Kama unasumbuliwa na panya pitia hapa

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,212
2,808
Je, umekuwa ukisumbuliwa na panya sana?

Je, umetumia pesa sana kununua sumu za panya bila mafanikio?

Kama jibu ni ndiyo basi soma na ufanye hivi;

Nenda duka la dawa nunua dawa inaitwa INDOCID (indomethacin 25 mg capsules) halafu katege kama unavyotegaga sumu nyingine za unga za panya. Baada ya siku 4-5 matokeo utakayoyapata naamini mwenyewe utaleta mrejesho.

Dawa hii hutumiwa na binadamu kama dawa zingine tu ila kwa panya ni sumu kwani wakishakula utaona siku ya nne panya wanakufa na wengine wanashindwa kutembea kwa kusagika sagika mifupa.

Kama una jirani yako mshauri naye atumie maana muda mwingine waweza kuta unahangaika kumbe wanahamia kutoka nyumba ya pili.

Dawa hii inaepusha gharama kwani pakiti ya buku (tembe 10) unaweza tega mara kadhaa bila kuimaliza pia ni salama kabisa wakati wa kutega kwani siyo sumu kwa binadamu.
 
Je umekuwa ukisumbuliwa na panya sana?

Je umetumia pesa sana kununua sumu za panya bila mafanikio?

Kama jibu ni ndiyo basi soma na ufanye hivi;

Nenda duka la dawa nunua dawa inaitwa INDOCID (indomethacin 25 mg capsules) halafu katege kama unavyotegaga sumu nyingine za unga za panya. Baada ya siku 4-5 matokeo utakayoyapata naamini mwenyewe utaleta mrejesho

Dawa hii hutumiwa na binadamu kama dawa zingine tu ila kwa panya ni sumu kwani wakishakula utaona siku ya nne panya wanakufa na wengine wanashindwa kutembea kwa kusagika sagika mifupa

Kama una jirani yako mshauri naye atumie maana muda mwingine waweza kuta unahangaika kumbe wanahamia kutoka nyumba ya pili

Dawa hii inaepusha gharama kwani pakiti ya buku (tembe 10) unaweza tega mara kadhaa bila kuimaliza pia ni salama kabisa wakati wa kutega kwani siyo sumu kwa binadamu
Hii ndo natumia siku zote kuulia panya
 
Fuga paka ndugu, tena tafuta breed inayowinda na kula panya.

Kero yake kuu ni pale panya watakapo kwisha ndani kwako ataanza kwenda kuwinda nje kisha anakuletea mizoga ndani.

Pia anavyozidi kukua ataanza kuwa jeuri na mwenye tabia za porini.

Mbali na hapo, hili ndilo suluhisho la kudumu. Panya wako very smart, wakijua nyumba hii kuna paka basi wanahama kabisa.
 
Kuna panya anapekenya sofa ndani kwa ndani, hatoki nje nahisi hata nikimtega ni kazi sifuri... nimeamua kumpuuza nione kama atalimaliza sofa!
Mimi alikaa kwenye sofa, anatoka usiku mchana anakausha unamsikia anavyohangaika.

Muda ukaenda akatanuka nakuongezeka size..... Kunasiku anatembea kwenye sofa namsikia anavyojipenyeza..... Aiseee nilipiga ngumi, vipepsi na mateke lile eneo alipo hadi akaanza kupiga ukunga....

Aisee nilitandika ngumi za maana hadi akatulia baada ya siku mbili nikaanza kusikia harufu ya mzoga nikajua tayari....
 
Back
Top Bottom