SUBIRA NA NGONGO MSIJIDANGANYE. MIMI NIKO ARUSHA MJINI NA HUWA NIKO SANA PEMBEZONI MWA MJI KWA UFUPI BATILDA ANA HALI MBAYA SAAANA. NA HAWEZI KUSHINDA LABDA UTOKEE WIZI WA HALI YA JUU SANA AU MUNGU MWENYEWE AAMUE ASHUKE.
NASEMA HIVI KWA SABABU NINA EVIDENCE
- NIMEHUDHURIA MMOJAWAPO WA MIKUTANO YAKE YA UFUNGUZI WA KAMPENI PALE SHULE YA MSINGI KIMANDOLU BAADA YA DK SLAA KUPITA. MKUTANO ULE HAUKUWA NA WATU ZAIDI YA 100 NA WENGI WALIKUWA WATAKA WASIKILIZE MZIKI WA MWANAMUZIKI WA BONGO FLEVA. MZIKI ULIPOISHA BATILDA AKAPANDA JUKWAANI NA WATU WAKAONDOKA AKABAKIA NA WENYE NGUO ZA KIJANI WASIOZIDI 50.
- JUZI JUMAMOSI TAREHE 16/10/2010 SAA 10. JIONI ENEO LA TINDIGANI KIJENGE JUU ALIKUJA NA DK. BILALI NA NILIKUWEPO. SUBIRI NA NGONGO MNGEKUJA MACHOZI YANGEWATOKA KWANI IDADI YA WATU ILIKUWA NUSU YA ILE YA MIKUTANO YA UBUNGE YA G. LEMA. UNFORTUNATELY NA WALIOKUWEPO WALILETWA NA HIACE ZISIZOPUNGUA 8
KUHUSU USAFI WA WAGOMBEA NI KWAMBA ALIYE SAFI KULIKO WOTE MIONGONI MWA SUBIRA, NGONGO, KILEO, BATILDA NA LEMA NA AWE WA KWANZA KUMRUSHIA MWENZAKE JIWE. AU WEWE UNAFIKIRI NI NANI?
Tusiwe na denials za wazi tuwe genuine katika argument zetu kwani ni jambo la wazi kabisa DK Batilda kuna kata hatapata hata kura 1000. Mikutano ya Batilda inajazwa na vikundi vya akina mama wanaojazwa kwenye Hiace na kuzunguka naye huku wakiwatukana wafuasi wa CHADEMA matusi kwa kuonyesha alama ya vidole. Mimi ni mmojawapo niliyetukanwa wakati nimejikalia tu nakunywa soda pale Kijenge kati. Batilda anapigiwa debe na wanywaji wa Dadii waliojawa na matusi tena wamama watu wazima wasio na mwelekeo.
Mara nyingi huwa naamini tabia ya wafuasi wa mtu inatoa taswira ya kiongozi wao. Kama walivyo hawa akina mama ambao hawana chembe ya soni wala staha.
Tathmini yangu inampa Batilda asilimia 15% ya kura za Arusha mjini lakini ya 85% au zaidi ni ushindi wa G.lema wa CHADEMA.
Subira na Ngongo kubalini matokea game limeisha hili msije pata pressure bure