Kama unasumbuliwa na panya pitia hapa

Kama unasumbuliwa na panya pitia hapa

Naomba ufafanuzi mkuu si kwamba nyoka watakuwa wengi mana chakula chao kinapatikana kwa wingi?
Ni kweli nyoka hula panya.
Ukiona panya anakaa sehemu ujue keshajiridhisha hapo mahali hakuna nyoka. Ukiona sehemu haina panya chunguza utakuta lazma nyoka hawakosekani hapo.
 
Unaweka bila tahadhari? Ni uzembe wa hali ya juu na unaweza kuua hata binadamu wewe. Sumu ya panya inawekwa kwa kuhakikishia sehemu iliyowekwa haiwezi kileta madhara kwa mifugo au watu. Na pia unatoa tahadhari kwa familia nzima ili kila mtu ajue.
Tahadhari iliwekwa. Nikafungia mbwa na kuku ndani. Huyu mtoto kaamka sijui kajisahau au ni wenge. Kafungulia kuku. Kuna mambo yanatokea unaweza piga mtu ila unaishia kusonya tu.
 
Usirudie huo mchezo mkuu.

Ukiweka dawa ya panya hom usifanye siri watangazie kila mtu ajue na uweke wewe mwenyewe na uwahi kuamka asubuhi kutoa mabaki wewe mwenyewe.

Kumbuka hiyo ni sumu. Siku ingine utawamaliza binadam wenzio.
Nilitoa taarifa kwa kila mtu. Ila sijui dada alijisahau au ni wenge. Going forward nitafungia mpaka binadamu ndani hakuna kutoka mpaka mimi ndio nitoke wa kwanza....
 
Uhakika
JPEG_20200913_225830_8416245196665233042.jpg
 
Fuga paka ndugu, tena tafuta breed inayowinda na kula panya.

Kero yake kuu ni pale panya watakapo kwisha ndani kwako ataanza kwenda kuwinda nje kisha anakuletea mizoga ndani.

Pia anavyozidi kukua ataanza kuwa jeuri na mwenye tabia za porini.

Mbali na hapo, hili ndilo suluhisho la kudumu. Panya wako very smart, wakijua nyumba hii kuna paka basi wanahama kabisa.
Paka wa siku hizi hawali panya, sijui ndio Tom & Jerry zimewaharibu!![emoji2817][emoji2817][emoji2817]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu katika wanyama wabishi na wenye akili paka hawezi kukosa, paka ni mjanja sana unaweza ukamtegea sumu lakini ataenda atainusa na kuiacha kama ulivyoweka watu wanasema paka ana tabia ya kunusa ndipo uanza kula na iwapo utatega sumu basi utakuta kama ulivyoweka
Paka kwa Carbon/graphite ya kwenye battery hachomoi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli nyoka hula panya.
Ukiona panya anakaa sehemu ujue keshajiridhisha hapo mahali hakuna nyoka. Ukiona sehemu haina panya chunguza utakuta lazma nyoka hawakosekani hapo.
Lakini si baadaye nyoka si watakuja baada ya kugundua uwepo wa panya kama chakula chake?
 
Mimi alikaa kwenye sofa, anatoka usiku mchana anakausha unamsikia anavyohangaika.

Muda ukaenda akatanuka nakuongezeka size..... Kunasiku anatembea kwenye sofa namsikia anavyojipenyeza..... Aiseee nilipiga ngumi, vipepsi na mateke lile eneo alipo hadi akaanza kupiga ukunga....

Aisee nilitandika ngumi za maana hadi akatulia baada ya siku mbili nikaanza kusikia harufu ya mzoga nikajua tayari....

Nimecheka Hadi kulia aisee dah.hapana jamani
 
Back
Top Bottom