Usijidanganye, kwa uzuri wa umbo na sura yako TU huolewi ng’o!

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,885
5,374
Nianze kwa kusema kwamba nimewa-miss sana wasomaji wangu!Ni wiki moja tu tangu tumeachana lakini kwangu naona nikama mwezi hivi kwani nilitamani niwe nakutana nanyi kila siku kupitia safu hii ila kutokana na mpangilio wa mambo nilishindwa.Hata hivyo, niwahakikishie tu kwamba, kila wiki tutakapokuwa tunakutana utakuwa unapata dozi ya kutosha ambayo naamini kabisa itakuwa na uwezo wa kuyaweka freshi maisha yako ya kimapenzi.

Wiki iliyopita nilizungumzia juu ya matatizo ya wanawake wazuri na namna ya kuyakabili. Baada ya kuandika makala hayo, nilipokea simu kutoka kwa dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Juliety mkazi wa Arusha. Tulizungumza mengi lakini kitu ambacho mwenyewe alikieleza kuwa ni tatizo katika maisha yake ya kimapenzi ni kukosa mwanaume wakumuoa.

“Nina miaka 33 sasa kaka yangu, uzee unaninyemelea lakini sijampata mwanaume wa kunitamkia suala la ndoa, kila ninayekuwa naye na kuhisi anaweza kuwa mume wangu, baada ya muda hunitosa. Nimekuwa mtu wa kuchezewa tangu nilipokuwa na umri wa miaka 18, sijajua nina tatizo gani kwani kwa sura na umbo la kuvutia tu, Mungu kanijaalia,”anaeleza mwanadada huyo anayeonekana kukata tamaa ya maisha kwa sababu tu ya mapenzi.

Ndugu zangu, hakuna kitu kinachowachanganya wasichana wengi kama kufikia kipindi cha kuolewa na wakakosa wanaume wa kuwafanyia nusura. Inachanganya kidogo na wengine hufikia hatua ya kuhisi wamelogwa ama wana matatizo ambayo wanaume wanaokuwa nao huyabaini na kushindwa kutangaza ndoa.Kiukweli kabisa kila jambo anapanga Mwenyezi Mungu, wapo waliowahi kuolewa na kujiona wana bahati huku wakiwacheka wenzao ambao hawajaipata bahati hiyo lakini leo hii wameachwa na suala la ndoa limebaki historia kwao.

Wakati wao wakiingia katika ndoa na kutoka, wapo ambao wameolewa wakiwa na umri mkubwa na sasa wanaishi maisha ya furaha. Yaani walichelewa tu kuolewa na ndiyo maana tunasema kuwa, kuolewa ni suala la muda kwani kama hujapangiwa na Munguuolewe sasa, hata uende kwa waganga wala huwezi kuolewa. Wakati ukifika utashangaa mambo yatakavyokwenda ‘fasta’.Kwa mantiki hiyo basi unapohisi unastahili kuolewa lakini mwanaume wa kufanya hivyo akawa hajitokezi, si wakati wa kuchanganyikiwa, tulia na endelea kumuomba Mungu aweze kukujaalia na tena akupatie mwanaume mwenye sifa atakayeyafanya maisha yako kuwa ya amani.

Lakini wakati ukiendelea kufanya maombi ili na wewe uweze kutimiza ndoto yako ya kuitwa mke wa mtu au ‘Mrs flani’ jaribu kwanza kujiangalia na kujiuliza, je una sifa za kumshawishi mwanaume akuoe? Nasema hivyo kwa sababu unaweza kufanya maombi ili upate mume lakini kumbe hata ukifanya hivyo usiku kucha kuolewa ni miujiza, kwanini? Kwa sababu unakosa vitu flani flani vidogo ama vikubwa ambavyo vinakukosesha heshima yakuolewa.

Yapo mambo mengi ambayo yanaweza kukufanya ukakosa mwanaume wa kukuoa licha ya kuwa na umbo zuri na sura yenye kuvutia ila kwa leo nataka kuzungumzia suala moja kubwa ambalo ndilo limekuwa likiwafanya wasichana wengi kukosa wanaume wa kuwaoa.Tabia za mwanamke husika zinachangia kwa kiasi kikubwa katika hili. Waswahili wanasema, tabia njema kwa kila mtu ndiyo silaha madhubuti ya maisha, ukiwa na tabia nzuri na mwenendo wa kupendeza kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida.Lakini pia linapokuja suala la mwanaume kutafuta mwanamke wa kuoa kitu cha kwanza kitakuwa ni kujua tabia za binti husika. Ndiyo maana wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini bado wako ‘singo’, ukiuliza kwanini? Jibu litakuwa ni tabia zao ni mbaya kupita maelezo.

Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kuishi katika maisha ya upweke licha ya wao kutoridhika na hali hiyo. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea nao aliyeonesha kulidharau suala hilo la tabia.Si hivyo tu, wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, lakini matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo inasababisha kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.Haya ndiyo yanayonifanya nione kwamba, hakuna sababu ya mwanamke kujiuliza mara mbili mbili chanzo cha kutokupata mwanaume wa kumuoa, anachotakiwa kuangalia yeye ni je, tabia zake zinawavutia wanaume? Je, ni mtu anayeonesha mapenzi ya kweli anapokuwa na yule aliyetokea kumpenda? Je, anayajua maisha na mapenzi? Ni mtu asiyependa makuu na mpenda maendeleo? Hayo ni mambo ya msingi ya kujiuliza kabla ya kulalama mbele za watu kuwa, unataka mtu wa kukuoa lakini hujampata.

Yawezekana ukawa na vigezo vyotevinavyokufanya ustahili kuwa mke wa mtu lakini haijatokea hivyo, la kufanya hapo si kunung’unika na kumkufuru Mungu, kuwa mstahimilivu na vuta subira kwani yawezekana muda haujafika.Yaani uishi bila mume maisha yako yote, kwani umemkosea nini Mungu? Vuta subira kwani kila jambo lina wakati wake ila wakati unafanya hivyo jichunguze tabia zako ili hata hao watakaojitokeza kutaka kukuoa wasiwe na sababu ya kukutosa.

Ni hayo tu kwa leo
SOURCE: Grobal publisherz
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
8,343
Tatizo la wale wazuri wa kupitiliza ni msimamo. Unakuta anafuatwa na watu hata kumi at a time. Na wote mambo safi. Anashindwa kuchagua; anataka yote; matokeo yake anakosa yote. Wanaume wengi ukishamchanganya anakutoa kwenye kundi la kuoa.

Nina wadada nao wajua wazuri wenye misimamo na wala uzuri haukuwa kikwazo kwao kupata wenza. They knew what they wanted from a man and they stick to one relationship bila kuyumbishwa na mapedeghee.
 

BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,761
572
tatizo la wanawake ambao wanafuatwa sana na watu wao hujiona ni bora au wazuri lakini ndivyo sivyo matokeo yake wanahangaika kubadili wanaume kama nguo kumbe ukweli halisi ni tamaa zao za pesa au umaarufu hujikuta watu wanamfuata sana na hii anajikuta anashawishilka
 

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
ni kweli wakuu. Unajua kuna watu hawatumii maji ya bomba la chooni hata kama masafi kiasi gani! source matters quite alot
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
8,343
Stereotyping inaweza kukufanya ukakosa mambo ya maana. To me it doesn't matter kama article imeandikwa na Global au the Economist, kama ni garbage ni garbage kama ni nondo, ni nondo.

Ndo zile familia unakuta kila mtu ananunua magazeti ya udaku kwa siri kisa aibu kusoma udaku. Mtu ananunua daily news na hata asomi. Mi udaku nanunua sana na naweka juu ya meza ofisini na wala heshima yangu haijashuka kwa hilo.

Na ndio maana hawa wa haya magazeti wanatajirika. Nyumba moja wananunua magazeti kumi kisa usiri.

Ninunue daily news natafuta kazi?
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,765
104,921
Stereotyping inaweza kukufanya ukakosa mambo ya maana. To me it doesn't matter kama article imeandikwa na Global au the Economist, kama ni garbage ni garbage kama ni nondo, ni nondo.

Ndo zile familia unakuta kila mtu ananunua magazeti ya udaku kwa siri kisa aibu kusoma udaku. Mtu ananunua daily news na hata asomi. Mi udaku nanunua sana na naweka juu ya meza ofisini na wala heshima yangu haijashuka kwa hilo.

Na ndio maana hawa wa haya magazeti wanatajirika. Nyumba moja wananunua magazeti kumi kisa usiri.

Ninunue daily news natafuta kazi?

Utawaweza wabongo!
 

SnowBall

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
3,054
2,837
ni kweli wakuu. Unajua kuna watu hawatumii maji ya bomba la chooni hata kama masafi kiasi gani! source matters quite alot
Hebu angalieni 'contents' jamani..source sio issue sana almradi kilichoandikwa kina 'hold water'...
 

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,885
5,374
Kuna wa2 hawaangalii kilichoandikwa ni nini? Wanaangalia kimetoka wapi? Hata malaya anaweza kukushaur kuhus maisha! Si kama ndo malaya hawez kukuambia ki2.
 

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,885
5,374
Stereotyping inaweza kukufanya ukakosa mambo ya maana. To me it doesn't matter kama article imeandikwa na Global au the Economist, kama ni garbage ni garbage kama ni nondo, ni nondo.

Ndo zile familia unakuta kila mtu ananunua magazeti ya udaku kwa siri kisa aibu kusoma udaku. Mtu ananunua daily news na hata asomi. Mi udaku nanunua sana na naweka juu ya meza ofisini na wala heshima yangu haijashuka kwa hilo.

Na ndio maana hawa wa haya magazeti wanatajirika. Nyumba moja wananunua magazeti kumi kisa usiri.

Ninunue daily news natafuta kazi?

perfect
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom