Kafulila,Tibaijuka live Star TV

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,525
2,000
Angali star tv muda huu uwasikilize hawa waheshimiwa wakijadili sakata la IPTL.

Waziri Tibaijuka anadai yeye alikuwa middle man katika upokeaji wa hiyo hela kama mchango kwa ajili ya shule na alilazimika kufungua account Mkombozi bank ili kukiza mashariti ya mtoa fedha kwani alitaka anaehitaji hiyo hela awe na account katika hiyo bank.

Kafulila pia ametoa ushahidi wa barua ya Lugemalila kwenda kwa Gavana ikimtaka Gavana asitoe hela mpaka kwanza yeye Lugemalila alipwe hela yake lakini BOT ilitoa hiyo hela kabla ya Lugemalila kulipwa hela yake ambayo ilikuwa ni dola milioni 67 kitu ambacho ni kinyume cha sheria.

Eti mama anasema nchi kukosa misaada ni kutokana Kafulila kuibua swala hilo.

Kwa kifupi,mama hana hoja na kwakweli amepanic na anaumbuka tu.
 

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,126
2,000
Tibaijuka anase JR ni kaka yake, amelipa kodi hana shida kunigawia.

Anasema yeye ni waziri wa ardhi hahusiani na nishati.
 

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,139
1,250
Masikini unajua wamemwita Mama wa watu bila kumwambia kuwa na Kafulila atakuja!!
Hhahaha! Dah STAR TV noma sana!

Halafu wa washe AC, mama wa watu anazidi kutoa jasho tu halafu kashkaji kametuliaaaa!
 

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,126
2,000
aliikuwa wa kwanza kwenda press conference kutangaza kupewa mgawo
 

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,139
1,250
Mh, nataka kuripoti bila ushabiki ila sitaweza bandugu. Naomba tu mwingine ajaribu.
Tibaijuka anaongea kwa kigugumizi cha mtu muongo sana. Halafu ni dhahir kuwa huyu mama hajazoea uongo!

Ka Kafulila sijui kanajiamini nini maana kana confidence hapo pembeni na kanamwangalia mama huku kakijua kabisa anadanganya.

Mama anasema, Rugemalira ana haki ya kuuza hisa zake, na alipewa yeye 1.6 kwa ajili ya shule. Ruge account iko Mkombozi, na account ya shule haiko mkombozi, hakutaka kusumbuka kuhamisha hela hivyo akaamua kupitisha kwa mama Tiba kama mmoja wa viongozi wa shule.


Kafulila anasema, Prof anavosema aliahidiwa kupewa hela bila kujua kiasi inatia shaka maana 1.6 billion ni hela nyingi sio tu TZ lakini dunia nzima. Kupewa tu dolla mill 1 bila taarifa inatia shaka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom