Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Haya mambo sio ya kushabikia kabisa kwa kuwa yanaweza kuwa na madhara hata kama uwe mpinzani, uwe mtawala, uwe mtawalia
 
Ila mkuu wakipiga pini hakuna rangi tutaacha kuona sisi wananchi, ni vyema wakiweza wangedili na hali hii bila kuumiza uchumi wa nchi. Tutaumia sisi huku walengwa wanakula maisha
Mkiumia mtaweza chukua hatua madhubuti kujinusuru.
 
Waandishi mnaojiita nguli hebu chambueni hii habari muitoe kulingana na tasnia ya habari inavyoelekeza.

Japo media za kibongo kwa sasa haziwezi kutangaza hii habari na hata zikitangaza, basi itakuwa ni kwa kugusigusia hewani tena kwa uoga mwingi ndiyo tulipofika na sio kosa lao.
 
ni kheri mara 1000 kutawaliwa kimabavu na mzungu tujue moja kuliko tena kutawaliwa kimabavu na mwafrika mtanzania mwenzetu. dah! aisee!
karne ya 21 mwafrika bado anawaza kutawala watu kimabavu!!!!!! laanahtuuullah afrika.
Nenda ukalime upate msosi usisubiri usodomanism wa Amsterdam ili akupe karo ya watoto wako
 
Ukiuwa upinzani wa ndani unakaribisha wa nje. Muhimu tupeleke mapolisi wakaue upinzani wa nje why mabeberu watuchezee sisi dona kantri
 
upambanie nchi wakati hujajiimarisha kudhibiti vikwazo watakavyokuwekea, mf wakikata misaada ya dawa za TB, ARV, MALARIA utapoteza ndugu wangapi katika ukoo wenu,, kwa sababu tu ya kuwatetea wachumia tumbo na familia zao,
Fikra zako bado ziko gizani hebu badilika unaonekane nimwelewa ila umelishwa matango pori hakuna mtu anaye mtetea mtu ila wewe ndo unashangilia nchi yako iamuliwe mambo na mabeberu na kuwaunga mkono
 
Eti laini laini wewe kwangu ni mwanamke mrembo kabisa zaidi ya Zuchu...
Ukianza matusi ni kuwa umeshindwa hoja, vijana wa Kikurya wa miaka hii mmekuwa laini laini sana na mmeacha kutumia bongo zenu vizuri. Kama huoni kuwa tulliba basi kacheki CPU yako mkuu
 
Watanzania wenzangu hapa ni kwamba haya yanayo endelea ni madrama wanatuigizia ni waambie tu wazi siku zote hakuna mtu atakupendelea mema ana taka uwe ombaomba siku zote wanaogopa tz itapiga hatua kubwa sana kwayo wanajaribu kutafuta sababu na kutuba ubaya ili watuandame tusikubali hata kido go kuonewa tuipambanie nchi yetu kwa umoja na mshikamano na hata Hivyo wangekua wanataka kuhukumu wangekuja kuchukua maelezo ya pande zote na si kusikiliza maneno ya kinasarungi peke yake kwani wanajulikana sio wazalendo wa kweli
Hata hivyo sisi ni matajiri Mbona tunaweza endesha nchi Kwa hela zetu
 
Ni ukurutu wa mawazo kushabikia vikwazo ndani ya ardhi unayotegemea kurithisha wanao. JPM hataishi milele.. Wajukuu zako hawataongozwa na yeye ila madhara ya vikwazo yataishi kwa muda mrefu mbele.
 
Back
Top Bottom