Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,097
- 871
Halitakuwa jambo la kushangaza ukisikia Mwanasiasa Mrisho Gambo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia CCM akihamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Taarifa zilizotolewa na watu wake wa karibu zinaeleza kuwa, GAMBO ni kiongozi mwenye tamaa ya madaraka, asiyeaminika kwa sababu mara baada ya kutupwa nje ya Serikali na kutopendekezwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa kugombea Ubunge wa Jimbo la Arusha mjini mwaka 2025, alianza kujisogeza kwa GODBLESS LEMA na kuanza harakati za kushirikiana na CHADEMA kwa siri.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa,GAMBO ameahidiwa kupewa nyadhifa ya ndani ya CHADEMA Kanda ya Kaskazini na huenda akatumia Mkutano wa hadhara unaotarajiwa kufanywa na CHADEMA katika viwanja vya relini Arusha mjini tarehe 22/05/2026 kuhamia CHADEMA.
Itakumbuwa pia, kuwa hivi karibuni GAMBO alisifu kukua kwa Demokrasia baada ya LEMA kuongoza kufanyika kwa Mkutano wa CHADEMA hivi karibuni.
Soma pia Mrisho Gambo aonekana kwenye msiba wa mwasisi wa CHADEMA, Mzee Mtei