Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,741
- 861,134
Akishakula hana uwezo wa kusogea hatua mbiliSasa wakienda kutinga chini ya kabati au sofa si watarevuka kabla hujawaona au kumuua
Akishakula hana uwezo wa kusogea hatua mbiliSasa wakienda kutinga chini ya kabati au sofa si watarevuka kabla hujawaona au kumuua
Dawa ipi mkuuNi kweli hata mimi huwa naitumia hiyo dawa wanakufa fasta halafu hawanuki utawakyta wamekaukaaa.
Asante kwa hii mbinu, nitajaribu kumtega kwa nyanya ila kama ana watoto namwonea huruma!
panya wengine wameshindikana
ninao paka3 na wako full patrol daily eneo lote..
sasa shida panya wanatembea juu ya bati na darini,hawashuki chin
leo nawawekea nyanya,indocid,valium na piriton kupunguza machungu
[emoji3]
Kuna siku panya kaingia kwenye kabati ya nguo niko na jamaa yangu tukaanza kupekura mule kabatini, pekenyua huku tunapigapiga bwana, yule panya si akatoka kwa spidi ya risasi.... Jamaa akaruka kwa mshituko [emoji3][emoji3] sasa kile kitendo cha kuruka ikawa ni kosa la jinai maana alimtimbatimba panya kapasukapasuka... Aisee siwezi sahau siku ile.
wewe wa wapiMlamu, panya wapo darini huko wewe unateseka na nini?
[emoji3][emoji23][emoji23][emoji23]sisi tulkua kama wanne hv tumejifungia na panya ndani tunawawinda wawil tu wakachomoka speed kali kila mtu alitafta pakutokea
haya mamuuzi ya kibabe sana mkuuuKuna panya anapekenya sofa ndani kwa ndani, hatoki nje nahisi hata nikimtega ni kazi sifuri... nimeamua kumpuuza nione kama atalimaliza sofa!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Labda mapanya ya Dar yaliyozoea kula kitimoto na mapaka kwenye bar.
Yale majanja hayalagi nyama zilizotegwa. Yatafanya kila yawezalo hata ikibidi kufungua friji na kula vilivyomo.
Watamaliza hakikaKuna panya anapekenya sofa ndani kwa ndani, hatoki nje nahisi hata nikimtega ni kazi sifuri... nimeamua kumpuuza nione kama atalimaliza sofa!
penye panya wengi hamna nyoka kivipi?Panya hujificha juu darini na kushuka chini kupata misosi au kuzaa/kulea.
Ukiiziba dari vizuri kwa singibodi au jipsam unakuwa umekata mzizi wa fitna.
Hapo akibaki juu lazma afe kwa njaa au ahame na akishuka chini unamkamata kilaini.
**Penye panya wengi ni salama zaidi, hamna nyoka hapo mahali.
Dawa ya panya ni paka tuJe umekuwa ukisumbuliwa na panya sana?
Je umetumia pesa sana kununua sumu za panya bila mafanikio?
Kama jibu ni ndiyo basi soma na ufanye hivi;
Nenda duka la dawa nunua dawa inaitwa INDOCID (indomethacin 25 mg capsules) halafu katege kama unavyotegaga sumu nyingine za unga za panya. Baada ya siku 4-5 matokeo utakayoyapata naamini mwenyewe utaleta mrejesho.
Dawa hii hutumiwa na binadamu kama dawa zingine tu ila kwa panya ni sumu kwani wakishakula utaona siku ya nne panya wanakufa na wengine wanashindwa kutembea kwa kusagika sagika mifupa.
Kama una jirani yako mshauri naye atumie maana muda mwingine waweza kuta unahangaika kumbe wanahamia kutoka nyumba ya pili.
Dawa hii inaepusha gharama kwani pakiti ya buku (tembe 10) unaweza tega mara kadhaa bila kuimaliza pia ni salama kabisa wakati wa kutega kwani siyo sumu kwa binadamu.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] wakikung'ata wanakupulizia kabisa usiamkeMkuu una bahati hao wako mbona wastaarabu. Kuna wengine wanakuvizia usiku mwingi umelala wanakula tartiiiiibu ile sehemu nyeupe nene ya unyayo wako.
Kuna wengine wadogowadogo sana anaingia kwenye begi anatengeneza uchochoro wa ndani kwa ndani kwa kula nguo kutoka upande mmoja wa begi hadi mwingine. Siku unataka mtoko unakuta kila nguo unayoitoa humo ina shimo mahali fulani.
Wiki iliyopita niliweka endocine na unga wa zembe panya walikufa wote kitu ambacho hakijawahi kutokea!
Ilikuwa nikiweka sumu za panya zingine hawafi wote ila safari hii nyumba imekuwa na amani