lakini bado wamingangania CCM
Heshima kwako calnde,
Mkuu ujauzito ni issue kubwa Arusha labda mtashangaa kidogo.
wanawake wengi wanauliza kakaa bungeni miaka kumi kashindwa kuisaidia hospital ya mkoa akina mama wawili mpaka watatu wanalazimka kutumia kitanda kimoja.Wanamwona msanii hatakwenda akujifungulia Mt Meru Hospital ikitokea akenda atapewa special treatment.Mama Batlda alikuwa akitegemea kura za wanawake lakini wamemgeuka mpaka kachanganyikiwa.
Mama Batilda kafanya kosa kubwa kuitenga CCM wilaya kaamua kuunda timu yake ya kampeni nje ya utaratibu wa chama chake,wenye chama wamekaa pembeni wanamcheka.Leo nilibahatika kukutana na kiongozi wa CCM wilaya bila kuficha alionyesha kufurahia anguko la mgombea wao.