Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Mimi naona watu wamejielekeza au kumuangalia Magufuli tu, najiuliza hivi kabla hata ya Magufuli hatukuwa tukitakiwa kuwekewa hivyo vikwazo? Au wakati huo demokrasia ilikuwepo, kulikuwa na ushindani sawa wa vyama siasa na haki za binaadamu zilikuwa zinalindwa?
 
Hahahaha
Tunajua kukosa mkopo ni taabu ila wasitulazimishe kuwa watumwa wao. Walijipanga kuiongoza Tanzania kupitia vibaraka wao sasa wameukosa urais ishakua nongwa

Hawataki tuwaache wakae na pesa zao. Sisi tukitaka mikopo tutaenda kwa marafiki wa utotoni China hata Korea.....tutaokoteza okoteza lakini hatutakufa!

Na baada ya hapo wasitujue sisi wala mali zetu
Mwendo wa kupitisha vibakuli Tu mpaka tufike uchumi wa kati
 
Mimi naona watu wamejielekeza au kumuangalia Magufuli tu,najiuliza hivi kabla hata ya Magufuli hatukuwa tukitakiwa kuwekewa hivyo vikwazo? Au wakati huo demokrasia ilikuwepo,kulikuwa na ushindani sawa wa vyama siasa na haki za binaadamu zilikuwa zinalindwa?
Nadhani 2015 wakati wa JK ulikuwa hujazaliwa
 
Habari za mida wanajamvi!

Naam, kumepambazuka huko Duniani, wazungu wamesikia kilio cha wanao penda demokrasia Tanzania, kwa umoja wao wameazimia kuwa watainyima Tanzania misaada inayo fikia Tshs trilioni 1.64 kwasababu haifuati ustaarabu wa kidunia wa multipartism yaani demokrasia ya vyama vingi.

Kilicho nifurahisha zaidi ni kwamba , wanasema kama Tanzania ikiendelea kukaidi basi itawekewa vikwazo vya kiuchumi ISIFANYE BIASHARA NA NCHI YEYOTE YA ULAYA. HAPO SASA!!

Nini maana yake? Ni kwamba hatuta uza chai kwao, wala kahawa haitauzwa kwao, maua na mbogamboga kamwe hatutauza kwao. Hatutauza dhahabu, hatutauza korosho wala minofu ya samaki. Yaani hatutauza chochote kwao.

Baada ya muda mfupi tu fedha yetu itashuka thamani usipime. Yaani dollar moja yaweza kuwa Tshs 5000/= kisa? Mtu mmoja hataki uchaguzi uwe huru , wa haki, credible na transparent!

Wazungu nimewavulia kofia! Nimetabasamu kwa mara ya kwanza tangu October 28. Ahsanteni wazungu .bye
 
Mimi naona watu wamejielekeza au kumuangalia Magufuli tu,najiuliza hivi kabla hata ya Magufuli hatukuwa tukitakiwa kuwekewa hivyo vikwazo? Au wakati huo demokrasia ilikuwepo,kulikuwa na ushindani sawa wa vyama siasa na haki za binaadamu zilikuwa zinalindwa?
Wizi wa mwaka huu ni kufuru
 
Wagombanapo tembo ziumiazo ni nyasi

Hawa wafadhili wangewawekea vikwazo akina Mahera na wengineo lakini sio kuadhibu taifa lote ikiwamo na waliodhulumiwa haki zao
 
Hata sijui tumefikaje hapa. Labda kupenda sifa maana electoral College 270 zilitutosha kuendelea na mitano tena ila haya mambo ya kutaka kupata college zote ndipo shida ilipoanzia. Anyway, fedha zao poa na watunyime tu ila wasiiwekee vikwazo vya kuuza bidhaa kwao, itakuwa msala sana.
 
Haya mambo sio ya kushabikia kabisa kwa kuwa yanaweza kuwa na madhara hata kama uwe mpinzani, uwe mtawala, uwe mtawalia
Watakaomia zaidi ni mashabiki wa CCM acha akili ziwakae sawa mana wengi ni tegemezi nchi hii pia sio walipa kodi
 
Wizi wa mwaka huu ni kufuru
Kwahiyo utawala huu huu wa CCM kabla ya Magufuli haukuwa ukistahili kufanya Tanzania kuwekewa vikwazo? Kwa maana kama tungewekewa vikwazo katika kipindi cha Kikwete au Mkapa ungeona si sawa?
 
Bila kupoteza Muda naomba kwenda kwenye mada moja kwa moja,

Leo nilitenga muda wa kusikiliza kile kilichokuwa kinajadaliwa na Hawa Viumbe wa "EU" (External affairs), Kama tulivyo taarifiwa juzi katika vyombo vya habari vya kwao huko na baadhi ya nyuzi hapa JF.

Ila Nimesikitika Sana kuwa nilichotarajia kukisia kutoka kwao na nilichosikia ni Kama "Vatican na Saud Arabia" (quit different).

In summary; Hiki ndo nilitarajia kukisikia kutoka kwa hawa Nguri wa Hoja duniani;.

1.Uchaguzi wa 28Oct202.
Nilitajia kusikia maswali kama; Kwanini CCM imeishinda kwa asilimia kubwa vile kuliko vyama vingine?
Je baada ya Matokeo Wananchi waliopiga Kura hizo wameridhika na Matokeo Yao au hapana na Kama Ni hapana, Kuna ishara yeyote waliyoionyesha kutokubaliana na walichokichagua( Hapa Wapigiwa kura hawahusiki).
Je baada ya Matokeo wagombea nafasi wa upinzani walioshindwa waliyachukulia je matokeo, Kama Ni ndio sawa na Kama Ni hapana, je Kuna njia zozote za kisheria walizochukua kupinga Matokeo hayo ili kupata haki Yao(ukiondoa ya Matokeo ya urais).

2. Ukandamizwaji wa haki za binadam na Ugaidi;
Nilitarajia kusikia hoja Kama hizi kutoka kwao;
Kwanini msumbuji imeshindwa kuwathibiti Wana mgambo walioweka makazi kwenye nchi yao mpaka Wanasababisha maafa na kukandamizwa kwa haki za binadam nchi jirani Kama Tanzania(Mtwara Kama walivyotaja wao)?. Na Wala siyo kuilaumu Tanzania kisa inapakana na sehemu ambayo magaidi wapo. Nikweli EU hawajui kuwa Msumbuji ni nchi huru na ina mipaka na jeshi lake ambalo haliwezi ingiliwa na jeshi lolote lile pasipo ruhusa?.

3. COVID19.
Nilitegemea kusikia ni, njia gani ilizotumia Tanzania kuondokana na janga la Corona mpaka kufikia hatua ya watu wake kuendelea na maisha yao Kama kawaida bila vifo Wala athari yeyote?
Na wala siyo kulialia kwanini Tanzania haina Corona na tunaipatia pesa, Mara pesa za Corona zimetumikatumika je, Mara Sijui Nini ,
Hapa kwakweli imeonesha wazi kabisa jinsi gani mataifa ya ulaya yalivyo na wivu mkubwa juu ya Tanzania hasa katika suala hili la Covid19.

My take; Tanzania ni nchi yangu na Nina ipenda Sana na Sina shaka na Kiongozi wangu mkuu Yani "JIWE" juu ya kudili na Mabeberu naamini nachokiwaza mimi kuanzia Sasa na kuendelea ndo anachokiwaza Rais wangu. Hizi hoja za Leo niza kupuuza na kukaa kimya kabisa kana kwamba hakuna kilichotokea maana inaonekana watu wenyewe wamejadili huku mioyo yao ikiwa imejaa chuki binafsi na wivu juu ya Tanzania pamoja na kulialia pasipo kuwa na "deep Intelligences".

