Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,789
- 52,756
Nakala Kwa Robert Heriel Mtibeli
Hizo sifa ni moja ya sifa muhimu wakati unachagua Mke.
Mke lazima awe na sîfa ya uzuri. Asije akakudanganya mtu.
Sifa zingine zikiwa constant
Nakala Kwa Robert Heriel Mtibeli
Ok mkuu nakubaliana na wewe asilimia 100%. Naomba nitangulize hofu ya Mungu kama kigezo cha kwanza , then IQ na vingine. Ila kuhusu uchawi ukichunguza zaidi kwa majirani na ndugu wa karibu wa binti wanaweza kukupa hint.Mkuu kama hujaoa nakupa pole, na kama umeoa na unadhani uko smart kwa wachawi unajidanganya na hujui kitu. Wachawi ni genge hatari na familia chache sana ziko free.
Inabidi nifunguke kidogo ili watu wengine wasiingie mkenge. Mimi mama (RIH) yangu alikuwa mchawi hiyo ni " rot in Hell".
Matatizo niliyopata hakuna sababu ya kuweka hapa.
Kilichonisaidia ni mimi kuwa mlokole na kuoa mke mlokole wa kumaanisha.
Sasa Mama alipokuja kuwanga kama kawaida yake siku hiyo yeye alimuona yaani walionana macho kwa macho.
Ila shida ataniambiaje mimi kwa mama mkwe mchawi. Ilichukua muda sana. Mimi na jirani yangu kulikuwa na kutoelewana ķuhusu mpaka na ikafika hatuongei mwaka mzima.
Sasa rafiki yake wife akaniambia anaeniletea matatizo ni mama yangu sio huyo jirani. Sikukubali wala kukataa. Niliamua kufuatilia kimya kimya.
Sasa mama alikuwa anakaa mbali na sisi, ila akija nyumbani lazima amchukue binti yangu anaenda nae kuoga. Yaani wanaoga wote uchi bafu moja. Mi nilikuwa sijui nakuwa kazini. Ndipo wife akanitonya kinachoendelea.
Mimi nilienda kwa wakubwa ambao hawamjui mama na nikatoa stori kama mhusika sio mimi wala faimilia yangu kutaka ushauri. Nikaambiwa huyo mama yangu sababu ameshakuwa mtu mzima alikuwa anatafuta mrithi. Hivyo mtoto mdogo akishazoea wakubwa kuwa uchi baadae akienda nae hatashangaa.
Sio hivyo tu alipata mama matatizo mengine ilibidi aende kwa siri kwa mganga alipelekwa na rafiki yake ambae sio mchawi. Akaja akagombana na huyo rafiki yake akimtishia kumpeleka polisi kwa wizi, kumbe aliyeiba ni ndg yake mama.
Sasa huyo rafiki yake ndio akatoa stori kwamba mganga alimwambia mama kwamba ajibu maswali ya ramli kama ni kweli ndio apate tiba.
Baadhi ya maswali ni pamoja na kula nyama za watu na viungo vya albino, ambapo mama alikubali.
Naishia hapo ila niko Free sasa mchawi mama ameshakufa.
Hakuna cha fununu mkuu.
Ila baada ya kushindwa kunitoa kafara ilibidi afe yeye mwenyewe kabla hajafa alimjia wife kwenye ndoto kumuaga kwamba anakufa. Wife baada ya kuota ile ndoto alimwendea mama nyumbani kwake na kumuambia ameota anamuaga. Mama akajibu ni kweli atak7fa muda sio mrefu.
Mama alikufa muda mfupi baada ya kuanguka akitokea chooni.
Kaa vizuri na Mungu wako Mkuu from experience ni vigumu kuwakwepa hawa watu. Tatizo wanaloga kote kote.
Mkuu ni sawa ndio maana hujalazimishwa. Ila mtoa mada amesema utamkumbuka baadae baada ya kufanya makosa. Kinga ni muhimu kuliko tibaKila mtu afanye kulingana na moyo wake unavyomtuma
MsitutisheMkuu ni sawa ndio maana hujalazimishwa. Ila mtoa mada amesema utamkumbuka baadae baada ya kufanya makosa. Kinga ni muhimu kuliko tiba
Mi nakushauri uokoke na uwe serious na wokovu.Ok mkuu nakubaliana na wewe asilimia 100%. Naomba nitangulize hofu ya Mungu kama kigezo cha kwanza , then IQ na vingine. Ila kuhusu uchawi ukichunguza zaidi kwa majirani na ndugu wa karibu wa binti wanaweza kukupa hint.