I believe this is a misconception. Tulipokea "mfumo wa utawala bora" kutoka wapi? Utawala bora ni "mfumo wa kimagharibi"? Kwamba ni kosa kwa kiongozi wa umma kupokea kickbacks kutoka kwa wafanyabiashara nchini Hispania au Marekani lakini ni sawasawa hapa Tanzania? And what is the alternative to good governance?
Unadhani mfano wako unakidhi dhana yangu kuhusu ninavyotazama utawala bora? Mbona unauzungumzia utawala bora katia dhana ya chini kabisa wakati utawala bora ni dhana pana? Unataka kuniambia kuna uhusiano wowote kati ya wizi na utawala bora au unataka kusema hicho ndicho hasa nimemaanisha? Suala la wizi na/ama ufisadi linaangukia kwenye suala zima la maadili na ndio maana nikazungumza mapema kwamba ni utani nchi ama jamii isiyo na maadili ku-practice utawala bora, kwa sababu, under this context, one of the main sub-pillar ya utawala bora ni utawala wa sheria na katika utawala wa sheria, mtu atabaki kuwa mtuhumiwa hadi inakuwa proved beyond reasonable doubt kwamba ametenda kosa analotuhumiwa nalo!
Tuje kwenye shaka yako kuhusu ikiwa Utawala Bora ni mfumo ambao tumekuwa nao tangu enzi na enzi au vinginevyo! Ina maana unataka kusema we'd this system since then? Are you serious? Hivi bara ambalo kiasi kikubwa cha viongozi wake walikuwa ni wale waliongia madarakani kwa mapinduzi unataka kusema walikuwa wana-practice utawala bora? Hivi bara ambalo hata uhuru wa maoni haukuwapo(na in fact bado haupo) unataka kuniambia lilikuwa lina-practice utawala bora? One of the main pillar of Utawala Bora ni Institutions ambapo msisitizo ni pamoja na transparency and fairness! Did we had, and in fact, do we have transparency and fairness; them being one of the main pillars of Good Governance? Hivi bara ambalo hata uhuru wa mahakama haukuwapo, na in fact, bado haupo wakati another pillar of good governance ni Law & Jurisdiction... hivi bado unaamini Africa lilikuwa lina-practice utawala bora since then? Unahoji ikiwa Utawala Bora ni mfumo wa Magharibi, je bado unaamini ni mfumo ambao tulikuwa nao kabla au labda unataka kumaanisha ulikuja kutoka East?
Alternative to Good Governance... oh, nimeshaandika sana kuhusu hilo kwahiyo naona uvivu kurudia but only I can say ni kwamba, Utawala Bora ni Mfumo Bora kwenye Jamii yenye Maadili Bora na kinyume chake ni disaster!
Wakati wa utawala wa Mwl. Nyerere, ilikuwa ni mwiko kwa kiongozi wa serikali kuwa mfanyabiashara. Lengo ni kuondoa "conflict of interests" na kuchochea utawala bora. Je, Mwl. Nyerere alipokea miiko hiyo kutoka nchi za Magharibi?
Hakuna uhusiano wowote kati ya ufanyaji ama kutokufanya biashara na suala zima la utawala bora, isipokuwa kama ulivyotangulia kusema, ufanyaji biashara kwa kiongozi wa umma kuna direct effect na conflict of interests na ndio maana, kwenye baadhi ya nchi, mtu anapokuwa kiongozi wa umma si kwamba anaambiwa acha au ufilisiwe kwamba bali biashara husika zitawekwa chini ya muangalizi maalumu! Katiba ya nchi inaweza kukataza viongozi wa umma kutofanya biashara kama ilivyokuwa kwa nchi nyingi za Kikomunisti lakini sidhani endapo miongoni mwao ipo inayoweza kujigamba kwamba ilikuwa ina-practice utawala bora! Kwahiyo ambacho kilikuwa under Nyerere Leadership ni kukataza viongozi wa umma kufanya biashara kitu ambacho hakina uhusiano na utawala bora! Rejea Five Pillars of Governance.
Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Tume ya Warioba imezungumzia mambo kama kiongozi kuwa na account nje ya nchi au waziri kuwa mbunge. Lengo likiwa kuweka mazingira yatakayochochea utawala bora. Je, hatupaswi kufanya hivyo kwa kuwa tutaonekana tumepokea "mifumo ya kimagharibi kama mazuzu"?
Yote hayo hayana uhusiano na Utawala Bora.
In fact, utawala bora is not about copying stuff from the West. It is about protecting basic human rights everywhere in the world. Nyerere alisema ili nchi iweze kusonga mbele, tunahitaji watu, ardhi, siasa safi,na uongozi bora. Kwa kufanya hivyo, hakupokea "mifumo ya kimagharibi kama zuzu".
Utawala Bora is more than protecting human rights everywhere but at least you've nailed some of it!
Na utawala bora/maadili hauhitaji "proof beyond reasonable doubt". Ukishakuwa implicated, unapaswa kuwajibika na hatua nyingine kufuata baadaye.
Sijui kwanini umeandika utawala bora kisha ukaweka slash maadili manake kwa tafsiri ya haraka haraka ni kama una maanisha utawala bora na maadili is one and the same but let's ignore this petty stuff na badala yake nirukie hapo unaposema:"Na
utawala bora/maadili hauhitaji "proof beyond reasonable doubt." Msisitizo kwenye RED!
Utawala Bora una misingi mikuu mitano, mmoja wapo ni Laws & Jurisdiction. Ndani ya Laws & Jurisdiction kuna Rule of Law, yaani Utawala wa Sheria! Unaposema utawala bora hauhitaji proof beyond reasonable doubt isipokuwa Ukishakuwa implicated, unapaswa kuwajibika na hatua nyingine kufuata baadaye...kwanza, upo sahihi kwa 100% lakini kwa upande mwingine unachanganya mambo! Upo sahihi kwa 100% kwa maana kwamba ni kweli ukishakuwa implicated unatakiwa kuwajibika lakini kuwajibika huko hakumaanishi kwamba umetenda kosa unalotuhumiwa... ni hadi ufikishwe mahakamani, na mahakama i-prove beyond reasonable doubt kwamba umetenda kosa unalotuhumiwa ndipo unaweza kuitwa mwizi, fisadi, tapeli na majina yote unayofahamu wewe hususani yale yanayochukiza!!! Hivyo basi, hapo ndipo unaposimama msingi wa hoja yangu!!!
Mosi, tuseme wote wanaotuhumiwa wanawajibika (hatua ya kwanza); ni mahakama gani ita-prove beyond reasonable doubt kwamba tuhuma dhidi ya hao jamaa ni sahii? Kuweza ku-prove beyond reasoable doubt, pamoja na mambo mengine, panapaswa uwepo wa uchunguzi wa kina kuthibitisha madai husika! Uchunguzi huo bila shaka utafanywa na watu wale wale kutoka jamii ile ile ambayo wenzao, tena wakiwa na majina makubwa kabisa na yenye kuheshimika bado majina yao yanaonekana kwenye orodha ya watuhumiwa! Ili mahakama ipate ku-prove beyond reasonable doubt, bado tunahitaji majaji waadilifu kabisa ambao tunatarajia watoke kwenye jamii ile ile ya hovyo hovyo!!
Matokeo yake ni nini? Ndipo pale Waendesha Mashitaka wanapokata shauri la kubadilisha aina ya mashitaka, na badala ya kufungua mashitaka ya wizi au ufisadi, wanalazimika kufungua mashitaka dhidi ya matumizi mabaya ya ofisi/madaraka kwa sababu wanafahamu fika kwamba wakifungua mashitaka dhidi ya ufisadi, watashindwa kuthibitisha beyond reasonable doubt (Rule of Law ambao ni sub-pillar ya Good Governance)! Matokeo yake, ndipo unakuta mtu ambae alikuwa na tuhuma za kufidi billions of money, anaishia kwenda jela miaka miwili... Refer Lyumba's case!!!