Na nilichokugundua Tangu tupate Rais jiwe kwelikweli Tanzania imekuwa femous sana ndani na nje ya Mataifa ya Ulaya. Na wanavyotenga muda wao kutujadili namna hiyo kwetu ni faida kubwa Sanaa maana Kupitia wao ndo wana tangaza na soko letu la utalii na kuwafanya watu wengi zaidi kuja Tanzania kujionea uteule wake.

Mfano; Suala la kututangaza juzi Kati kwenye media zao kuwa "Tanzania ndo nchi pekee dunian ambayo haina maambuzi ya Corona kwa takribani wiki46" na leo walivyosema kwenye mkutano wao kuwa, "tunawapa je Msaada Tanzania angali hawana Corona". Hii itaongeza idadi ya watu wengi Sana wa ulaya waliochoka na lockdown kuja kula maisha kwenye Peace land ya Tanzania huku soko letu la utalii likipanda siku Hadi siku.

#Mungu Mlinde Jiwe, Mungu tulinde Watz wote, Mungu ilinde nchi yangu.

#I love my country .

Wafanye watakalo lakini mambo ya familia yetu sisi watanzania wamwachia mamaTanzania
Hiyo misaada yenye masharti ndio inayoimaliza Afrika

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu John Pombe Joseph Magufuli
 
Ni ukurutu wa mawazo kushabikia vikwazo ndani ya ardhi unayotegemea kurithisha wanao. JPM hataishi milele.. Wajukuu zako hawataongozwa na yeye ila madhara ya vikwazo yataishi kwa muda mrefu mbele.
Vikwazo ni muhimu ili kukomesha ujinga.
Yani huyu kwa uroho wa madaraka inafikia hatua anatamani siku moja aamke akute tanzania imezama haipo tena.

Alivyo mjinga na mpumbavu anashindwa kutafakari je tanzania ikizama yeye atakuwa wapi?

Tamaa ya madaraka imemtoa ufahamu kabisa mbwa huyu.
Jaribu kufikiri, je kulikuwa na ulazima gani kupakia kura kwenye mabegi??
 
Hatua hii itafurahisha wengi hasa kwakuwa CCM imeligawa mno taifa hatuna umoja Tena madhila waliyofanyiwa wapinzani ndio yanaliumiza taifa kusema ukweli wale wote ambao kura zao ziliibiwa na wote wanaopenda demokrasia na walioumizwa na Mambo aliyofanyiwa lisu ben sanane azory mdude mbowe nk watafurahia hii hatua wataona huu ndio ushindi wao maana ule wa sanduku la kura umeporwa kimsingi ni jukumu la usalama wa taifa kuliponya taifa kwa kuchukua hatua za haraka anaeumia ni mama Tanzania Wala sio viongozi wa CCM. Hii ni habari njema sana no matter what kwa waliowengi.
Habari za mida wanajamvi!

Naam, kumepambazuka huko Duniani, wazungu wamesikia kilio cha wanao penda demokrasia Tanzania, kwa umoja wao wameazimia kuwa watainyima Tanzania misaada inayo fikia Tshs trilioni 1.64 kwasababu haifuati ustaarabu wa kidunia wa multipartism yaani demokrasia ya vyama vingi.

Kilicho nifurahisha zaidi ni kwamba , wanasema kama Tanzania ikiendelea kukaidi basi itawekewa vikwazo vya kiuchumi ISIFANYE BIASHARA NA NCHI YEYOTE YA ULAYA. HAPO SASA!!

Nini maana yake? Ni kwamba hatuta uza chai kwao, wala kahawa haitauzwa kwao, maua na mbogamboga kamwe hatutauza kwao. Hatutauza dhahabu, hatutauza korosho wala minofu ya samaki. Yaani hatutauza chochote kwao.

Baada ya muda mfupi tu fedha yetu itashuka thamani usipime. Yaani dollar moja yaweza kuwa Tshs 5000/= kisa? Mtu mmoja hataki uchaguzi uwe huru , wa haki, credible na transparent!

Wazungu nimewavulia kofia! Nimetabasamu kwa mara ya kwanza tangu October 28. Ahsanteni wazungu .bye
 
Back
Top Bottom