Kama unasumbuliwa na panya pitia hapa

Kama unasumbuliwa na panya pitia hapa

Je umekuwa ukisumbuliwa na panya sana?

Je umetumia pesa sana kununua sumu za panya bila mafanikio?

Kama jibu ni ndiyo basi soma na ufanye hivi;

Nenda duka la dawa nunua dawa inaitwa INDOCID (indomethacin 25 mg capsules) halafu katege kama unavyotegaga sumu nyingine za unga za panya. Baada ya siku 4-5 matokeo utakayoyapata naamini mwenyewe utaleta mrejesho

Dawa hii hutumiwa na binadamu kama dawa zingine tu ila kwa panya ni sumu kwani wakishakula utaona siku ya nne panya wanakufa na wengine wanashindwa kutembea kwa kusagika sagika mifupa

Kama una jirani yako mshauri naye atumie maana muda mwingine waweza kuta unahangaika kumbe wanahamia kutoka nyumba ya pili

Dawa hii inaepusha gharama kwani pakiti ya buku (tembe 10) unaweza tega mara kadhaa bila kuimaliza pia ni salama kabisa wakati wa kutega kwani siyo sumu kwa binadamu
Hii si dawa ya panya ni dawa ya mifupa ya binadamu......sasa basi panya anapoila inaenda kusagasaga mifupa yake mwilini ni mwishowe hufa ila inachukua kama siku mbili ivi kwa panya kufa.......njia nzuri ambayo panya hachomoki ni nyanya kata vipande vinne then chukua icho kidonge kipachue ule unga wake nyunyuzia kwenye majimaji ya nyanya nenda katege majibu utayapata tu wala usiwe na haraka.....
 
Kuna panya anapekenya sofa ndani kwa ndani, hatoki nje nahisi hata nikimtega ni kazi sifuri... nimeamua kumpuuza nione kama atalimaliza sofa!

so umeamua kumsusia sofa lako ...wewe kiboko... 😁 😁 😁 😁 😁
 
Mimi alikaa kwenye sofa, anatoka usiku mchana anakausha unamsikia anavyohangaika.

Muda ukaenda akatanuka nakuongezeka size..... Kunasiku anatembea kwenye sofa namsikia anavyojipenyeza..... Aiseee nilipiga ngumi, vipepsi na mateke lile eneo alipo hadi akaanza kupiga ukunga....

Aisee nilitandika ngumi za maana hadi akatulia baada ya siku mbili nikaanza kusikia harufu ya mzoga nikajua tayari....

mbona ulitumia nguvu kubwa hivyo ..kumbuka huyo kiumbe naye anafamilia
 
kipindi kile cha corona imechachamaa...niliweka sumu ya panya bahati mbaya nikapitiwe na kale kaugonjwa ka kupoteza uwezo wa kunusa au kusikia harufu...ebwanee walikufa panya kama saba hivi wakaozea ndani bila mm kujua kabisaaa
 
mi niliwekaga tu mtego wa gundi, walikoma wote hadi leo miaka miwili imeisha hawasogelei maskani
 
Mimi bado najiuliza yule Dereva wa daladala aliyenambia kua INDOSID nidawa kwa binadamu lkn pia nidawa nzuri sana kwakutibu MAFUA YAKUKU ..
hii idea niliipata toka March mwaka huu nikiwa kwene daladala nilipanda siti yambele,katka story story huyu dereva akanipa hii idea tena ikanibid niiandike kwene diary kabisa,kwabahati hadi leo sijaitumia.Duh kumbe ningemaliza tukuku twangu
 
[emoji28][emoji28][emoji1787][emoji28][emoji86]lazima ana watoto huyo

Ila udhaifu wa panya ni nyanya, pamoja na ujanja wake kwenye nyanya hachomoki
Mkuu sio kwelii.

Kama kwako kuna samaki na nyanya panya hapo sio mzalendo wa nyanya kiasi kwamba aache samaki ale nyanya.

Atakula samaki na nyanya utaikuta pale pale tu mkuu.

Ila ikiwa ndani kwako kuna ndoo,sufuria tupu na nyanya unadhani atakula sufuria aache nyanya ?
Atakula kilichokuwepo tu mkuu tena kwa shingo upande.

Mimi nna nyanya kwangu na wala hawazili
 
mkuu mimi kwangu kuna shida ya panya mmoja tu!
ubaya panya huyu anakula nyaya za umeme tu na soksi, nishatega nyanya, samaki nazikuta vile vile ila nikinunua soksi tu, yeye aichukua moja inabaki moja tu!

nifanyaje!
Panya mtu huyo
 
Nilikuwa naenda kununua dawa ya panya. Sijui nani kanituma nitembelee JF.

Kama ni kweli Basi naenda kununua sasa hivi hii dawa.
 
Nilikuwa naenda kununua dawa ya panya. Sijui nani kanituma nitembelee JF.

Kama ni kweli Basi naenda kununua sasa hivi hii dawa.
Ni dawa kweli jana nimeweka leo stoo kimya kabisa hakuna mishe mishe zao nasubiri harufu tu.
 
Hiyo Indocid ndugu utawapata wawili au watatu wa mwanzo tu, wakishajua umewatega hawalii! Ukitaka kuwakomoa vizuri wewe mwaga Ugoro tu kwenye njia yao au hata Nyoka kama wanakutembelea sana. Mwaga Ugoro tu uone kimbembe chake, panya, nyoka hawana Chafya.
Aisee hii mbinu ya kivita kabisa nimeielewa sana [emoji3]
 
Njia rahisi la kuwamaliza panya mtaa mzima au shambani kwa wingi hii utumika kuuwa malundo ya panya. Fanya hivi.
Nunua cement kilo moja, Mchele si zaidi ya kilo moja, vumbi la dagaa, au la samaki Kama huna saga dagaa au samaki wakavu.
Kisha vichanganye vyote na cement, then mchanganyiko huo uweke kwenye ungo au chochote kipana kisha wawekee maji ya kunywa.
Panya watafata harufu ya dagaa wakifika watavamia msosi wenye mix na cement, cement itawafanya wapate kiu watakimbilia kunywa maji, hapo watakuwa wamekoroga cement tumboni cement na maji uganda, ikiganda inaharibu digest sytem watarudi kufia mashimoni mwao. Hii dawa haina expired ni hadi panya wote mtaani watakaomba poa.
 
Back
Top Bottom