Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,634
- 46,278
Umoja wa Ulaya kwa kauli moja ya wanachama wote 27 wamepitisha kitita cha msaada wa Euro billion 50 kwa ajili ya Ukraine.
Orban wa Hungary aliyekuwa ameweka mkwamo wa pesa hizo kutoka kwa muda mrefu hatimaye amekubali kuondoa kura yake ya veto na kupelekea msaada huo kupitishwa .
Ukraine imekuwa katika ukata mkubwa baada ya Republicans kuchukua uongozi wa bunge la wawakilishi mwaka 2023 na kukata msaada wa serikali ya Marekani ambao ndio ulikuwa mkubwa zaidi. Hata hivyo Biden wa anajaribu kukiepuka kikwazo cha bunge la Marekani kwa kutumia sheria inayompa Rais mamlaka kuamua ni silaha zipi zimeisha muda wake na hivyo zinaweza kugaiwa bure au kuuzwa kwa bei rahisi bila ridhaa ya bunge.
Kwa hali hii vita ya Urusi na Ukraine bado ipo sana ikiendelea kwa muda mrefu sana kuliko ilivotarajiwa.